Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Kwanza nakupongeza sana kwa hotuba nzuri yenye ufafanuzi mzuri wa sekta mbalimbali za Wizara yako. Pili, naunga mkono hoja hii kwa asilimia 100. Pamoja na kuunga mkono hoja, naomba kuchangia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa walimu; Wilaya ya Mpwapwa ina upungufu mkubwa sana wa walimu hasa shule za sekondari za kutwa na hii inachangia kiasi kikubwa elimu kushuka katika Wilaya yetu ya Mpwapwa. Naishauri Serikali kupeleka Walimu wa kutosha katika Wilaya ya Mpwapwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukarabati wa shule ya sekondari ya Mpwapwa na Chuo cha Ualimu Mpwapwa; kwanza naishakuru sana Serikali kwa ukarabati uliofanyika katika Taasisi hizo mbili (Mpwapwa High school na Mpwapwa TCC). Pamoja na ukarabati huo, nyumba za walimu ziliachwa na zina hali mbaya sana na zingine hazijafanyiwa ukarabati muda mrefu mpaka zimeweka nyufa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuzifanyia ukarabati nyumba za walimu, Chuo cha Walimu Mpwapwa na Mpwapwa High school ambayo ni shule kongwe hapa nchini ilianza mwaka 1926.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usafiri katika shule ya sekondari Mpwapwa na Chuo cha Ualimu Mpwapwa; kwa usafiri ni muhimu sana katika Taasisi, Mpwapwa High school yenye wanafunzi zaidi ya 600 hakuna Gari kwa ajili ya huduma kwa wanafunzi na walimu. Pia Chuo cha Walimu Mpwapwa chenye wanachuo zaidi ya 1000 hakina Gari kubwa kwa ajili ya huduma ya Wanachuo. Je, kuna mpango gani wa kupeleka Magari katika Taasisi hizi mbili, Mpwapwa High school na Mpwapwa TTC? Pia Serikali ina mpango gani wa kukibadilisha Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Chisalu cha Mpwapwa kuwa chuo cha ufundi (VETA) kwa Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa, hakuna Chuo cha VETA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.