Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Josephine Tabitha Chagulla
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Watumishi pamoja na Vifaa Tiba katika Hospitali ya Mkoa wa Geita?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina swali moja la nyongeza. Hospitali za Wilaya ya Nyang’hwale, Mbogwe, Bukombe na Chato hazina madaktari bingwa wa watoto na akina mama. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kupeleka madaktari bingwa wa watoto na akina mama katika hospitali hizi ili tuweze kupunguza msongamano wa wagonjwa uliopo katika Hospitali yetu ya Mkoa wa Geita? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambayo anaifuatilia sana hospitali yake ya Mkoa wakati wote pamoja na namna ambavyo anajua mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye Wilaya za Mkoa wake wa Geita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumwambia Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwanza kwenye miongozo ya Wizara kuna utaratibu wa rufaa; na kila level ya hospitali ina aina gani ya kada inahitaji kwa level fulani ya elimu. Mimi na mwenzangu Mheshimiwa Dkt. Dugange tutakaa naye tumweleze na tuone namna ya kushirikiana na kuelekeza namna ya kushauri wananchi, inapotokea mambo mbalimbali yanayohitaji baadhi ya aina ya madaktari wafanye nini kwa wakati huo, ahsante sana. (Makofi)
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Watumishi pamoja na Vifaa Tiba katika Hospitali ya Mkoa wa Geita?
Supplementary Question 2
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto kubwa ya Watendaji katika Hospitali ya Mkoa ya Kitete Tabora. Serikali ina mpango gani wa kutuongezea wafanyakazi wenye weledi katika hospitali yetu ili waweze kutoa huduma thabiti kwa wananchi wa Tabora?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mpango wa kuboresha na kama ambavyo umesikia, hata mwaka huu upo utaratibu kwamba wataajiriwa watumishi wengine. Ndiyo maana wiki iliyopita nilikuwa pale, ni kwa ajili ya kuhakikisha tunaboresha huduma kwenye Hospitali yetu ya Kitete. Mheshimiwa Waziri wa Afya alinituma pale nimekwenda, nimeangalia matatizo mbalimbali yaliyohitaji kuchukua uamuzi pale tumechukua uamuzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwambam kwa maelekezo ya Waziri wa Afya, pale Hospitali ya Wilaya ya Kitete itakaa vizuri kama Waheshimiwa Wabunge mlivyotegemea. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved