Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rose Vicent Busiga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. ROSE V. BUSIGA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini ninataka kujua ni lini itajenga Barabara ya Geita – Nyarugusu mpaka Kahama?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Geita – Nyarugusu hadi Kahama imegawanywa katika vipande viwili. Kipande cha Kahama hadi Ilogi tayari mkandarasi yuko site anaijenga kwa kiwango cha lami. Kutoka Ilogi – Nyarugusu hadi Geita tupo katika hatua za mwisho wa manunuzi, ili kuweza kusaini mkataba kwa kilometa zote 61.2, ili kuunganisha Mkoa wa Geita na Mkoa wa Shinyanga. Ahsante.

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini ujenzi wa Barabara ya Itoni – Lusitu kwa kiwango cha zege utaanza baada ya kusimama kwa muda wa mwaka mmoja? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mwanyika ni ambayo mkandarasi alishapatikana, yuko site na muda si mrefu tutamlipa fedha za awali, ili aweze kuendelea na kazi. Niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, katika barabara zile 27 za kipaumbele fedha ni nyingi sana; tumeshalipa barabara 17, tatu zimelipwa nusu na chache hizi ambazo hazijalipwa malipo ya awali fedha inatafutwa iweze kulipwa haraka, ili wakandarasi waendelee na kazi. Ahsante.

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mbulu – Garbabi, kilometa 25. ujenzi wake umesimama. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyoitaja ni kweli ilikuwa imesimama, lakini tunavyoongea sasa hivi mkandarasi yuko site na ameshapata fedha za awali. Kwa hiyo, tunaamini kazi zitaanza haraka iwezekanavyo. Ahsante.

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 4

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Uvinza mpaka Kasulu kwa kiwango cha lami? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Genzabuke. Kipande cha barabara hiyo kilichobaki kinatoka Mpanda hadi Kasulu. Tunategemea itakuwa ni sehemu ya barabara ambayo tutaijenga kwa kiwango cha lami kwa fedha ambayo ilibaki kwenye barabara zilizojengwa katika Mkoa wa Katavi. Kwa hiyo, ipo kwenye mpango iweze kujengwa kwa kiwango cha lami, ili tuunganishe Katavi na Kigoma, kwa maana ya Uvinza hadi Kasulu. Ahsante.

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 5

MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni lini Barabara ya Mingoi – Kiembeni ambayo imerudishwa chini ya umiliki wa TANROADS itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kabla ya kuijenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami, kwanza ni lazima ijengwe katika standard za TANROADS, halafu iweze kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ikiwa ni maandalizi ya kuijenga kadri fedha itakavyopatikana. Ahsante.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 6

MHE. MARY F. MASANJA: Mheshimiwa Spika, ni lini Barabara ya kutoka Nhungumalwa - Ngudu hadi Magu itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, barabara aliyoitaja, ambayo tutaanza kujenga kilometa 10, tayari ilishatangazwa na sasa hivi tuko kwenye hatua za manunuzi. Ahsante.

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 7

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, ni lini Mkandarasi wa Barabara ya Nansio – Rugezi atarudi site na kukamilisha ujenzi wa barabara ile? Ninashukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni Mkandarasi mzawa ambaye anajenga hiyo barabara na tayari tumeshapokea maombi yake ya advance pamoja na kazi ambayo ameifanya. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, sasa hivi tunaandaa malipo yake, ili aweze kuendelea na kazi. Ahsante.

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 8

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ni lini Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara aliyouliza Mheshimiwa Mbunge, ndio zile barabara saba ambazo nimesema utaratibu mpya umeandaliwa na hizo barabara tutazielezea namna zitakavyotekelezwa tofauti na ule mpango uliokuwepo awali. Kamati imeundwa rasmi, maalum, kwa ajili ya kuzipitia barabara hizo na kutafuta namna sahihi ya kuzijenga kwa utaratibu ambao tumeuzoea. Ahsante.

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 9

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Spika, Mkandarasi wa Barabara ya Katumba – Suma – Ruangwa, ni lini atapeleka mitambo site ikizingatiwa kwamba, ameshalipwa advance? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mkandarasi huyo amelipwa advance kama wiki moja au mbili zilizopita, anachofanya sasa hivi ni kukusanya wafanyakazi na kuainisha maeneo ambayo atajenga kambi zake; atajenga kambi mbili kwa maana ziko barabara mbili na mkandarasi ni mmoja. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunaamini utakapofika mwezi Februari katikati kazi zote zitakuwa zimeanza, lakini tumemhimiza kabla mitambo haijafika aanze kufanya zile kazi, kwa maana ya magari yaanze kupita mle ambamo yanakwama kwa sababu, hatukupanga fedha za maintenance, yeye ndio anatakiwa afanye hiyo kazi.