Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Chake Chake
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nianze kwa kusema kwamba miaka mitatu inatosha kujitathmini kile tulichopanga na tulichofanya na sasa tukaja na mpango mpya. Kwa miaka mitatu tulipanga kutumia trilioni kadhaa, mwaka 2015/2016 tulipanga shilingi trilioni 29, mwaka 2016/ 2017 tukapanga shilingi trilioni 31 na mwaka 2017/2018 tukapanga shilingi trilioni 32 hizo tulizoziandika. Hii inatosha kujitathmini kwamba mipango yetu tuliyopanga na kile tunachokifanya ni realistic? Kwa hiyo, ni lazima tujiulize are we realistic kwa tunachokipanga na tunachokifanya kama Serikali? Hilo ni la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili nililisema kwenye Mpango wa 2016/2017 na jana kalisema Mheshimiwa Silinde, mimi naona hakuna succession plan kwamba awamu hii na awamu hii wanapeana vipi mambo yao. Ilivyo sasa awamu hii anatoka na kitabu chake na awamu ijayo anakuja na kitabu chake kipya kabisa which is quite different. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na suala la Katiba Mpya. Katiba Mpya imetumia mamilioni ya pesa za Watanzania. Sasa hivi watu humu wanapita wanasema aah, ilikuwa mambo ya kisiasa, eeh! Katika legacy ambayo ataiacha Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, katika legacy muhimu kuliko zote mnazoziona leo, basi ni kuandika Katiba Mpya ya Watanzania. Kama leo mnaona Standard Gauge Railway na Stieglers’ Gorge leo ni ya msingi, basi Katiba Mpya ni ya msingi zaidi kwa vizazi na miaka 100 ijayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimelisema hili kwa sababu, Rais wa awamu iliyopita, Mheshimiwa Kikwete alileta Katiba Mpya, imefikia katika hatua za mwisho kumalizika tumeiacha tunasema kwamba hatuna mpango nayo. Sasa hivi awamu hii ya Rais John Pombe Magufuli imekuja na Stieglers’ Gorge, imekuja na Standard Gauge Railway, imekuja na ATCL, atakuja Rais mwingine, tumefika Makutupora tunataka twende Mwanza - Isaka kwenye Standard Gauge Railway asipokubali…
T A A R I F A . . .
MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachozungumza ni mambo ya msingi, kwa sababu mimi Mheshimiwa Vuma ni rafiki yangu, acha tu aseme alichotaka kusema hakina shida.
Mheshimiwa Mwenyekiti, the issue is tunatumia rasilimali pesa ya Watanzania, tume-invest kwenye Katiba Mpya mabilioni ya pesa lakini sasa suala la Katiba Mpya tumeacha tumeanzisha Standard Gauge Railway, awamu itakayokuja 2025/2035 akisema kwamba mimi kipaumbele changu siyo Standard Gauge Railway, tunafanyaje? Atakapokuja mwingine akasema kwamba mimi kipaumbele changu siyo ATCL, tunafanyaje? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachoshauri kuwe na Kamati au Tume Maalum ambayo inaratibu hii miradi ya kimkakati kwa nchi ili rasilimali zisipotee burebure, tumepoteza mabilioni ya pesa. Kila mtu akija na kitabu chake, Tanzania maisha yote tutalaumiana, humu tutakuja kuchekeshana, lakini hatutafika pale tunapotaka, ni lazima kuwe na succession plan, ni lazima kuwe na Tume itakayoratibu masuala ya Kitaifa ya kimkakati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimemsikia Rais mara mbili, mara ya kwanza alisema ataendelea pale alipomalizia Rais wa awamu iliyopita, lakini mara ya pili amesema hana mpango wa kutenga pesa ya Katiba Mpya. Mimi naomba nimshauri Waziri Mkuu, yeye ni msimamizi wa Serikali katika Bunge hili, Rais ni mtu, inawezekana ameteleza, inawezekana amekosea, Mheshimiwa Waziri Mkuu nenda kamshauri Rais juu ya Katiba Mpya, ni lazima irudi kwa Watanzania amalize mchakato huu na legacy yake itakuwa kubwa zaidi kuliko kitu kingine chochote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia, Mheshimiwa Waziri Mkuu rudi kwa Mheshimiwa Rais, mimi ni mdogo sana, rudi kwa Mheshimiwa Rais kamshauri, mwambie yeye ni binadamu kama sisi as long as amepewa tu mamlaka ya kuongoza nchi hii, ni binadamu anaweza akakosea. Nenda kwa Rais mshauri tena kuhusu suala la Katiba Mpya amalize hapa palipobaki, ataacha legacy kubwa kuliko vitu vyote atakavyoviacha kwa muda mwingi utakaokuja au vizazi vyote vinavyokuja Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni mahusiano. Nataka nizungumze kidogo kuhusu mahusiano ya washirika wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na nitazungumza kwenye vitu viwili tu, kwanza suala la VAT kwenye umeme. Suala hili pengine halitakiwi kuzungumzwa lakini tumelizungumza kwenye mipango yote kwamba Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania si nchi nje ya Tanzania. Sisi tunauza umeme, sisi tunanunua umeme VAT hiyo haipo. Kwa hiyo, sasa imefika muda Mheshimiwa Waziri wa Fedha alichukue na alilete kwenye mpango na kwenye bajeti liishe.
T A A R I F A . . .
MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeipokea tarifa hiyo ya Mheshimiwa Jaku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nachotaka kusema ni kwamba miaka mitatu tunaenda mwaka wa nne tunazungimzia suala hili. Mara tunaambiwa kaeni na Wizara ya Nishati na Madini ya wakati ule mta-solve, mwaka wa pili inaenda hivyo hivyo, mwaka wa tatu hivyo hivyo, huu ni mwaka wa nne, sasa ni muda wa Serikali kutekeleza jukumu lenu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi ni nchi washirika. Zanzibar siyo Rwanda au Burundi, Zanzibar ni nchi ndani ya Muungano huu, ni washirika, hatuwezi kuuziwa umeme tofauti. Mnawauzia umeme Zambia lakini hakuna VAT hii, Kenya mnanunua Kenya mnanunua hakuna VAT hii, kwa nini Zanzibar?
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.