Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nianze kwa kuishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa Magufuli kwa uimara wake katika kuendesha vyema nchi jambo ambalo limewezesha kuleta matokeo mengi mazuri. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Watendaji wake wote kwa kuweza kuitengeneza na kuiwakilisha hotuba hii kwa ufasaha wa hali ya juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo, kwanza ni kuhusu ziara za viongozi wa Serikal. Napenda kuchukua nafasi hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa viongozi wote wa Serikali namna wanavyofanya ziara katika nchi yetu. Hili ni jambo zuri ambalo linaamsha ari kwa sehemu zinazotembelewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba naomba ziara za viongozi wa taasisi za Muungano ziendelee kwa pande zote za Muungano. Kwa kuwa ziara hizi pamoja na mambo mengine zinaimarisha Muungano ni vyema zikatiliwa mkazo kwa kuwekewa mpango maalum wenye msisitizo wa kutembelea sehemu hizi za Muungano ili kuimarisha na kuchochea maendeleo katika Jamhuri yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nizungumzie uwekezaji. Naipongeza Serikali yetu kwa juhudi kubwa inayochukua katika kutilia mkazo uwekezaji katika nchi yetu. Uwekezaji ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya uchumi katika nchi. Aidha, uwekezaji unachochea upatikanaji wa ajira kwa watu wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri ambayo yatawavutia wawekezaji wa ndani na wa nje kwa kuweka miundombinu rafiki itakayorahisisha uwekezaji. Aidha, Serikali iweke mazingira bora yatakayoondoa urasimu wa upatikanaji ruhusa ya uwekezaji kwa wageni na wazawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.