Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ili wananchi waweze kupata huduma?

Supplementary Question 1

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nichukue nafasi ya pekee kuishukuru Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutujengea Mahakama nzuri katika Wilaya yetu ya Buhigwe. Pamoja na ujenzi huo na huduma zimekwishaanza, nina maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Mahakama ya Mwanzo ya Muyama katika Tarafa ya Muyama majengo yake yamechakaa sana, ni lini Serikali itakarabati mahakama hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Tarafa ya Manyovu kijiografia ni tarafa kubwa ina eneo la utawala wa kata 14. Mwaka 2022 Serikali ilikubali kutujengea mahakama mbili; moja Manyovu na nyingine eneo la kimkakati katika Kata ya Janda. Lini Serikali inaaanza ujenzi wa mahakama hizo? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru kwa pongezi ambazo zimetolewa kwa Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uboreshaji wa sekta ya Mahakama kama inavyoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umuhimu wa kukarabati Mahakama ya Muyama, nikiri tu kwamba Mahakama zetu za Mwanzo katika maeneo mbalimbali ikiwemo hii ya Muyama iliyopo huko Buhigwe, ni kweli mahakama hizi ni kongwe na ni chakavu zinahitaji ukarabati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupanga ni kuchagua na kulingana na uwezo wa kibajeti mwaka huu tumeweza kujenga Mahakama ya Mwanzo ya Manyovu. Naomba Mheshimiwa Mbunge pamoja na jitihada zake za kutaka haki iwafikie wananchi wake atuvumilie pale hali ya bajeti itakavyoruhusu basi Mahakama ya Muyama itakarabatiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu tarafa kubwa hii ya Manyovu yenye kata 14 kuhitaji mahakama katika Kata ya kimkakati ya Janda ninaomba nilichukue ombi lake hili ili sekta ya mahakama iweze kuliingiza katika mpango mkakati wake, ili pale fedha zitakapopatikana eneo hili la Janda liweze kujengewa Mahakama ya Mwanzo, nashukuru. (Makofi)

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ili wananchi waweze kupata huduma?

Supplementary Question 2

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Nalasi, Mahakama ya Nalasi, ni moja ya Mahakama ambazo ziliwekwa kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha unaondelea kuweza kujengwa. Ni lini ujenzi ule wa Mahakama ya Nalasi utaanza? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiri kwamba katika Mkoa wa Lindi zipo Mahakama ambazo zipo katika mpango wa kujengwa upya na kukarabatiwa ikiwemo hii ambayo Mheshimiwa Mbunge ameirejea. Nimwahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba pale fedha zitakapopatikana mahakama hiyo itaweza kufanyiwa ukarabati, nashukuru.

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ili wananchi waweze kupata huduma?

Supplementary Question 3

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, Mahakama ya Wilaya ya Lushoto ni ya zamani sana, lakini Serikali iliahidi kwamba itajenga mahakama ile. Nataka kujua ujenzi ule utaanza lini? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafahamu jinsi Mheshimiwa Shekilindi anavyofuatilia uimarishaji wa sekta ya mahakama katika wilaya yake hasa ukizingatia Wilaya ya Lushoto kipo pia Chuo cha Mahakimu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Mahakama ya Lushoto mwaka huu ipo kwenye bajeti, pale taratibu za manunuzi zitakapokamilika ujenzi wa Mahakama hiyo utaanza, ahsante.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ili wananchi waweze kupata huduma?

Supplementary Question 4

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tunashukuru kwa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Bunda maana tulipanga kwenye nyumba ya mtu kwa muda mrefu, tumeshaondoka na hilo tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna uchakavu wa Mahakama za Mwanzo hasa ambazo zimechakaa sana Mahakama ya Mwanzo Kabasa na Mcharo. Ni lini sasa mtahakikisha mtatukarabatia au kutujengea Mahakama za Mwanzo katika hayo maeneo niliyoyataja kwenye Jimbo la Bunda Mjini? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa pongezi zilizotolewa na Mheshimiwa Bulaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa Mahakama ya Bunda ya Wilaya, nimweleze tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango wa mahakama ni kujenga na kukarabati. Kwa maana ya juhudi zilifanyika sasa na hivi karibuni Mkoa wa Mara unafahamu Mheshimiwa Bulaya, ulijengewa Intergraded Justice Centre (Kituo Jumuishi cha Mahakama), zinajengwa Mahakama, zimejengwa Mahakama Butiama, imejengwa Bunda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Mahakama za Mwanzo, mwaka huu tutajenga Kinesi, Mugumu na tutajenga Lugangabilili. Kwa hiyo, pale fedha zitakaporuhusu mahakama uliyoitaja ya Kabasa na Mcharo zitaweza kujengwa wa upya au kukarabatiwa kulingana na kiwango cha uchakavu uliofikiwa, nashukuru.

Name

Ahmed Mabukhut Shabiby

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Gairo

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ili wananchi waweze kupata huduma?

Supplementary Question 5

MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Mwanzo ya Gairo, ilipitishwa toka mwaka 2010 na ilipita kwenye bajeti, lakini mpaka leo bado haijajengwa, ni lini itajengwa? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema wakati najibu jibu la msingi, ni mpango wa sekta ya mahakama kuboresha mahakama zake, lakini hii inakwenda na uwezo wa kibajeti na upatikanaji wa fedha. Kwa Mkoa wa Morogoro, Mahakama ya Wilaya ya Ulanga na Mahakama ya Kilosa ipo kwenye mpango wa ujenzi, lakini pale fedha zitakaporuhusu, pale fedha zitakapopatikana Mahakama ya Gairo itazingatiwa pia, nashukuru.

Name

Innocent Edward Kalogeris

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe ili wananchi waweze kupata huduma?

Supplementary Question 6

MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Kata ya Bwakira Chini imo katika mpango wa bajeti ambao tunaumalizia mwezi huu wa Juni, ni lini itajengwa kwa sababu muda wa bajeti na umeshakwisha?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Kalogeris kwamba Mahakama yake ya Bwakira Chini kama alivyosema imo kwenye mpango wetu wa ujenzi na hivi sasa taratibu za manunuzi zinakamilishwa na pale zitakapokamilishwa ujenzi huo utaanza mara moja, wala hautaathirika na kuhama kwa mwaka wa fedha, kwa sababu ni fedha za maendeleo zitaombewa Wizara ya Fedha na kuhamisha hizo hizo kutumika hata baada ya Julai, nashukuru.