Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amina Daud Hassan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA DAUD HASSAN aliuliza:- Je, Serikali inatambua uwepo wa rushwa kwa wanafunzi katika vyuo vyetu hapa Nchini?

Supplementary Question 1

MHE. AMINA DAUD HASSAN: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali ni vigezo gani ambavyo vinatumika kwa wanafunzi wengine wachache ambao wamefanya vizuri kuachwa na kuchukuliwa wanafunzi wengine ambao wamefanya vibaya?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, samahani, sijaelewa swali lake.

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika.

SPIKA: Maana nahisi lile linahamia kwenu kwa sababu linahusu wanafunzi vyuoni, kwa nini wanaachwa waliofaulu wanachukuliwa waliofeli? Kama siyo rushwa.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kama nimeelewa swali lake, nili-frame vizuri ili niweze kulijibu. Kama anasema kwamba kuna wanafunzi wameomba kujiunga na chuo halafu kuna ambao wamefaulu zaidi wameachwa lakini ambao wamefaulu kidogo wakachaguliwa, maelezo yake yanaweza yakawa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, moja, unaweza ukawa umefaulu vizuri sana lakini course uliyoiomba wewe ina ushindani mkubwa zaidi kiasi kwamba waliofaulu kuliko wewe wamechukuliwa lakini course nyingine ambayo ungeomba ungeuipata hukuiomba wewe, halafu mtu ambaye hakufaulu kama wewe akaomba akaipata.

Mheshimiwa Spika, lakini ili kuhakikisha kwamba kuna haki wakati unapoomba kujiunga na chuo tunatangaza majina ya waliyoomba, tunatangaza marks zao, tunaonyesha cut off kwa kila program. Ili endapo unaona ulikuwa umefikia cut off kwenye course uliyoiomba na hujachukuliwa unaruhusiwa kulalamika na sisi tutafuatilia uingie chuoni na waliofanya hivyo wachukuliwe hatua mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, suala muhimu ni kuhakikisha kwamba unapoomba kujiunga na chuo ujue ile program unayoiomba angalia kwa mfano mwaka jana cut off ilikua kiasi gani. Unaweza ukawa umepata first class umeomba kusoma sheria University of Dar es Salaam lakini University of Dar es Salaam inachukua first class yenye point chache zaidi kuliko ulizoomba wewe. Halafu ungeomba kwenda kusoma course nyingine pale pale University of Dar es Salaam ungechaguliwa lakini hukuomba halafu mwenye marks kidogo kuliko wewe, point kidogo kuliko wewe kaiomba ile kachukuliwa. Hiyo inaweza ikaonyesha kana kwamba pengine aliyefaulu vizuri hakuchukuliwa lakini kwa sababu ya choice uliyoifanya.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunashauri kila anayeomba kwenda kusoma aangalie matokeo. Kila kitu kipo kwenye website, anaweza akajua kama nikiomba course hii ni vipi naweza nikapata kuingia, nashukuru sana. (Makofi)

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA DAUD HASSAN aliuliza:- Je, Serikali inatambua uwepo wa rushwa kwa wanafunzi katika vyuo vyetu hapa Nchini?

Supplementary Question 2

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, ahsante, Mamlaka ya Usimamizi wa Mitihani Vyuo Vikuu kuwa chini ya Wahadhiri imekuwa ni miongoni mwa sababu ya rushwa ya ngono vyuo vikuu. Sasa ni kwa nini sasa Wizara isione umuhimu wa kushirikiana na Wizara ya Elimu kuondoa Mamlaka ya Usimamizi wa Mitihani kwa Wahadhiri ili kuzuia mianya ya rushwa ya ngono ambayo inaweza kujitokeza vyuo vikuu. (Makofi)

Name

Peter Joseph Serukamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kaskazini

Answer

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, la kwanza, nashukuru sana kwa fursa hii. Vyuo vikuu vyenyewe vinaendeshwa kwenye mambo ya taaluma na senate zao na kama ulivyosema taratibu za kusahisha mitihani zipo, kuna Bodi za kupitia ile mitihani lakini vilevile kuna wanaokagua mitihani hiyo mara nyingi wanatoka chuo cha nje hata nje ya Nchi lakini naomba nitoe kauli ifuatayo:-

Mheshimiwa Spika, malalamishi yoyote ya rushwa ya aina yoyote hasa rushwa ngono tunahimiza yaripotiwe mara moja. Tunachukulia very serious suala la kumuonea mwanafunzi kwa kutaka rushwa na hasa rushwa ya ngono na tuhuma tukizisikia hata kwa hisia sisi tunaanza kuzifanyia uchunguzi wenyewe.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ningetoa wito kwa Watanzania wote, wazazi na wanafunzi wakati ambapo kuna dalili yoyote kama hiyo tafadhali toa taarifa lakini muhimu kutoa taarifa ya ukweli. Kwa sababu ukitoa taarifa ambayo inajikanganya wakati mwingine kama alivyojibu Mheshimiwa Naibu Waziri hapa wakati mwingine inakua vigumu sana ku-establish lakini Serikali inachukulia serious sana kuwa na haki katika usahihishaji wa mitihani ili tuhakikishe wanaofaulu kweli wamefaulu wamefauli kwa haki, nashukuru sana.