Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kupata fursa hii ya kuchangia mpango wetu wa maendeleo. Kidhati kabisa nichukue fursa hii kumshukuru Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake na watendaji ambao wamewezesha kutuletea kitabu hiki kwa sababu natambua kwamba, siyo kazi rahisi, lakini imewezekana na imekuja tumeanza kujadili toka juzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maeneo machache ya kuzungumza. Nianze kwa kutambua achievement moja ambayo imepatikana katika Serikali ya Awamu iliyopita na Awamu hii, hususan katika utekelezaji wa mipango yetu kwa upande wa establishment na implementation kwa Tanzania Agricultural Development Bank ambayo imekuwepo kwa lengo la kusaidia ukuaji wa kilimo kupitia katika sekta mbalimbali lakini vilevile kupitia kwa individual. Mheshimiwa Mbene alizungumza despite kwamba TADB ipo na inaendelea na utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kifedha lakini bado tabu ipo palepale. Kwa maana kwamba individual ambaye amejishirikisha na kilimo akitaka kupata mkopo gharama inakuwa kubwa kwa sababu kwanza TADB requirement yao lazima upitie PASS (Private Agricultural Sector Support) ili wakuandikie plan ambayo mara nyingine inakuwa very expensive kwa mtu ambaye anataka production kwenye kilimo. Tumeweka hiyo TADB lakini masharti yake yamekuwa sawasawa na benki nyinginezo, kwa hiyo, utaona kwamba kumekuwa na ugumu uleule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ingekuwa vizuri kama tumeweka TADB kwa ajili ya kusaidia kilimo isiwe TADB inafanana na commercial banks nyingine. Lazima kuwe kuna utaratibu ambao umewekwa specifically kwa ajili ya kuwapatia mikopo. Inawezekana kabisa rate ni ndogo TADB ukilinganisha na banks nyingine lakini ile gharama ya acquisition ya mkopo yenyewe inakuwa ni kubwa kwa sababu anakumbana na vikwazo vingi. Kwa hivyo, tunaomba TADB utaratibu wa kuwakopesha wakulima pamoja na kampuni zinazojishughulisha na kilimo uangaliwe upya ili tuweze kuona kwamba tunafikia malengo tunayokusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilikuwa nataka kuzungumzia ni katika ukurasa wa 42, udhibiti wa katika matumizi ya fedha za umma, imetokana vilevile na ukurasa wa 41, mahitaji ya rasilimali fedha. Ni jambo zuri katika mambo yote yaliyotajwa kwamba kuhakikisha kuwa kampuni zote ambazo Serikali ina hisa zinaendeshwa kwa ufanisi na hivyo kutoa gawio stahiki kwa Serikali. Ni jambo zuri sana na mimi napata moyo sana kwenye hili kwa sababu kuna sehemu nyingine ambapo Serikali tumekuwa na hisa lakini kweli hatupati gawio kama inavyokusudiwa. Tunaweza kuwa tunapata gawio lakini sio kama inavyostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba nimkumbushe Mheshimiwa Dkt. Mpango, kuna mashirika mengine ya Serikali ambayo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanatoa gawio, Zanzibar haijawahi kupata stahiki yake katika magawio ambayo yapo katika mashirika ya Muungano. Tunaomba katika usimamizi wa utaratibu huu kwa mpango huu Zanzibar iwe inapata gawio stahiki kutokana na mashirika ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo Zanzibar ni sehemu yake nayo inaingia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini si hilo tu, vilevile katika usimamizi wa taasisi na mashirika ya umma, tuhakikishe mashirika ya umma yanajiendesha kibiashara, yanaandaa mwongozo wa gawio utakaotoa utaratibu wa malipo ya gawio kwa Serikali. Hili limeanza kufanyika, nadhani tumeshuhudia sio mbali Mheshimiwa Rais akipokea gawio kutoka katika mashirika yetu ya umma. Kuna mashirika baadhi ya mashirika ni ya Muungano lakini Zanzibar kabisa haijapata senti katika gawio ambalo limetolewa na ni gawio stahiki kabisa kwa hivyo, tunaomba hilo liangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa taasisi ya umma ambayo inatoa gawio ni Benki Kuu ya Tanzania, hakuna gawio lingine linalotoka katika taasisi nyingine. Tunaomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha kuanzia mwaka huu wa fedha Zanzibar iwe inapata stahiki yake kama ilivyo kwa mujibu wa Katiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo huu umetambua sana umuhimu wa miundombinu kwa ajili ya ukuaji wa uchumi. Katika aspect hiyo, imeongelea kabisa ujenzi wa bandari, ujenzi wa barabara pamoja na viwanja vyetu vya ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana wakati nachangia mpango na niliuliza kwa nini mpango huu hauja- integrate Zanzibar, nilipata majibu ambayo kwa wakati ule pengine yalikuwa valid kwamba katika Katiba iliyopendekezwa tunakusudia kuweka Tume moja ambayo itashughulikia mipango. Sasa hivi hatuna matumaini ya Katiba Mpya, Mheshimiwa Dkt. Mpango tunafanya nini, as a follow back position? Kwa sababu huu mpango Zanzibar haimo ni sawa, lakini utekelezaji wake kwa namna yoyote uta-integrate masuala ya Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye masuala ya bandari, kuna barua imeandikwa sijui toka lini kwa ajili ya acquisition ya mkopo kutoka Exim Bank ya China kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri Zanzibar. Document inakwenda inarudi, kwa Mwanasheria imerudi, kwa maoni ya Kamati imerudi, kwa NDMC imerudi, miaka nenda miaka rudi. Kwa taarifa nilizozi-dig out hii Bandari ya Mpiga Duri imeanza kuzungumzwa miaka 25 iliyopita, hakuna kinachoendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu bandari ni kichocheo kikubwa sana cha uchumi hususani uchumi wa visiwa, tunaomba vile unavyo-feel kwamba huu mpango aspect yake kubwa ni pamoja na miundombinu, feel kwa Zanzibar aspect ya ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri. Aspect ya ujenzi wa Terminal III iko katika ngazi zenu, tunaomba mliangalie hili ili sasa na uchumi wa Zanzibar ambao hauja- integrate humu kwenye mpango na wenyewe uweze kuendelea kutokana na mipango ile ambayo itatekelezwa. Tunaweza kule kutengeneza mpango lakini unahusika na wewe moja kwa moja, tunaomba sana hili lizingatiwe tena lizingatiwe kweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitabu cha Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nadhani na wao wanafanya research na wanakuja na alternative. Kuna taarifa hapa imenishtua kidogo hususani ukurasa wa kwanza wanasema kwamba kiwango cha umaskini Tanzania kimefikia asilimia 47, hii ni taarifa ya kutisha na haiwezekani kabisa. Wakati tunafanya research zetu ni lazima tuangalie vyanzo sahihi vya information kwa sababu document hii wanaweza wakaja wengine wakasema kama ni reference document. Unaandika taarifa ambayo tumem-quote William Atwell, mimi nimekuwa very much interested nimekwenda kumtafuta huyu William Attwell ni nani? Yeye mwenyewe katika taarifa ambayo iko kwenye website ya Frontteers Strategy Group amekuwa quoted huyu hiyo asilimia 47 ameipata yeye kutokana na recent visit yake kwa East African countries. How could you just to have a recent visit ukaweza kupata estimate ya 47% ya population. Nadhani this is very wrong. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jumba lina dhamana kubwa katika nchi hii. Sina uhakika kwenye Kanuni zetu lakini just kutoa taarifa kwenye blogs halafu tunakuja tunazileta hapa ndiyo zisaidie maendeleo ya Taifa hili, it’s just very wrong. Tunatarajia takwimu sahihi katika vyanzo vya kuaminika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haraka haraka nimekwenda kwenye website ya World Bank, taarifa ambayo imetolewa mwaka 2017 inasema Tanzania basic poverty line ni 28% lakini food poverty line ni 10%. Sasa tunasema hii 47% imepatikana wapi? Tunaomba sana pamoja na mambo mengine Kanuni zetu ziwe zinazingatia takwimu sahihi kwa sababu wananchi wanaotuamini wanaweza waka-quote hii kama ni takwimu sahihi, hususani kwenye hizi blogs inakuwa ni mawazo ya mtu mwenyewe binafsi rather than kuwa takwimu sahihi.