Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ummy Ally Mwalimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tanga Mjini

Primary Question

MHE. UMMY A. MWALIMU aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaunganishia umeme wa gharama nafuu wananchi wa maeneo ya pembezoni yenye sifa za Vijiji, Tanga?

Supplementary Question 1

MHE. UMMY A. MWALIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, kata 10 kati ya kata 27 za Halmashauri ya Jiji la Tanga zina mitaa yenye sifa za vijiji, kama vijiji vya Muheza, Handeni, Mkinga, Pangani na Korogwe Vijijini. Kwa nini mitaa hii yote isiingizwe katika utaratibu wa wananchi kupata umeme wa REA wa shilingi 27,000?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa, Wakuu wa Nchi wamepitisha Azimio la Nishati Safi la Dar es Salaam chini ya uenyeji wa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa nini Serikali isianzishe programu maalum ya kuwawezesha wananchi kuunganisha umeme wa mkopo halafu walipe kidogo kidogo, kupitia matumizi ya kila siku ya umeme? Ahsante.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kuhusiana na Mitaa ya Tanga Mjini ambayo Mheshimiwa amesema iunganishwe na REA kwa sababu, ina sifa za vijiji. Ndiyo maana Serikali tunatekeleza miradi ya Peri-Urban kwenye maeneo haya, ili kurahisisha kuwafikia wateja wengi zaidi kwa gharama nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, kwa sasa hivi ndiyo maana tumepeleka umeme katika vitongoji 15, lakini miradi ya Peri-Urban inaendelea, ili wananchi waweze kuunganisha umeme kwa gharama nafuu. Jambo la kuendelea kuwasisitiza, ni kwamba, wakati miradi inaendelea, basi wananchi waweze kuunganisha umeme, ili kuepuka kadhia pale ambapo miradi inaisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la pili la wananchi kuunganisha umeme na kulipa kidogo kidogo. Ninapokea wazo la Mheshimiwa Mbunge na tutaendelea kulichakata ili kuona namna ya kulifanyia kazi kwa sababu, huko nyuma tayari TANESCO walijaribu kufanya hivyo, baadaye wakawapatia Akiba Commercial Bank kufanya hivyo, lakini marejesho hayakuwa mazuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutaendelea kuchakata kuona namna ambayo tunaendelea kulifanyia kazi ili wananchi waendelee kupata huduma. Kwa hiyo, ni wazo zuri, tutaendelea kulichakata. Ahsante.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. UMMY A. MWALIMU aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaunganishia umeme wa gharama nafuu wananchi wa maeneo ya pembezoni yenye sifa za Vijiji, Tanga?

Supplementary Question 2

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaunganishia umeme wananchi wa Kijiji cha Magugu, Jimbo la Babati Vijijini, kwa bei ya shilingi 27,000 badala ya 321,000?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa swali la Mheshimiwa Mbunge. Maeneo ambayo ni Vijiji-Miji ambayo ina center ndogo, gharama yake ya kuunganishwa umeme ni shilingi 321,000. Ndiyo maana tunapeleka Miradi ya Vitongoji, kwa ajili ya kuwafikishia wananchi huduma ili wakati wanaunganisha gharama ipungue.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka huu wa fedha tutaongeza vijiji hamsini kwa jimbo ambalo ameuliza Mheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo, niendelee kuwasisitiza wananchi, wakati miradi inaendelea waweze kuunganisha umeme ili kuweza kukwepa kadhia hii wakati miradi inaisha. Ahsante.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. UMMY A. MWALIMU aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaunganishia umeme wa gharama nafuu wananchi wa maeneo ya pembezoni yenye sifa za Vijiji, Tanga?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. ANGELINE S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mitaa ya Masemele, Kilabela, Bujingwa, Nyanguku, Butingo na Koronto, ilikuwa katika ile mitaa 15 iliyokuwa inawekewa umeme wa REA. Hata hivyo, baadaye mitaa hii imeondolewa kwa sababu, iko mbali na line kubwa. Je, ni lini sasa mitaa hii itasogezewa line kubwa, ili na wao waweze kupata umeme kama ambavyo wanapata wengine?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Miradi ambayo sasahivi tunakwenda kwenye vitongoji ni miradi ambayo ni jazilizi, lakini inajumuisha kujenga miundombinu kwenye maeneo ambayo yamepitiwa tu na line kubwa. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, katika miradi tunayoianza (kama hii ya vitongoji takribani 9,000 tutakayoianza kwa mwaka huu wa fedha), basi na mitaa hiyo tutaona namna ya kuiangalia ili na yenyewe iweze kunufaika na huduma hii. Ahsante.