Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Iringa Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana kwa kunipa nafasi lakini nalidhani Serikali ingekuwa inavumilia ikatujibu kwenye hoja, sisi ndivyo tunavyoona, hayo ni maoni ya Kambi ya Upinzani. Naona mnaogopa kivuli chenu wenyewe huku mnasema mmejipanga na tupo tayari kutoa ushahidi. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, jambo likishafanyiwa maamuzi usilete ushabiki ambao hauna maana. (Makofi)
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Toka Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani imefanya maamuzi makubwa matatu na maamuzi madogo madogo mengi ambayo kwa ujumla wake siyo chini ya 10. Serikali ya Awamu ya Tano ilifanya maamuzi ya Kikokotoo, korosho, Muswada wa Habari, Muswada wa Takwimu, kutokufanya kazi na CAG, Muswada wa Vyama Siasa, Stiegler’s Gorge, SGR, ununuzi wa ndege na kuhamia Dodoma. Is a major decision toka Serikali ya Awamu Tano imeeingia madarakani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya sifa za viongozi duniani ni pamoja na kufanya maamuzi (decision making), sina tatizo na hilo lakini tunapaswa tujue kama Taifa kwamba consequences are more important than decisions. Matokeo ya maamuzi tunayoyafanya ni ya muhimu zaidi kuliko maamuzi tunayoyafanya. We don’t live by decisions we live by consequences, hatuishi kwa maamuzi tunayoyafanya dakika moja tunaishi kwa matokeo ya maamuzi tunayoyafanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kabla ya kufanya maamuzi watu wenye busara, wenye hekima wanaoongoza lazima wajifunze consequences. You have to study the consequences before you make decisions. Unafanya research, unatafuta information, unatafuata historical data, unatafuta watu wengine wamefanya maamuzi gani katika mambo unayokwenda kuyafanya na unajifunza kwa watu wengine katika maamuzi unayokwenda kuyafanya. nimezungumza tumefanya maamuzi makubwa sana kama Serikali na Serikali tunazungumzia masuala ya utawala bora na Serikali za Mtaa, haya mambo yote lazima yawe synchronized ili tupate matokeo yaliyo bora. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukienda kwenye Kikokotoo, Mheshimiwa Jenista anahusika. Mlikuja hapa na nyimbo nyingi sana kuhusu Kikokoto na kwa mujibu wa taratibu ili sheria ije Bungeni inapitia hatua mbalimbali. Inaanza kwenye Wizara husika, inakuja kwenye Cabinet Secretariat, inakuaja kwenye MMC, Makatibu, inaenda kwenye Baraza la Mawaziri, inaenda kwa wadau inakuja Bungeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa baada ya kufanya maamuzi ya Kikokotoo tukapitisha kwa nyimbo nyingi sana hapa na tuliwaambia humu ndani, baada ya miezi mitatu mkaweka U-turn. Swali la kujiuliza, are we capable to lead this country? Kama kupitia hatua zote hizi mmefanya haya mambo yote ndani ya miezi kadhaa Kikokotoo kikageuka, mkarudi na ngonjera zingine za kukipinga Kikokotoo ninyi wenyewe hapo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais, ameteua wengine hapa Maprofesa, Madaktari, degree holders wanaoweza ku-scrutinize vitu, kuona kama vina hoja; think tank ya Ikulu, nasi Wabunge tunaowawakilisha wananchi hapa, tukaimba ngonjera nyingi bila kuangalia consequences. Tunaitumbukiza nchi kwenye matatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, lilikuja suala la Korosho hapa, tunasema tunataka tuwe na maendeleo, mkaondoka mpaka na azimio la kusifu maamuzi ya Korosho. Baada ya muda mfupi, leo tunaambiwa kangomba hawana makosa. Tuliitwa Kangomba sisi huku. You guys did you study the consequences of the decision you are making? (Makofi)
MHE. JOHN W. HECHE: Mnaita mhindi anunue kilo ngapi...
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi ambao mnasema mko fit kuiongoza nchi hii, did you study the consequences? Kama hiyo haitoshi, Muswada wa habari, nilitegemea maswali; kama nilivyosema inapitia maeneo yote hayo; Muswada wa Habari, mnataka kuniambia Mawaziri walikuwa hawajui kwamba unakinzana na Jumuiya ya Afrika Mashariki? Mmekuja hapa mmelazimisha, mnataka kusema mlikuwa hamjui, kama unakinzana na Jumuiya ya Afrika Mashariki! (Makofi)
MHE. JOHN W. HECHE: Na mli-ratify wenyewe.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi wenyewe Baraza zima la Mawaziri, mlileta hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, mkaleta takwimu, tukapitisha na azimio la kusema hatufanyi kazi na CAG. Leo vitabu vyake viko hapa na sahihi iko hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu kwenu, ninyi mnapofanya maamuzi, huwa mnajifunza consequences? Do you do research? Maprofesa mko hapa, huwa mnafanya research ili mfanye hayo maamuzi. Leo tumefanya maamuzi makubwa. Nia na dhamira nzuri ya Stiegler’s Gorge na Standard Gauge ni mambo mazuri ya kuhamia Dodoma na kununua ndege, vyote ni vitu vizuri. Ila consequences zinazotokea sasa hivi kwa maamuzi hayo makubwa ambayo tulikuwa hatuna priorities, ndiyo maana tunaona hamwezi kuajiri wafanyakazi wapya. Those are the consequences na hamkuliandaa Taifa kwamba hatutaajiri wafanyakazi wengine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna increment kwa wafanyakazi, mishahara haiongezeki, hakuna motisha. Halafu haya mambo makubwa mnategemea staff wataleta positive result katika mambo haya ambayo hamkufanya study? Asimame mtu hapa atuambie what are the consequences na tuta-suffer kipindi hiki bila kuajiri wafanyakazi wapya for how long? Leo mnasimama hapa mnasema, ukisikiliza hotuba za Mheshimiwa Rais, ni contrary kabisa na ninyi Mawaziri mnavyofanya kazi hapa, zote! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna Wizara moja tu ambayo mimi naiona Mheshimiwa Rais hazungumzi ni Wizara ya Ulinzi. The rest, kwenye mikutano yake huko, Wizara karibu zote, tulizungumza na Mheshimiwa Mpango, hayupo hapa leo; tulimwambia utaratibu wa kodi unaofanya haufai, leo Mheshimiwa Rais anasema yale yale tuliyosema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulizungumza mambo ya msingi mengi hapa hamkutusikiliza. Leo mnasema wawekezaji. Tuliwaambia mnafukuza wawekezaji, leo Mheshimiwa Rais ndiye analalamika kwamba wawekezaji wanakimbia. Why do you expect wawekezaji waje katika nchi ambayo hakuna democracy, hakuna good governance, hakuna kuelewana! Mnataka kupuuza kwamba sisi wote hatuna social capital katika nchi hii? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnataka kupuuza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani kwamba hana social capital katika nchi hii? Hatuna wafuasi katika nchi hii? Nani atakuwa na confidence ya kuleta mitaji hapa nchini aweze kuwekeza kwenye nchi hii ambapo hakuna uhuru wa mawazo, hatuwezi kuji-express? Nani ataleta mitaji katika nchi ili mambo yaende vizuri mahali ambapo Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, kila mtu anaenda njia yake? Mheshimiwa Rais anatoa maagizo haya, Mkurugenzi anatoa haya, Waziri anasema haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kuleta mabadiliko na tabia za kama Manaibu Waziri akina Mheshimiwa Waitara hapa, ambao kila saa anadhani tuko kwenye Mikutano ya Siasa. Changamoto tulizonazo zinahitaji big brain. Tanzania tuna matatizo makubwa kutoka hapa tulipo. Hatupo kwenye Mikutano ya Kisiasa hapa ndani. Uliondoka CHADEMA, is over. Do the job, mwonyeshe Mheshimiwa Rais kwamba you are capable. Show your talent! Show your ability. (Kicheko/ Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa mambo ya kusema nilikuwa CHADEMA, mipasho, haitusaidii. Mheshimiwa Rais amewapa hiyo kazi, hebu tuonyesheni uwezo wa kututoa hapa tulipo. Nchi hii haina mashimo ya vyoo sasa hivi, mnasema huko, vyanzo vyote kwenye hotuba yetu tumezungumza, vimehamishwa vyote vimekuja Serikali Kuu, lakini hela hiyo hairudi kwa wananchi.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Reverend Msigwa. (Makofi)
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Nimemaliza! (Makofi)