Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 2 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 28 | 2023-08-30 |
Name
Taska Restituta Mbogo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TASKA R. MBOGO, aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Mkongo wa Mawasiliano katika eneo la Sikonge hadi Inyonga?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI, alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kuwa ni muhimili wa mawasiliano hapa nchini. Katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 Serikali imepanga kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuanzia Tabora – Sikonge – Inyonga – Majimoto – Kizi wenye urefu wa Kilomita 369.
Mheshimiwa Naibu Spika, Hadi sasa Serikali kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imesaini mkataba na Mkandarasi kwa ajili ya kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika maeneo hayo. Hatua za utekelezaji zimeanza ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2024.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved