Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia hoja hii katika suala la uvunjwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa katika utundikaji au upeperushaji wa bendera za vyama kwenye Ofisi na mabango mbalimbali. Hivi karibuni katika Mkoa wa Iringa umetokea mtindo anakuja kiongozi wa nchi bendera za CHADEMA zinaondolewa zote na kutundikwa bendera za CCM. Hii haikubaliki tuko katika mfumo wa vyama vingi ni vyema Jeshi la Polisi likalinda mali za jamii na watu wake. Bendera ziliondolewa Mafinga na Iringa Mjini.

Mheshimiwa Spika, askari wanahitaji kuongezewa mishahara na pia kupata posho za mazingira magumu ya kazi yao. Mara nyingi wanakosa karatasi, printer na mafuta ya kuendesha programu mbalimbali. Nashauri waongezewe fungu ili wafanye kazi kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza wamekuwa hawana mavazi/sare kwa kugharamiwa na Serikali, wananunua kwa fedha zao wenyewe kinyume na taratibu. Serikali ifanyie kazi suala hili ili wapewe sare za kazi.

Mheshimiwa Spika, suala la maadamano na mikutano ya hadahara limekuwa ni changamoto kufanyika hasa kwa vyama vya upinzani. Nashauri Jeshi la Polisi lifuate sheria na Katiba inayotaka kuwapo kwa maandamo pamoja na mikutano ya hadhara na mikutano/vikao vya ndani. Jukumu la Jeshi la Polisi ni kulinda amani katika mikutano/vikao na maandamano.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na mlundikano wa mahabusu. Nashuri kuanzishwe Kitengo Maalum cha Usuluhishi Polisi ambacho kitasuluhisha migongano ya waliofika kituoni ili kuwajengea umoja wananchi na kuwaweka karibu na Polisi kama sehemu ya kimbilio.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.