Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tecla Mohamedi Ungele
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 1
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa jitihada kubwa za Serikali za kupeleka maji kule Matekwe na kule Lihimalya. Nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ni shahidi alivyopita Ngunichile, aliona maji wanayokunywa wananchi wa Ngunichile, alishuhudia mwenyewe maji ya kuokota chini. Je, hizi fedha zilizoombwa milioni 670 ili kukamilisha ule mradi wa kupeleka majisafi na salama Ngunichile, lini fedha hizo zitapelekwa? (Makofi)
Swali la pili, Kata ya Kandawale, Kilwa Kaskazini ni sehemu yenye mwinuko na ni changamoto kubwa ya majisafi na salama. Je, ni lini Serikali mtapeleka maji safi na salama Kata ya Kibata? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tecla Ungele, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kumpongeza Mheshimiwa Tecla, kwa kweli alinipa ushirikiano sana kwenye ziara yangu, nilipokwenda kule. Eneo hili la Ngunichile kweli tumefika na kazi zimeanza, kadri fedha zitakapoendelea kupatikana Mheshimiwa Tecla Ungele, tutaendelea kupeleka fedha kwa awamu hakika Ngunichile wanakwenda kunufaika kwa maji safi na salama kwa ufuatiliaji wako mahiri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Eneo la kule Kilwa hii Kata uliyoitaja Mheshimiwa ipo katika mpango wa kuhakikisha tunakwenda kupeleka maji kwa kuchimba kisima kirefu na kusambaza vichotea maji maeneo ya karibu na makazi ya wananchi. (Makofi)
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mradi wa maji ya mserereko Chagongwe pamoja na Nongwe, Wilaya ya Gairo imechukua muda mrefu sana. Ili wananchi waweze kupata maji ya kutosha ni lini mradi huu utaanza?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Christine Ishengoma, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikupongeze Mama yangu Mheshimiwa Christine Ishengoma, umefuatilia hili suala toka ukiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Maji na Mazingira, nikuhakikishie mradi huu tunakwenda kuutekeleza katika mwaka ujao wa fedha. Tunahitaji kuona Gairo, inakwenda kupata majisafi na salama ya kutosheleza pamoja na jitihada zote zinazoendelea za muda mfupi ili wananchi waweze kuendelea kupata majisafi na salama. (Makofi)
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 3
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itasambaza maji yanayotoka kwenye Visima vya Kisarawe Two katika Kata ya Toangoma?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Chaurembo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, visima vya Toangoma tayari DAWASA wanaendelea na jitihada kuona wanakwenda kusambaza maji, wataanza mwaka huu wa fedha na mpaka kufika mwaka ujao wa fedha maeneo yale yote ambayo yapo ndani ya mradi yatakwenda kufikiwa.
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 4
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Busokelo hususani Kata ya Lwangwa Mjini, kuna tatizo kubwa sana la miundombinu ya maji pia wananchi hawapati maji. Je, ni lini wananchi wa Kata ya Lwangwa, Kata ya Ntaba, Kata ya Kambasegela na Kata ya Kisegese watapata majisafi na salama? Ahsante.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fredy Atupele Mwakibete, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Lwangwa Mjini. Pale Lwangwa chanzo cha maji kiko chini na Mji kidogo upo juu eneo lile la Busokelo ni milima na mabonde, kwa hiyo kile chanzo kwa sababu kiko chini maji yanafika machache pale juu. Kwa hiyo, tayari RUWASA Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana RUWASA Wilaya wanafanya jitihada ya kujenga chanzo kingine kwenye mwinuko ili kuona sasa pale Busokelo, Lwangwa Mjini, wanapata maji ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ya Ntaba, tulikuwa na Mkandarasi mbabaishaji na Mkandarasi huyu pia alikuwa anafanya mradi mmoja pale Mbarali tulishamuondoa, kwa hiyo na hapa Ntaba pia tunamuondoa tunaenda kupeleka Mkandarasi ambaye yuko serious na kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie Bunge lako Tukufu wale Wakandarasi wote wababishaji kiama chao kimefika hatutaweza kuendelea kuwavumilia kwa sababu wanarudisha nyuma jitihada za kumtua ndoo Mama kichwani. (Makofi)
Name
Rose Vicent Busiga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 5
MHE. ROSE V. BUSIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Nami naomba kuuliza swali la nyongeza.
Ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inatatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Geita.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali nyongeza la Mheshimiwa Rose Busiga. Ninakupongeza kwa swali zuri lakini unafahamu nimeshafika Geita kufanya ziara na tuna miradi mingi sana ndani ya Mkoa wa Geita na fedha nyingi zimeweza kuelekezwa. Kwa hiyo, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha miradi hii iliyoanza inakamilika lakini miradi mengine tutaendelea kuibua kadri ya mahitaji.
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 6
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusa na ridhaa yako kwa dhati kabisa naomba nitoe shukrani zangu kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutuletea miradi ya maji ya mabilioni ya fedha Jimboni Arumeru Mashariki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukrani hizo mradi wa maji wa Kata za Imbaseni, Maji ya Chai, Kikatiti hadi Samaria unatekelezwa kwa kusuasua sana. Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu huyo miradi?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Pallangyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo yote uliyoyataja Mheshimiwa Mbunge, mimi na wewe tumekwenda ziara na shughuli zinafanyika tumeshuhudia sisi wote. Miradi kukamilika tutaendelea kupeleka fedha ili kuona kwamba Wakandarasi wanafanya kazi na miradi hii inakamilika wananchi wananufaika na majisafi na salama.
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 7
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji vilivyopo kwenye Kata za Kalunde, Itonjanda, Ndevelwa, Ikomwa na Kakola katika Jimbo la Tabora Mjini, havijanufaika na mradi wa Maji wa Ziwa Viktoria mpaka hivi ninavyozungumza. Serikali, mna mpango gani wa kusambazia wananchi hawa maji ili waweze kunufaika na mradi huo wa mabilioni ya fedha uliofikishwa Tabora?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mwaifunga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Hawa kwa kufuatilia na sisi Wizara ya Maji maeneo yote ambayo mtandao wa maji Viktoria umepita Mkoa wa Tabora kazi zinaendelea. Juzi nimeenda mimi mwenyewe ziara vilevile nimekwenda na Kamati ya Kudumu ya Bunge. Katika vijiji hivi ulivyovitaja vya Mkoa wa Tabora, maeneo haya kama yapo mbali na mtandao wa bomba tutawapelekea huduma mbadala kama kuchimba visima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tutaangalia uwezekano wa kuona kwamba Mkoa wa Tabora, maeneo yote ambayo yanafikika Jimbo la Tabora Mjini, ambapo ndiyo chanzo kikubwa na tenki kubwa lilipo wataenda kunufaika na tunaendelea na jitihada hizi. Mimi na Mheshimiwa Waziri na Kamati ya kudumu ya Bunge tumeangalia kwa jicho la kipekee Jimbo la Tabora na Mkoa wa Tabora. (Makofi)
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
Supplementary Question 8
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Waziri wa Maji na Naibu Waziri wake, katika Kata ya Kiwira wamejitahidi kutuongezea nguvu. Je, ni lini watapeleka maji katika Kata ya Kisondela kwa maana wanawake wa kule wanashindwa kupata maji?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Sophia, hili swali tumeshali-discuss na tumeshaliingiza kwenye mpango kazi wetu wa mwaka 2024/2025 ili kuhakikisha Kisondela wanakwenda kunufaika na majisafi na salama. (Makofi)