Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika, nami nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia kwenye taarifa mbili za Kamati. Nazipongeza taarifa zote mbili ile ya Kilimo na ile ya Maliasili ambayo mimi ni Mjumbe wake.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameona kilio cha wakulima na wafugaji ambapo wamenyanyaswa sana hasa wafugaji na wameonewa kwa miaka mingi na ametoa tamko na ameagiza Mawaziri walishughulikie suala hili kwa haraka. Tamko hili linaweza kuchukuliwa tofauti na likichukua muda bila kufanyiwa kazi watu wataingia ndani ya hifadhi na kuharibu uhifadhi wakisema kwamba walikuwepo miaka mingi. Kwa hiyo, tunaomba Mawaziri waliopewa jukumu hili wachukue hatua za haraka kuhakikisha kwamba tamko hili la Mheshimiwa Rais linafanyiwa kazi kwa haraka ili kuokoa uhifadhi.

Mheshimiwa Spika, tunapoongea yapo maeneo ambapo watu walikuwa wametoka miaka mingi kwa mfano Bonde la Kilombero lakini baada ya lile tamko tunaona wanarudi kule kwenda kulima kwa matreka usiku na mchana. Kwa hiyo, hili litakuwa ni tatizo kama hatua za haraka hazitachukuliwa, tutakuwa tunakwenda kuharibu uhifadhi. Naomba tamko hili lifanyike kwa uhakika ili migogoro ya wakulima na wafugaji iweze kuisha na waweze kupata maeneo ya kufugia na kulima.

Mheshimiwa Spika, niende kwenye National Housing. Kwa miaka mingi National Housing imefanya kazi nzuri na baada ya kuwepo kwa Mkurugenzi Mkuu aliyeondoka, Ndugu Mchechu. National Housing kwa mwaka 2010 mpaka 2018 wameweza kutengeneza mtaji kutoka shilingi trilioni 4.3 na walikuwa na projection ya kwenda kwenye shilingi trilioni 7 mwaka 2025 lakini National Housing leo ni kama iko stacked, imetulia. Walikuwa na miradi mingi ya strategic kama Mradi wa Kawe na Morocco lakini miradi ile imesimama wakati wameshawekeza fedha nyingi na mingi iko zaidi ya 40% ya utekelezaji wake.

Mheshimiwa Spika, tunaiomba Serikali kwa kuwa wamezuiliwa sasa kuchukua mikopo kuendeleza miradi ile Serikali ione mikopo iliyowekezwa pale inazalisha riba waweze kutoa kibali waweze kuiendeleza ili kuokoa fedha ambayo imewekwa pale lakini pia National Housing iendelee. Tusipoangalia Shirika ambalo tumelipongeza miaka mingi litakufa kwa sababu tu ya watu ambao walikuwa wana maslahi yao.

Mheshimiwa Spika, tunajua wako watu wengi sana walitamani National Housing, miaka mingi lilikuwa ni shirika ambalo linamilikiwa na watu, nyumba zilikuwa hazijulikani, ni kama lilikuwa si shirika la umma, walikuwa wanamiliki watu mikononi. Baada ya kuonekana kwamba nyumba sasa zimetambuliwa ni nyumba za umma, shirika linafanya kazi, linapendezesha miji yetu mikubwa, watu walipiga vita kubwa sana na wamefanikiwa. Serikali iangalie, si kila ushauri waupokee waangalie ushauri ambao unawezesha kupiga hatua kwenda mbele. Wengine walitamani tu kwamba viongozi waliokuwa wanasimamia Shirika lile wakae pembeni ili waendelee kupiga deal na huu ndiyo uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie shamba la miti la Sao Hill. Tumekwenda Sao Hill na nashukuru TFS kwa kazi nzuri sana lakini zipo changamoto. Tunaiomba Serikali, kuna utitiri mkubwa wa kodi zaidi ya 32 kwa wafanyabiashara. Tunajua wafanyabiashara wa Taifa hili ni wadau wakubwa wa maendeleo na Mheshimiwa Rais kila siku anasema, tunaomba kwanza kodi zile zipungue.

Mheshimiwa Spika, lakini kingine, kuna kodi moja ambayo inaitwa kodi ya cess. Bungeni mwaka jana tulibadilisha sheria ya cess kutoka 5% kwenda 3% lakini Mkoani Iringa bado cess ya mazao bado ni 5%. Si hilo tu wanatoza mara mbili; mti ukiwa porini unatozwa cess 5% na ukitolewa mbao unatozwa cess 5%, Halmashauri na Sao Hill wote wanatoza. Wafanyabiashara wanaumizwa na hawa ndiyo wadau wa maendeleo. Tunaomba kwanza cess iwe moja lakini pia kodi zipungue ili waweze kuchangia vizuri maendeleo.

Mheshimiwa Spika, tumekwenda pale kwenye kiwanda tumeangalia, zaidi ya malori 20 yana nguzo za REA yamekaa mwezi mzima yamezuiliwa kuondoka kwa sababu TANESCO inatakiwa kulipa cess kwa mara ya pili wakati nguzo hizo zimelipiwa cess zikiwa kule Sao Hill. Sao Hill inakusanya zile cess inatoa percent inapeleka kwenye Halmashauri. Leo mbao ziko kiwandani tayari kusafirishwa Halmashauri inasema hakuna kutoa nguzo mpaka ilipwe tena cess nyingine, kwa nini kuwe na double taxation? Tunaiomba Serikali ihakikishe kunakuwa na cess moja lakini pia kodi ziondolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni la LMD, kuna fedha ambayo wafanyabiashara wenyewe wamemua kuchanga…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)