Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kama ulivyosema kwenye jibu lako la msingi kwamba ni mita 400 tu ambazo zimejengwa kwa hiyo bado kama kilometa 64 hazijajengwa. Je, ni lini sasa Serikali itapata fedha ili barabara hii ianze kujengwa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Barabara ya kutoka Old Shinyanga kwenda Solwa inaunganisha Manispaa ya Shinyanga kwa maana ya Mkoa kwenda kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, lakini kipindi cha mvua haipitiki na tumeona juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali kwa kujenga lami katika Halmashauri ya Msalala, Bulige, Segese na sehemu nyingine na kuweka taa.
Mheshimiwa Spika, je, kwa sababu Halmashauri ya Shinyanga ndiyo makao makuu na hakuna hata kilometa moja, ni lini Serikali itaweza kutujengea angalau mita chache katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninaomba kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge kwa pamoja.
Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba barabara hii pia ndiyo inayopita katika Makao Makuu ya Halmashauri na tulishapokea maombi rasmi ya mkoa kwa maana kwamba tufikishe barabara hii mpaka makao makuu.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kujenga kipande cha lami walau kifupi katika eneo la halmashauri, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutalifanyia kazi, kwa sababu mpango ni kwamba katika maeneo yote ya Makao Makuu ya Wilaya au Halmashauri, basi eneo linalohusu huo mji liweze kuwa na lami.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutalichukua na kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na ombi la RCC kuunganisha Mji wa Shinyanga na Halmashauri ya Shinyanga DC. Ahsante.
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 2
MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Wanabukoba tunamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia kwa kufanya miradi ya kimageuzi katika mkoa wetu na Bukoba Mjini tukiwemo. Sasa ujenzi wa barabara ya njia nne katika Mji wa Bukoba Mjini unaogharimu shilingi bilioni 12.4 tayari umeshaanza, naomba kufahamu ni lini mradi huu utakamilika? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna mradi wa kujenga kutoka barabara mbili kwenda barabara nne na tumegawanya katika vipande viwili. Kipande cha kwanza kiko karibu 44%. Kwa mujibu wa mkataba tunategemea kufikia mwishoni mwa mwezi Mei iwe imekamilika. Kipande cha pili kikihusisha na Mto wa Kanoni ambao tumetumia hela za emergency kwa sababu kunakuwa na mafuriko; kwa mujibu wa mkataba tunategemea ikamilike mwezi Desemba mwaka huu. Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 3
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa nikiwa nauliza kila mara kuweza kupata jibu la lini Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya barabara yetu inayounganisha Wilaya tatu: Kahama, Nyangh’wale, Busisi-Sengerema, ni lini atapatikana maana hata juzi niliuliza Waziri akasema kwamba nimfuate, tuongee, sasa leo ninataka anijibu kwenye Bunge hili Tukufu. Ni lini sasa Mshauri huyu atapatikana? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli aliuliza swali na ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Nyangh’wale kwamba barabara hii inaunganisha Mikoa mitatu, Geita, Mwanza na Shinyanga na junction ni Mji wa Nyangh’wale. Ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunavyoongea sasa hivi mikataba ipo kwa Mwanasheria Mkuu kwa ajili ya kupitiwa kwa mara ya mwisho na tunategemea kwamba mwezi Machi baada ya mwezi huu wa Februari, Mhandisi Mshauri atakuwa site kwa ajili ya kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Ahsante.
Name
Ally Anyigulile Jumbe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 4
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, ni lini Barabara ya kutoka Matema – Lyulilo - Ikombe itafikia mwisho kwa kilometa mbili zilizobaki? Ahsante sana.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge alikuja ofisini na baada ya kueleza changamoto ambazo zinawakabili wananchi, Wizara iliagiza Makao Makuu TANROADS wamwagize Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya aende akafanye tathmini ili aweze kuleta mapendekezo ya haraka nini kiweze kufanyika ili kuondoa adha ya wananchi ambayo wanaipata katika barabara hiyo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameisema. Ahsante.
Name
Hassan Seleman Mtenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 5
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iwaeleze wananchi wa Mtwara kwenye upanuzi wa Barabara ya kutoka Mtwara - Mnivata mpaka Masasi, wale ambao waliahidiwa watalipwa fidia na wakapeleka documents zao zote pamoja na kufungua akaunti za kuingizia hizo fedha. Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi hao ambao walipisha ujenzi wa Barabara ya Mtwara? Ninakushukuru. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Mtwara kwamba tayari tuko kwenye maandalizi ya kupata hizo fedha ili tuweze kuwalipa kwenye huo mradi ambao unaendelea. Ahsante.
Name
Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 6
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya bypass Songea Manispaa? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, bahati nzuri Barabara hiyo ya Songea bypass ndiyo inayounganisha na ukarabati mkubwa wa Barabara ya Songea kwenda Lutukira hadi Njombe. Sasa hivi tunavyoongea Mkandarasi yupo site na tayari tumeshaanza kuwalipa fidia wananchi ambao watapisha hiyo barabara. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari mkandarasi ameshapatikana na tayari yupo site, tumeshalipa fidia ili kazi ianze, ahsante.
Name
Mussa Ramadhani Sima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mjini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 7
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Spika, ni lini Barabara ya bypass ya kilometa 46 itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami ukizingatia upembuzi yakinifu tayari? Ninashukuru.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara hiyo imeshafanyiwa usanifu wa bypass ya Singida na Serikali tunaendelea kutafuta fedha ili tuweze kuijenga kupunguza msongamano mkubwa ambao sasa upo katika Mji wa Singida, ahsante.
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 8
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Njia Nane unaoanzia Kibaha Maili Moja hadi Chalinze uko katika hatua ipi?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni mwendelezo wa Barabara ya Kimara kwenda Kibaha. Hii barabara tunategemea tuijenge kwa Mfumo wa PPP.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sasa hivi ipo kwenye hatua za usanifu na baada ya hapo nadhani wakandarasi ambao wamejitokeza tutatafuta mkandarasi ambaye anaijenga na ni mwendelezo kutoka Kibaha hadi Morogoro na Morogoro hadi Dodoma, ahsante. (Makofi)
Name
Innocent Edward Kalogeris
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 9
MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Spika, ni lini mkandarasi wa Barabara ya Bigwa – Kisaki atapata advance payment ili aweze kuingia kikamilifu katika kutekeleza majukumu yake na kuwaokoa wananchi katika adha ya kukwama hasa katika kipindi cha mvua? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Barabara aliyoitaja ya Bigwa - Kisaki kilometa 78 ilishapata mkandarasi na barabara zote ambazo zilikuwa zimekwama kwa kusubiri advance, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge sasa hivi tumeshaanza kutoa fedha na barabara nyingi ikiwemo hiyo ipo kwenye mpango ambao tuna uhakika muda siyo mrefu itapata advance ili mkandarasi aendelee na kazi.
Name
Issa Jumanne Mtemvu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibamba
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 10
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Victoria - Mbezi Shule - Mpiji Magohe imetangazwa kwa kilometa 12 zaidi ya miezi sita na mkandarasi bado hajapatikana. Je, ni lini mkandarasi atapatikana na barabara hii itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hata Wizara tunajua umuhimu wa barabara hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa foleni ambayo ipo katika Jimbo la Mheshimiwa. Taratibu zinazoendelea ni za kupata huyo mkandarasi sahihi, tulishatangaza na kwa hiyo taratibu za manunuzi zitaendelea. Tukishakamilisha mkandarasi ataingia site kuanza ujenzi huo muhimu wa Barabara, ahsante.
Name
Christopher Olonyokie Ole-Sendeka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Simanjiro
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 11
MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Spika, Barabara inayotoka Arusha, Orkesumet - Kibaya – Kongwa ambayo ni barabara ya EPC+ Finance itaanza kujengwa lini kwa kiwango cha lami? Nakushukuru sana.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikijibu mara kadhaa kuhusu hiyo barabara ambayo ilikuwa ni moja ya zile barabara saba ambazo zilikuwa kwenye utaratibu wa EPC + F. Mara kadhaa nimekuwa nikieleza Bunge hili kwamba tumebadilisha utaratibu; Kamati imeundwa na kutafuta utaratibu.
Mheshimiwa Spika, tutawatumia walewale wakandarasi, lakini tutajenga kwa utaratibu tofauti. Hii imeundwa kuona kwamba wakandarasi ambao tulikuwa tumewapata ikiwezekana ndiyo waweze kufanya hiyo kazi, ikiwepo na hiyo barabara ambayo Mheshimiwa Ole-Sendeka ameitaja, ahsante.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Barabara ya Old Shinyanga hadi Solwa utaanza?
Supplementary Question 12
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona, Barabara ya kutoka Matai kwenda Kasesha Border ni barabara muhimu sana na sasa hivi mkandarasi hayupo. Je, ni lini atalipwa fedha ili ujenzi uendelee?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli barabara ilishaanza na mkandarasi ailikuwa site, lakini tunachofanya sasa hivi ni kutafuta fedha ili mkandarasi huyo aendelee na kazi kwa kuendelea kulipa IPC ambazo amezileta Wizarani. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba muda siyo mrefu mkandarasi huyo ataanza kuendelea na hiyo kazi ambayo alikuwa anaifanya. Ahsante.