Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kuisoma nukuu hii inayosema; “Udikteta wa wengi wape. Udikteta wa wengi wape ni ile hali ambapo Serikali au mamlaka nyingine inayoungwa mkono kidemokrasia na wafuasi wake wengi walio katika vyombo vya maamuzi wanapoamua kutengeneza sera au kupitisha maamuzi yenye kufaidisha maslahi yao lakini bila kujali haki wala ustawi wa watu wengine wote walio chini ya utawala wao.”

MWENYEKITI: Niambie source yake.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, source yake ni kwenye dictionary.

MWENYEKITI: Niambie dictionary ipi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni Oxford Dictionary.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ni wawakilishi wa walipa kodi na kuna myth inataka kutengenezwa katika Bunge hili kwamba sisi wapinzani hatuwapendi polisi. duniani kote polisi wanasimamia law and order na tunahitaji Polisi hakuna mtu ambaye hawataki Polisi, hiyo ieleweke kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wanataka kupotosha hapa na kujipendekezapendekeza kana kwamba sisi hatuwataki polisi, hata sisi tukichukua nchi tutawataka polisi. Kuna mambo Jeshi la Polisi linafanya kazi vizuri na ndiyo maana kwenye Utawala Bora Mheshimiwa Mollel alisimama hapa kuwatetea wafanyakazi wa umma ambao ni pamoja na polisi wapate mishahara yao. Kwa hiyo, hiyo myth iondoke kwamba sisi hatuwataki Polisi, tunawataka polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja kubwa tunayojenga dhidi ya polisi ni pale ambapo hawafuati sheria. Kuna Police General Order (PGO) lakiniPolisi hawaifuati na sisi hapa ni wajibu wetu kama Wabunge kuhakikisha inafuatwa. Sisi tunasema wafuate sheria ninyi hamtaki, sasa mnataka waendesheje Jeshi, tunataka wafuate sheria kwa sababu hazifuatwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijasahau, Mheshimiwa Kangi, nina maswali kadha ambayo lazima uwaambie Watanzania na Mheshimiwa IGP ananisikia hapa. Mheshimiwa Rais hivi karibuni aliliambia Jeshi la Polisi kwamba Watanzania siyo wajinga, ile move ya MO, haieleweki. Tunataka uwaambie Watanzania exactly what happened? Kwa sababu polisi kazi yao ni kulinda raia na mali zao, full stop. Mimi kama Mtanzania Polisi ana wajibu wa kunilinda, exactly tunataka tujue movehiyo na Rais alisema, kama mnapinga maamuzi ya Rais sijui, alisema Watanzania siyo wajinga na IGP akasema baada ya siku tatu atatoa taarifa, sasa hivi muda umepita hiyo taarifa haijatoka, we want to know that. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, number two, polisi bado hawajatuambia, what exactly, ni kitu gani kilimtokea Roma Mkatoliki, bado tuko gizani hatuna majibu hayo, tutakuwa Wabunge wa hovyo sana kuliruhusu Jeshi la Polisi mambo ya hovyo yanatokea halafu eti tuseme polisi wang’atwa na mbu, hawalali si ndiyo kazi ya polisi, yaani mwanajeshi akienda vitani tuanze is not doing as a favor that is his job. Utuambie Roma Mkatoliki kilitokea kitu gani nchi haijui. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, polisi haijatambua kuvamiwa kwa Clouds, hamjatoa maelezo yoyote Clouds ilivamiwa kilitokea gani? Nani alihusika nani alikamatwa hatuwezi kukaa kimya halafu tukasifu tu Jeshi la Polisi hapa. Polisi haijasema kuhusu Azory na jana nimesikitika sana kumsikia Mheshimiwa Mwakyembe hapa anasema eti mtu mmoja tu tunaangaika naye. Uhai wa mtu mmoja ni wa thamani sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwenzangu ame-quote Biblia out of context lakini Biblia inasema tumeumbwa kwa image ya Mungu, mtu mmoja akipotea Taifa lazima linununike, watu wanaokufa siyo inzi ni binadamu. Polisi hamjasema kitu gani kimetokea kwa Ben Saanane mnabumba bumba mpaka leo. You must tell us nani alimuuwa Mawazo polisi mmekaa kimya, Jeshi la Polisi halijasema Mheshimiwa Kangi, polisi hamjasema mpaka leo dunia nzima mnasema (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. MCH. PETER S.MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Tundu Lissu anawabagaza Polisi hamjasema nani alimpiga risasi kwa Tundu Lissu…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpe taarifa huyu.

MHE. MCH. PETER S.MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna uchunguzi tutakaaje kimya tuseme Jeshi la Polisi tunalishangilia matukio makubwa kama haya, dunia inaona, Polisi hawatoi ripoti sasa kazi yao nini? Kazi ya Polisi ni kulinda raia na mali zao ndiyo kazi ya Polisi. Polisi anawajibu wa kulinda raia na atoe ripoti kwa nini raia wameuwawa tuende wapi, wao ndiyo wana mabomu, wao ndiyo wana vitendea kazi, tumewakabidhi watulinde na wapo kwa ajili ya hiyo. Nani alimnyooshea bunduki Mheshimiwa Nape we are quite, polisi hawajatoa ripoti nani alionesha bunduki pale amechukuliwa hatua gani? Sasa tukae hapa tuseme hoo wanang’atwa na mbu sasa wana kazi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia duniani wenzetu Marekani ambapo demokrasia imeshamiri George Washington alivyokuwa anaunda Serikali walitaka kumfanya awe mfalme akasema lazima tuwe na Serikali ambayo itakuwa na nidhamu kwa wananchi. Leo vyombo vya dola tunaonekana kama sisi ni watumwa swali la kujiuliza; are we captive or we are citizen in this county? Kwa sababu maonezi yanayofanywa kwenye Vituo vya Polisi ni makubwa sana sisemi Jeshi la Polisi lote. Kama mimi Mbunge nimesingiziwa kesi ya kuchoma nyumba, nimesingiziwa kesi ya kubomoa nyumba hawa raia wa kawaida na siyo Mbunge fala, lakini nimesingiziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kesi zimeenda Mahakamani within a minute zimefutwa kwa sababu ni uovu, RCO wa Iringa amehamishiwa sasa hivi Pemba anatengeneza kesi za uongo kabisa nimelala mahabusu kwa kuonewa na wengine wenu hapa hamna legitimacy ya kuongelea mambo ya custody wala huko kwenye cell, you have never been there! Hamjui ukienda central pale how it looks like? We have been there. Hamjaenda Segerea mnasema tu hapa hamjaona watu wanavyoteswa kule ndani, hamna hiyo legit. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongea haya mambo kwa sababu tuna experience, anasimama leo, leo Kikatiba mtuambie kama Katiba haifuatwi hii, nchi ni ya utawala wa sheria, Katiba inatupa haki ya kuandamana, anasimama RPC, mtumishi wetu, mtumishi wa umma sisi siyo captive, we are not captive we are citizen anasimama and we pay them na wamekuja hapa kuomba hela ili tuwalipe…

MWENYEKITI: Ongea na Kiti.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, yes sir, anasimama kwenye vyombo vya habari anasema nitawatandika nitawachakaza who he think he is? Nataka niwaambie Polisi kuna watu ambao walifanya makosa katika Vita vya Pili vya Dunia… (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa ongea na Kiti, huwezi kuwaambia Polisi ni-address mimi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu ambao walifanya makosa katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia leo wanalipa gharama you never go away pale ambapo mlipaswa msimamie sheria mkafunika mkadhani sheria haitawafuata; somewhere in the future tutakuja tutakukamata kwa sababu sheria inakutaka ufuate sheria, watu wanaoza kwenye vituo, wanakamatwa raia, sheria inasema wakae masaa 48 wanakaa miezi miwili, wanakaa miezi mitatu, tumekuwa na torturing chamber katika nchi hii watu wanapigwa, kuna yule mzungu amevunjika miguu, anateswa na mabinti wengine wa kike wanamwambia aoneshe uchi wake wanamtesa, “how can we live in this county. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tuseme tusikemee haya mambo haya tutasemea wapi? Raia wanakufa kwenye mikono ya Polisi kila wakati halafu tusiseme halafu tuseme wapi. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)