Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kuridhia Ubadilishaji Hadhi Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika – Orugundu kuwa Hifadhi za Taifa

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kuridhia Ubadilishaji Hadhi Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika – Orugundu kuwa Hifadhi za Taifa

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi uliyonipatia pia niweze kuchangia azimio ambalo liko mbele yetu. Niishukuru pia Serikali kwa kuweza kusikiliza ushauri wa Kamati na kuweza kupandisha mapori haya ya akiba kuweza kuwa chini ya TANAPA.

Mheshimiwa Spika, ni matarajio ya wananchi wa maeneo yale kwa sababu maeneo haya yalikuwa ni mapori kutokana na kwamba Serikali ilikuwa haiwekezi kwenye mapori haya ya akiba na yalikuwa ni mapori kiasi kwamba ndiyo maana Wabunge wanasema kwamba yalikuwa ni vichaka vya majambzi na vichaka vya wezi. Matarajio sasa ya wananchi wa maeneo yale kwamba baada ya mapori haya kupandishwa kuwa hifadhi za Taifa watanufaika kikamilifu sana na uwepo wa hifadhi hizi jirani yao.

Mheshimiwa Spika, naomba pia niipongeze TANAPA kwa kazi nzuri wanayoifanya chini ya Mkurugenzi wake Mkuu na Watumishi wote wanafanya kazi kubwa sana lakini kwa mazingira magumu sana. Tunapowaongezea majukumu, lazima pia tuangalie namna ya kuwawezesha wapate finance ya kutosha kuweza kuwekeza kwenye mapori hayo. Kama TANAPA hawatawekeza kwenye mapori haya yakaweza kuwanufaisha wananchi wa maeneo yale kiukweli itakuwa ngumu sana kwa mapori haya kuweza ku-success kwa sababu bado ujangili utaendelea katika maeneo yale kwa sababu hawataweza kufanya doria za kutosha.

Mheshimiwa Spika, pia TANAPA wana miradi ya out reach, wana miradi inaitwa miradi ya “ujirani mwema” ambapo wanawawezesha wananchi wa maeneo yanayowazunguka kuwajengea miundombinu mbalimbali ya elimu, ya afya na mambo mengine kiasi kwamba inawafanya wananchi wanaona sasa maeneo yale ni maeneo yao. Kwa hiyo kama TANAPA wasipowezeshwa waweze kutoa miradi ya ujirani mwema wananchi hawa hawataona umuhimu wa kuweza kuyatunza maeneo haya. Kwa hiyo naiomba sasa Serikali wakati wanaiongezea TANAPA mzigo wa majukumu ya kazi pia waangalie namna ya kuwawezesha ili waweze kufanyakazi hii kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, TANAPA pamoja na kufanya kazi yao vizuri, kutunza mapori 16 na sasa hivi wameongezewa mengine na wanaendelea kuongeezewa, lakini pia wanalipa kodi zote stahiki kwa Serikali. Naiomba Serikali, kwa kuwa tunaiongezea TANAPA majukumu, TANAPA iliambiwa kulipa 10 percent ya mapato yake yote kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, kwa kuwa sasa tunaiongezea TANAPA majukumu mazito zaidi, tupungue ile asilimia inayokwenda kwenye Serikali Kuu ili sasa wabaki nayo kwa ajili ya kuwezesha mapori haya ambayo tunawapa. Tuangalie Ruaha imeshindwa hata kutengeneza barabara vizuri kutokana na kwamba kipato chao ni kidogo.

Mheshimiwa Spika, mapori haya haya tuliyoyafanya kuwa chini ya TANAPA, sasa pia yanahitaji utangazaji, lakini pia yanahitaji kuweza kuhakikisha kwamba miundombinu yake kule ndani inakuwa mizuri. Kwa hiyo pamoja na nia nzuri ya Serikali, kama mapori haya hayatawezeshwa, lakini pia wananchi wale waone faida zake kuhakikisha kwamba hakuna migogoro. Leo TANAPA kuweza kuondoa migogoro kwenye maeneo kama Mikumi, hakuna migogoro kabisa na maeneo mengi wametumia rasilimali kubwa, wamefanya kazi kubwa kwa hiyo migogoro ya ardhi, maeneo ya jirani yakiwa kila siku haiishi bado TANAPA watakuwa na mzigo mkubwa wa kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, naiomba sasa Serikali kwanza ifanye kazi kubwa kuhakikisha kwamba maeneo yale ambayo wananchi wale wamezunguka ihakikishe kwamba inasaidiana na TANAPA kuweza kuhakikisha kwamba wananchi wale wanakubali maamuzi yale yaliyofanywa na Serikali ili waweze kukubali kwamba maeneo yale yatakwenda kuwanufaisha lakini siyo kwa maneno, waone kwa vitendo kwenye maeneo yao. Waone hospitali zinajengwa, waone shule zinajengwa, waone vituo vya afya vinajengwa, waone miundombinu yao inawezeshwa ili wawe part and parcel ya maeneo haya ambayo yameweza kupandishwa hadhi kuweza kuwa hifadhi za Taifa.

Mheshimiwa Spika, naunga hoja hii mkono kwa malengo kwamba Serikali ihakikishe kwamba TANAPA inawezeshwa vya kutosha na hasa ile 10 percent ya mapato makubwa kwenye Mfuko wa Serikali ipungue iwe five percent ili percent inayobaki iende kuwekeza kwenye mapori ambayo tunaipa TANAPA mzigo wa kuweza kuendesha.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.