Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Taska Restituta Mbogo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TASKA R. MBOGO, aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Mkongo wa Mawasiliano katika eneo la Sikonge hadi Inyonga?
Supplementary Question 1
MHE. TASKA R. MBOGO : Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwanza naipongeza serikali kwa kutufikiria kujenga Mkongo wa Taifa kutoka Sikonge mpaka Inyonga.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutoka Sikonge, Ipole, Inyonga mpaka Mpanda hakuna mawasiliano, Mkongo wa Taifa unaoenda kujengwa unatoka Inyonga kwenda Majimoto mpaka Kizi. Kutoka Inyonga kwenda Mpanda kuna kilomita 130, hapana mawasiliano na ni hifadhi ya Taifa;
Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga Mkongo wa Taifa katika eneo hilo?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwenye Mkoa wangu wa Katavi kuna vijiji ambavyo mawasiliano ni duni. Kwa mfano Kijiji cha Bujombe Wilaya ya Tanganyika na Kijiji cha Mapili kata ya Ilela. Kuna ahadi yako Mheshimiwa Waziri ulisema utaweka Mkonga wa Vodacom;
Je, ni lini utatimiza ahadi yako?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Restituta Mboga kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kutoka Sikonge kufauta ile barabra ya lami, sehemu kubwa ya eneo lile halina huduma ya mawasiliano. Serikali kupitia TTCL tumefanya tathmini na tumekusudia kuweka minara mitatu mpaka minne kwenye hilo, eneo ili hilo eneo lipate mawasiliano. Tunajua lipo tatizo kubwa la watu kusafiri hasa wakati wa usiku kwa sababu ya kukosa mawasiliano. Tumeshaweka utaratibu na tumefanya tathmini. Wakati tunajenga huu Mkongo na nguzo za mawasiliano zitawekwa kwenye haya maeneo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kule alikokutaja kwenye kijiji tunafanya tathmni upo mnara karibu na hiki kijiji tuone kama ukiongezwa nguvu tuone kama unaweza kuhudumia eneo hili. Lakini lile eneo ambalo nilitoa hadi kwmba tutaweka mnara Vodacom kwenye ile minara 758 kuna mnara mmoja ambao unakwenda kujengwa kwenye hili eneo. Hatua za awali za manunuzi zimekamilika vifaa vipo njiani vinakuja na ujenzi utaanza mara moja kwa ajili ya kutoa huduma kwenye eneo husika.
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. TASKA R. MBOGO, aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Mkongo wa Mawasiliano katika eneo la Sikonge hadi Inyonga?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ningependa kuiuliza Serikali, wakati tunasubiri utekelezaji wa mikataba iliyosainiwa mwezi Juni, je, kuna mpango gani wa kuongeza nguvu minara ambayo ipo, ambayo ina nguvu ndogo sana inayotoa mawasiliano kwenye maeneo madogo sana?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kakunda kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bajeti iliyopitishwa hapa Bungeni ya mwaka 2023/2024, bajeti imepitishwa ya kuongeza nguvu ya minara 388 kwa ajili ya kuiongezea nguvu kama ambayo Mheshimiwa Mbunge ametoa ushauri. Naamini maeneo anayoyataja yanaweza kuwa sehemu ya hii 388 na kama hayamo, bado kuna fedha nyingine kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuongeza uwezo wa minara ambayo tunayo ili tuachane na huduma ya 2G tuende kwenye 3G, 4G na sasa 5G.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved