Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE.JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwapongeze Mawaziri, Naibu Mawaziri na watendaji wote kwa kazi nzuri wanayoifanya chini ya uongozi wa Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, Awamu hii ya Tano ya utawala wa Jemedari wetu Mkuu, Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, ameudhihirishia ulimwengu inaumahiri na uhodari, maarifa na umakini mkubwa wa kufanya mageuzi ya kiutendaji kwa watumishi wa umma na kupiga vita rushwa na ufisadi, uzembe kazini na uwajibishwaji wa viongozi wazembe. Kwa sababu hiyo na nyinginezo, nashauri kuwe na mfumo endelevu kwa awamu zote za utawala wa nchi utaozingatia uwajibikaji na uwajibishwaji watumishi wa umma ambao hawazingatii viwango vilivyopangwa ili kuleta tija kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii itasaidia baada ya awamu hii muda wake wautawalakuisha. Nidhamu na mifumo hii iendelee bila kutupwa kapuni kama yalivyotupwa au kuachwa mambo mazuri ya Awamu ya Kwanza. Mazuri mengi ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli, Rais wa Tanzania hayapaswa kuachwa hata kidogo. Kizazi hiki kitahukumu iwapo Awamu zinazofuata zitasahau mazuri haya. Mungu ibariki Tanzania naviongozi wote, amina.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia 100.