Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Mkoa wa Mtwara utaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa?
Supplementary Question 1
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza, umeme umekuwa ukikatika sana katika Mkoa wa Mtwara na Wilaya zake zote, wakati mwingine inakuwa kama vile kuna mtoto anachezea. Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusiana na kukatika huku kwa umeme kunakosababisha wajasiriamali wanaotumia umeme kushindwa kuendelea na shughuli za kiuchumi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa huko nyuma tulipewa mkakati wa muda mfupi ikiwepo kufunga anti-closure, lakini imeonekana hazijasaidia. Je, nini hatua ya dharura itakayosababisha changamoto hiyo kwisha kabla ya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maswali ya Mheshimiwa Mbunge na naomba niyajibu kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu tulifanya hatua za muda mfupi kwa ajili ya kuboresha umeme katika Mkoa wa Mtwara, vilevile katika Mkoa wa Lindi. Katika hatua zile za muda mfupi tuliweza kusimika mashine kubwa zaidi ya kuzalisha umeme wa megawati 20, vilevile tulifanya ujenzi wa njia ya kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 kutoka Nanganga hadi Masasi kwa ajili ya kuimarisha umeme katika Wilaya za Newala pamoja na Masasi.
Mheshimiwa Spika, hatua hizo zilisaidia kwa kiasi chake, kwa sasa hivi tunao mkakati wa kuendelea kufanya marekebisho makubwa katika laini zetu za umeme na kuendelea kubadilisha nguzo katika maeneo ambayo yanakuwa yana majimaji kuweka nguzo za zege pamoja na kupunguza urefu wa laini ili maeneo ya wilaya nyingine pia yaendelee kupata umeme ambao umeimarika zaidi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tumechukua hatua za muda kwa kipindi cha tarehe 23 mpaka 25 katika Mkoa wa Lindi pia tutafanya vilevile katika Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuendelea kuimarisha hali ya umeme. Niwahakikishie wananchi wa Mkoa wa Mtwara tutaendelea kufanya marekebisho na matengenezo ili hali ya umeme iendelee kuimarika. Ahsante.
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Mkoa wa Mtwara utaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa?
Supplementary Question 2
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi. Sababu inayofanya umeme uache kutulia Wilaya ya Liwale ni kukosekana kwa substation, umeme kutoka Maumbika mpaka Liwale umbali ni mrefu sana hatuna substation pale kati jambo ambalo linaathiri sana utulivu wa umeme. Je, lini Serikali inafikiria kutujengea substation katika njia hiyo?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Serikali tunatekeleza mradi wa kuimarisha nguvu ya umeme mradi unaojulikana kama gridi imara na utekelezeka kwa hatua mbalimbali. Kwa sasa tumeshafikia zaidi ya 40% kwa hatua ya kwanza, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge substation na yenyewe ipo katika mpango kadri tunavyoendelea kutekeleza kwa hatua na wenyewe vilevile watafikiwa. Ahsante.
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Mkoa wa Mtwara utaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa?
Supplementary Question 3
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, ili kuunganishwa na Gridi ya Taifa wananchi wa Jimbo langu la Nanyumbu wameachia maeneo yao ili kupisha mradi huo, sasa ni mwaka wa pili hawajalipwa fidia. Ni lini watalipwa fidia? Ahsante sana.
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ni kweli mradi wa kuunganisha gridi kwenye Mkoa wa Mtwara kutokea Songea - Tunduru – Masasi – Maumbika kuna wananchi wameachia maeneo yao kutoka eneo la Tunduru – Namtumbo – Masasi - Maumbika hadi kwenye jimbo la Mheshimiwa Mbunge. Tumewaelekeza TANESCO kwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu wachukue fedha za ndani waanze kulipa fidia na zoezi hilo litaanza hivi karibuni. Ahsante.
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Mkoa wa Mtwara utaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa?
Supplementary Question 4
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, Miongoni mwa hatua ambazo zilipendekezwa hapo awali ili kutatua changamoto za kukatika kwa umeme katika maeneo ya Nanyamba, Tandahimba na Newala ni kuibadilisha laini ile na kujenga nguzo za zege. Je, Wizara ina mpango gani wa kukamilisha mradi huo? Ninakushukuru.
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ni kweli tunao mkakati wa mradi huo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutafanya. Kwa sasa hivi tumeweka nguvu kubwa katika kuendeleza mradi huu wa kufikisha gridi katika Mikoa ya Mtwara na Lindi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na itatekelezeka. Ahsante.
Name
Sebastian Simon Kapufi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Mjini
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Mkoa wa Mtwara utaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa?
Supplementary Question 5
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika, mara ya mwisho mwezi Desemba mwaka 2024, tuliambiwa Gridi ya Taifa ingefika Mkoani Katavi, sasa ni miezi minne imepita. Je, ni lini Gridi ya Taifa itafika Katavi?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Mradi wa kupeleka umeme wa gridi katika Mkoa wa Katavi umeshafikia zaidi ya 95%. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ndani ya kipindi kifupi tutakamilisha mradi huu na Mkoa wa Katavi na wenyewe utakuwa umeunganishwa katika Gridi ya Taifa. Ahsante.