Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza:- Je, nini mpango wa Serikali wa kupima na kurasimisha maeneo yanayozunguka Mamlaka za Miji ili kuepuka kuendelea kuwa na makazi holela pamoja na kuweza kupeleka huduma za dharura kama ambulance na zimamoto?

Supplementary Question 1

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Wizara, ninaomba kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Manispaa ya Moshi ndiyo manispaa ndogo zaidi Tanzania yenye kilometa za mraba 58; na kwa kuwa upanuzi wa makazi na shughuli za kiuchumi ambazo zinasababisha ukuaji wa mji ule zinakwenda kugusa mamlaka za sehemu nyingine ambazo watendaji wa Wilaya ile hawana mamlaka nazo.

Nini nafasi ya Serikali katika kurasimisha maeneo hayo kabla ujenzi holela haujaendelea?

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA
MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Priscus Jacob Tarimo, Mbunge wa Moshi Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Manispaa ya Moshi ina eneo dogo, na katika kupanuka kwake inabidi iguse na maeneo mengine ambayo yako nje ya utawala wa Manispaa ya Moshi. Lakini taratibu za Serikali ziko wazi, pale ambapo maeneo ya utawala yanatakiwa kuongezwa ama kupunguzwa, taratibu lazima zifuatwe kupitia Wizara ya TAMISEMI ili kuweza kujua uhalali wa kuweza kuongeza eneo waweze kupata kama wanavyohitaji. Vinginevyo hawawezi kufanya zoezi katika eneo ambalo si la Manispaa, isipokuwa waliopo Moshi DC wanaweza wakafanya zoezi la urasimishaji na kupanga maeneo yao kutokana na sheria inayo…