Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Kaskazini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja?
Supplementary Question 1
MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Pamoja na majibu hayo nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; ninapenda kujua kwa kipindi hiki cha miaka miwili, mwaka 2023 na huu mwaka 2024, ni watu wangapi ambao wametiwa hatiani kwa makosa hayo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; ninapenda kujua mikakati madhubuti ya Serikali katika kuhakikisha tunakomesha au inakomesha matendo hayo kwenye jamii, kwa sababu bado tunaona pamoja na sheria zilizopo, lakini kule field bado matukio hayo ni mengi, sasa walete sheria, walete Muswada hapa Bungeni tutunge sheria kuiongezea meno sheria iliyopo kukomesha matendo hayo.
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninapenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza linahusu takwimu. Kwa swali hili ninaomba tukutane ili nimtafutie takwimu, ili tuone ni matukio mangapi yametokea katika mahusiano ya jinsia moja ili tuweze kujua na kuukomesha ukatili huu wa kijinsia.
Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, sisi sote tunafahamu masuala haya ya mmomonyoko wa maadili kwamba yanakera sana kwa jamii. Tunapaswa kujua kuwa Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan iko makini kwa usimamizi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa ili kuweka heshima na kuwa sehemu ya kuimarisha misingi ya utawala bora. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutaendelea kuimarisha kutoa elimu kwa jamii ili kukomesha vitendo hivi vya kikatili na mapenzi ya jinsia moja kwa kuhakikisha kwanza mila na desturi za Mtanzania zinaimarishwa. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved