Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri yenye ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Wizara yake.

Mheshimiwa Spika, pili, naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja. Pamoja na kuunga mkono naomba kuchangia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nalipongeza sana Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) na wafanyakazi wote kwa kazi nzuri ya kurusha na kutangaza habari kwa Watanzania.

Pamoja na kazi nzuri wanayoifanya watangazaji, wanakabiliwa na changamoto zifuatazo:-

(1) Uchakavu wa mitambo ya TBC mingi ni ya miaka ya zamani. Naishauri Serikali inunue mitambo mipya na ya kisasa ili TBC 1 iweze kuonekana vizuri nchi nzima na TBC Taifa (Radio) isikike vizuri nchini kote.

(2) Maslahi duni ya wafanyakazi wa TBC husababisha wafanyakazi kuhamia vyombo vingine binafsi.

(3) Magari yamechakaa hasa kwa TBC Kanda ya Kati na ni machache na hivyo kuwafanya wasitembelee maeneo mengine ili kuchukua habari. Habari nyingi zinakuwa za mjini tu badala ya vijijini ambapo wapo wananchi wengi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Waandishi wa Habari ni wachache, habari zinazoandikwa nyingi ni za mijini tu siyo vijijini. Naishauri Serikali iajiri Waandishi wa Habari kila Wilaya.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kuna migogoro mingi ya vilabu vya mpira wa miguu: Je, nini chanzo cha migogoro hiyo? Pili, Serikali inasaidiaje kutatua migogoro hiyo ili kuboresha hali ya soka hapa Tanzania? Je, Serikali ina mpango gani wa kuisaidia Serengeti Boys ili wafanye vizuri katika mashindano yanayoendelea hivi sasa?

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja.