Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika Kata za Kikolo na Kagugu - Mbinga Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Spika, naomba niishukuru Serikali kwa kukubali kufanya tathmini katika Kata ya Kikolo na Kagugu kwa kuwa zina changamoto kubwa ya mawasiliano.
Mheshimiwa Spika, swali langu la nyongeza, baada ya kufanya tathmini, je, Serikali inaweza ikanihakikishia kwamba mpango huo utaingizwa katika bajeti ya mwaka 2025/2026?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Jonas Mbunda kwa kuishukuru Serikali kwa kazi ambayo tunaendelea kuifanya katika eneo hili la Mbinga Mjini. Pia, nampongeza kwa ushirikiano ambao tunaendelea kufanya baina yako na sisi Wizara.
Mheshimiwa Spika, nataka kukuhakikishia ni dhahiri baada ya tathmini kukamilika, basi itaingizwa kwenye bajeti ijayo na kuja kuhakikisha minara inajengwa na usikivu unaimarishwa. (Makofi)
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika Kata za Kikolo na Kagugu - Mbinga Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa minara iliyojengwa na Kampuni ya TTCL katika vijiji vya Nandete, Pungutini, Mwengei na Chapita, haifanyi kazi kwa ufanisi wa kutosha. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha mawasiliano katika minara hiyo? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, tunamshukuru sana Mheshimiwa Francis, amekiri minara imejengwa vijiji hivi vyote alivyovitaja. Kwa hiyo, tutafuatilia nini tuweze kufanya ili minara hii iliyokamilika iweze kuboreshwa na itoe huduma iliyokusudiwa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved