Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, upi mkakati wa kuzirudishia Hospitali za Mafunzo Vyuo Vikuu vyenye Programu ya Afya kama UDOM na MUHAS ili kukidhi miongozo ya Kimataifa?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali moja zito la nyongeza. Kwa sababu amesema kwamba, hizo Hospitali zilikuwa ni Hospitali za Vyuo Vikuu; je, baada ya ripoti ambayo iliongozwa na Profesa Pallangyo, kupelekwa pale kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali haioni haja sasa ya kuifanyia kazi ile ripoti ili kurudisha hizo hospitali zishikiliwe na vyuo kwa 80%? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia masuala ya taaluma na tiba, ninamhakikishia kwamba swali hilo siyo zito kwa sababu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni moja, Wizara ya Afya ni sehemu ya Serikali pia Wizara ya Elimu ni sehemu ya Serikali, kwa hiyo Serikali inashirikiana na inafanya kazi kama Serikali moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie kitu kimoja kwamba leo kwa maana ya MUHAS pale Mloganzila wanajenga mabweni, lakini pia wanajenga nyumba za walimu wakishirikiana na Mloganzila kwa maana ya kwamba walimu watakuwa pale na wakati huo huo wanafunzi wanakuwa pale kwa ajili ya kutumia hospitali.
Mheshimiwa Naibu Spika, tusisahau kwamba Wizara ya Afya ina kazi ya kusimamia tiba, lakini Wizara ya Elimu ina kazi ya kusimamia taaluma. Ukianza kuwafanya hawa Maprofesa wakati wanatakiwa kufundisha aanze kuwaza bei za dawa na kuhakikisha anatengeneza faida wakati huo huo aanze kufikiria namna ya kutengeneza kichwa kizuri cha kuweza kusimamia dawa. Ku-calculate masuala ya dawa unaweza ukachanganya hiyo habari na ukaleta shida ambayo utapunguza ubora kwenye upande wa tiba, wakati huo huo utapunguza ubora kwa upande wa taaluma. Kwa hiyo, tunafikiri kila mahali ambapo imetengenezwa elimu wasimamie elimu lakini pia tiba wasimamie tiba na kwa kushirikiana kama Serikali moja tutaleta ubora mzuri. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved