Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa utukufu aliyenijalia kusimama hapa siku hii ya leo. Pili, nikushukuru wewe kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia kwenye taarifa za utekelezaji wa shughuli za Kamati za Bunge za mwaka 2018/2019 ambazo ni Kamati za Maendeleo ya Jamii, Serikali za Mitaa na UKIMWI.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba niende kwenye suala linalohusu maboma. Katika maboma ambayo yamejengwa na wananchi kwenye suala la afya na elimu ikiwa ni madarasa pamoja na zahanati na vituo vya afya ni mengi sana katika nchi hii. Inapotokea kwamba nguvu za wananchi ambazo zimetumika, wananchi ambao wamejitolea kwa dhati kabisa kujenga maboma yale na ikaonekana kwamba nguvu za wananchi hawa zinapotea bure wananchi hawawezi kuielewa kabisa Serikali dhidi ya nguvu zao ambazo zinapotea bure. Kwa hiyo, naomba Serikali iangalie namna ya kuweka mkakati wa makusudi kabisa kuhakikisha kwamba maboma yale yanamaliziwa na watoto wetu waweze kuanza kuyatumia kwa madarasa lakini pia zahanati na vituo vya afya vianze kutumika haraka iwezekanavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie suala la Local Government Development Grant. Huu mfuko ulikuwa unasaidia sana Halmashauri zetu, najiuliza ni kwa nini Serikali imeondoa Mfuko huu? Kama kulikuwa na changamoto zozote kwa nini Serikali isi-maintain Mfuko huu ili mwisho wa siku uweze kuendelea kusaidia katika Halmashauri zetu?

Mheshimiwa Spika, kuna suala linahusu TARURA. TARURA ni jambo ambalo limeletwa kama ugatuaji wa madaraka katika Serikali za Mitaa. Hata hivyo, TARURA huyu yeye ni kama wakala tu katika Halmashauri hizo kwa sababu barabara ni Halmashauri lakini pia hata fedha ni za Halmashauri. Mimi nashangaa sana huyu TARURA anaposhindwa kuwa ni miongoni mwa wajumbe ambao wanashiriki kwenye vikao vya Mabaraza ya Halmashauri zetu ili wale Madiwani waweze kusema ni barabara ipi ambayo inatakiwa itengenezwe badala ya TARURA wao kukaa tu kama kakikundi pembeni wakaanza kujipangia wenyewe kwamba tunakwenda kutengeneza barabara hii, barabara hii bila kujali kipaumbele cha wananchi ambao wanawakilishwa na Madiwani ambao wanajua kipaumbele cha barabara za kutengenezwa.

Mheshimiwa Spika, nilidhani kwamba utaratibu huu ungerekebishwa. Nitole tu mfano, anakuja mtu anaingia nyumbani kwako, anaanza kuchukua sufuria jikoni, anakwenda chumbani kupika, anavuruga utaratibu. Kwa hiyo, ni vizuri hawa TARURA wakashirikishana na wakawa
wanaripoti kwa Halmashauri ili waweze kubainisha vizuri zile barabara na taratibu zote ziweze kwenda sawia. Nachoamini ni kwamba Diwani wa Halmashauri au Halmashauri haitakuwa na mamlaka ya kupanga au kutafuta wazabuni lakini hata kuelekeza tu kwamba nadhani barabara hii kutoka sehemu fulani mpaka sehemu fulani ingefaa itengenezwe kwa sasa kulingana na changamoto iliyopo, nayo pia wananyimwa? Ni jambo gumu sana.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa niende kwenye suala la watumishi wa Halmashauri. Kwenye suala la afya na elimu kuna changamoto ya watumishi hasa hapa kwenye suala la afya. Zahanati zetu unakuta labda kuna Daktari mmoja au sehemu nyingine hakuna Daktari kabisa ni Mhudumu tu wa kawaida kama Nesi anafanya kazi za udaktari, huyo huyo azalishe na shughuli nyingine, kwa hiyo, kumekuwa na shida kubwa sana. Utendaji kwenye zahanati zetu na vituo vya afya hauridhishi mwisho wa siku tutaendelea kuwaumiza wananchi wetu, watakuwa hawapati matibabu yale yanayostahili kulingana na vile ambavyo ingefaa.

Mheshimiwa Spoika, sasa naomba niende kwenye suala la UKIMWI, naomba hapa mnisikilize kwa makini sana. Tanzania 90, 90, 90 inawezekana lakini inawezekana pale tu ambapo kutakuwa na ruhusa ya watu kujipima wenyewe. Kuna watu wengine wanaona aibu kwenda kupimwa kwenye vituo vya upimaji hasa wanaume. Hawa ndiyo wamekuwa wakifanya kazi ya kusema kwamba maadamu wewe umepima basi tutakuwa tuko sawa, siyo kweli. Ni kwa sababu tu wanaona aibu kwenda kupima lakini utaratibu wa kila mtu kujipima mwenyewe utakuwa ni mzuri zaidi, mnaweza mkakaa watu wawili wenyewe mkajipima, ukampima mwenzako na wewe ukampima mkapata majibu hapo hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia katika suala la UKIMWI kuna suala la mkono sweta. Mkono sweta kwa utafiti ambao umefanyika…

SPIKA: Mheshimiwa Jaqcueline, Kiswahili hiki sijui kama kila mtu anelewa ni kitu gani hicho. (Kicheko)

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, mkono sweta ni wale wanaume ambao hawajatahiriwa. Hili jina wamejaribu kuliboresha sana badala ya kuliita govi wamesema mkono sweta angalau limeboreshwa boreshwa. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, mkono sweta ni janga.

T A A R I F A

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, nimeipokea kwa mikono miwili na nashauri tuanze na Wabunge wote humu ndani ambao pengine watabainika hawajafanya hiyo tohara basi wafanyiwe mara moja. (Kicheko/Makofi)

SPIKA: Bahati mbaya hoja yako haikuungwa mkono. Endelea Mheshimiwa. (Kicheko)

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, naomba nilindie dakika zangu.

Mheshimiwa spika, suala la mkono sweta ni tatizo kubwa. Ili kufikia 90, 90, 90 ni lazima tuhakikishe kwamba mikono sweta yote inaondolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utafiti uliofanyika unaonyesha kwamba mkono sweta umekuwa ukiambukiza magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa UKIMWI. Maambukizi ni kwa mwenye mkono sweta lakini pia kwa mwanamke kwa asilimia 60. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda niseme ni namna gani ambavyo unaambukiza UKIMWI lakini pia umekuwa ukiambukiza kansa. Endapo mkono sweta ule umekutwa na virusi aina ya human papilloma virus ni rahisi kumuambukiza mwanamke virusi hivyo ambavyo mwisho wa siku mwanamke anakuwa anapata kansa ya kizazi. Kwa hiyo, naomba sana…

T A A R I F A

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, kwa kweli sasa naongea kwa masikitiko sana. Pale unapoona kwamba hawa wanaume wenye mikono sweta wanakwenda kuwaambukiza wanawake wenzetu ikiwemo pengine na wanawake wengine kama itatokea…