Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

TAARIFA YA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE KUHUSU SHAURI LA KUDHARAU NA KUDHALILISHA BUNGE LINALOMKABILI NDUGU PROF. MUSSA ASSAD, MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

TAARIFA YA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE KUHUSU SHAURI LA KUDHARAU NA KUDHALILISHA BUNGE LINALOMKABILI NDUGU PROF. MUSSA ASSAD, MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza niungane na Kamati kwamba ni kweli maneno yaliyotumika yalikuwa siyo mazuri. Nitoe tahadhari tu kwa wenzangu wengine, hapa kuna watu walisema Waheshimiwa Wabunge wanasinzia. Tulifurahi Wabunge wote kwa kuletwa mbele ya Kamati mtu aliyesema hivyo. Aliletwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hapa Makonda, alikosea; aliletwa Mheshimiwa Mnyeti hapa kwamba alikosea na sote tulikubali kwamba alifanya jambo siyo zuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie katika mantiki moja, kwa nini naunga mkono? Bunge jukumu lake ni kusimamia na kuishauri Serikali, lakini CAG ni part ya Bunge, yeye ndiye anayeona vitu, analeta katika Bunge na Bunge tunafanyia kazi. Katika collective responsibility yeye CAG ni part ya Bunge, haiwezekani kwa mtu kama yeye peke yake akasema sisi ni dhaifu halafu na sisi dhaifu bado aendelee kufanya kazi nasi. Hicho kitu hakitawezekana. Siyo kitu kizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Profesa Assad yeye ni CAG, tumempa Kamati ya LAAC anafanya kazi, tumempa Kamati ya PAC anafanya nayo kazi; na kama ilikuwa mahali pa kusemea, ni kule. Kwenda kusema udhaifu nje ya sehemu ya mipaka yake ya kazi hapo amedhalilisha. Kuna msemo wa Kiswahili unasema, akutukanaye hakuchagulii tusi. Pia mshairi mwingine anasema kwamba ndugu akufukuzaye, hakwambii kwangu hama. Ukiambiwa dhaifu, ina maana kuna jambo kubwa zaidi unaloambiwa. Viile vile akutukanaye hamtaji mama yako. Kwa hiyo, kudhalilishwa siyo lazima utajiwe kwamba mwana kadha kadha, hata hili ni jambo la kudhalilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Bunge ndio ambao tumeona hicho kitu. Kwa hiyo hicho kitu kinaudhi. Kuna mtu mwingine hapa nimpe tahadhari tu, ukizungumzia haki, uhuru na uwazi wa kutoa taarifa au kufanya mawasiliano, siyo kwamba umdhalilishe mwenzio. Katoe taarifa, unayo haki hiyo. Kafanye mawasiliano. Unayo haki ya kufanya mawasiliano, lakini siyo utoe taarifa za kumkashifu mwenzio. Ukitoa taarifa za kumkashifu mwenzako, ina maana kwamba umemkosea yule mtu, unapomalizia wajibu wako, ndipo haki ya mwenzako inapoanza. Kwa hiyo, nami nazungumzia hili neno udhaifu siyo neno zuri na shahidi amekiri kwamba yeye alilisema hili neno, lakini anajaribu kukengeuka kusema kwamba hiyo siyo tafsiri yake, yeye anatumia tafsiri ya kihisabati. CAG hatujampa kazi ya ku-access Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mheshimiwa mmoja hapa alisema kwamba taaluma yake ndio inayomfanya kwamba yeye aseme hivyo, hakuna taaluma ya kuli-assess Bunge akajua upi udhaifu wa Bunge? Yeye ana taaluma ya ku-assess account akaleta taarifa kwa Bunge katika Report na Bunge ndiyo linafanyia kazi. Sasa yeye sijui ka-assess wapi hilo Bunge akagundua kwamba kuna udhaifu. Hawezi kujua, hana kipimo. Kwa hiyo, hapa amekusudia kulifanyia vibaya Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
(Makofi)