Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nashukuru kupata nafasi nami niweze kuchangia katika hoja hii iliyo mezani inayohusu Kamati Tatu za Kudumu za Bunge. Kwa sababu ya muda naomba niende haraka haraka tu.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli napongeza Kamati zote tatu, viongozi wao pamoja na Wanakamati wote kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wameifanya, tumezisikia ripoti zao, zimekaa vizuri, wala hakuna shaka yoyote juu ya hiyo. Tunachokifanya hapa ni kujaribu kuongeza nyama kidogo, lakini kuweka msisitizo kwa baadhi ya mambo ambayo wameyazungumza wenzetu kwenye ripoti zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa haraka haraka niseme kwamba sasa Serikali yetu ya Awamu ya Tano iliyoko madarakani imemaliza miaka mitatu. Ni kazi kubwa ambayo imeshafanyika sasa hivi, kila mtu anaiona. Kazi hii ndiyo ilikuwa chanzo cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli kusema kwamba katika awamu hii yeye anasema Hapa Kazi Tu. Katika Serikali ya Awamu ya Tano bila kuwa na Hapa Kazi Tu, mambo makubwa yanayotendeka yasingeweza kutendeka kufikia hapa tulipofika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba Serikali iliamua kwa dhati, kwa kauli moja kwamba tuijenge Tanzania ya Viwanda ambayo itaisaidia nchi hii kuvuka toka katika uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati. Hizi ndizo kazi kubwa zinazofanywa na Wizara mbalimbali. Kati ya Wizara hizo, ziko Wizara ambazo zinasimamiwa na Kamati hizi tatu ambazo tunajidiIi hapa leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikizungumzia kwa uchache kabisa, Kamati ya TAMISEMI, tunazungumzia masuala ya elimu. Katika elimu, Awamu ya Tano walisema Elimu Bila Malipo. Elimu Bila Malipo bila kumung’unya maneno, imekuwa na matokeo chanya sana kwa Taifa letu, tunawapongeza sana. Tulikuwa na kampeni ya kuhakikisha watoto wetu wote wanaingia darasani na wanakaa kwenye madawati, tulifanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kupitia kauli hii ya Elimu Bila Malipo, sasa hivi tatizo la madawati limerudi pale pale, kwa sababu watoto walioandikishwa kuingia Darasa la Kwanza wamekuwa wengi kuliko vile ilivyotegemewa. Kazi kubwa bado tunayo mbele, tunatakiwa tuifanye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, kuna maboma mengi ya madarasa na nyumba za Walimu ambayo yanahitaji kumaliziwa. Tunafahamu Serikali inatoa rai kwa Halmashauri zetu kuhakikisha kwamba maboma yote yanakamilishwa ili yaweze kutumika inavyostahili.

Mheshimiwa Spika, naomba kupitia hadhara hii leo kwamba siyo Halmashauri zote ambazo zina uwezo wa kukamilisha maboma hayo kwa muda mfupi. Kwa hiyo, naiomba Serikali zile Halmashauri ambazo kwa sababu moja au nyingine zinapata shida kuyakamilisha maboma, kwa Serikali iwaunge mkono ili maboma haya yaishe, watoto waingie madarasani waweze kusoma.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo kwa haraka haraka kabisa, tunaipongeza Serikali sana kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67, ujenzi wa Vituo vya Afya 350 katika Wilaya mbalimbali na Kata mbalimbali. Hata hivyo, huko nako kuna tatizo kubwa la maboma. Naendelea kuiomba Serikali ijaribu kuzisaidia Halmashauri ambazo haziko vizuri kuhakikisha kwamba nao wanaweza kukamilisha maboma hayo na wananchi waweze kupata huduma inayostahili kama tulivyokuwa tumekusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kuzungumza suala zito na muhimu kabisa la majisafi na salama. Bado tatizo la majisafi na salama ni kubwa sana katika vijiji vyetu, pamoja na vijiji ambavyo kwa kweli…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Joel.

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, naunga mkono hoja Kamati zote tatu. Ahsante sana.