Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, sina budi kwanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na taasisi yote ya Wizara yake kwa bajeti nzuri waliyotuletea ambayo inaeleweka na pia Mheshimiwa Waziri jinsi alivyo-present hapa pia unataka kumsikiliza vilevile sina budi kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchagua majembe akayaweka Wizara ya afya yanatufanyia kazi nzuri na tunaridhika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitakuja kwenye ile kinga ya kansa ya kizazi. nakumbuka mwaka jana kulikuwa na kampeni ya watoto wetu wa miaka tisa mpaka miaka kumi na nne ambao hawa wafanyiwe chanjo ile ya kinga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna baadhi mikoa nasikia kuna vijana hawakwenda wazazi wao wamewazuia sijui kama taarifa hiyo mnayo. Na kama mnayo kwanini waliwazuia wakati Serikali ilishagharimika ilishatafuta pesa na hii ni kinga kwa wao wenyewe itakayo wasaidia huko mbele watakapo endelea na maisha yao lakini wakawa hawakuwapeleka ingawa mlitumia shule mkaenda mkafanya hiyo lakini bahati mbaya baadhi ya wazazi waliwazua watoto wao. Sasa tunataka kujua kwa nini ilitokea Hivyo na kama ni kweli nyinyi mnajua na mmechukua hatua gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja nyingine kwenye fistula kwa kina mama suala hili hata mwaka jana lilizungumzwa. Kwa sababu CCBRT wao ndio wanashughulika na suala fistula lakini utakuta kuna watu wapo mikoa tofauti na fistula wanapata. Fistula hachagui ni bahati mbaya tu unaweza ukapata, sasa kwanini hamsomeshi watu wenye fani hii mkawasambaza katika hospitali za mkoa, hospitali za kanda ili wakaweza kuwa mabingwa wa ainai ile mtu likimtokea jambo hili asiweze kuhangaika anajua mimi hiki kimenitokea na madaktari hapa wapo wenyewe wataona na wanaweza wakamtibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Waziri nataka hili mliangalie kama madaktari wa fani hiyo hawana msomeshe ili muweze kupata madaktari waweze kuwatibu wananchi bila matatizo maana kuwa na fistula wakati haja inatoka bila kawaida ni tatizo kwa binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja suala la watoto njiti, mama anapobeba mimba sijui kwa uzoefu anajua kuwa mimi nitazaa njiti au nitazaa mtoto aliyekamika. Sasa ninataka nijue wakati wanapokwenda kliniki mnatoa elimu au na wale madaktari wanakuwa hawajui kama atazaa mtoto njiti? Kwa sababu unapomzaa na baadhi ya hospitali haina vifaa utaambiwa umuweke kufuani, umuwekee tumboni apate joto hilo tatizo. Unajua kama mama wakati mwingine ana joto la kutosha? Mama wengine wapo baridi tu. Sasa kama mkiwa hamjaangalia mkawa mnatoa elimu toka watu wapo kliniki kwamba mtoto njiti yuko hivi mzazi unatakiwa kuwa hivi au unahisi kabla hujazaa uko hivi ili mama anakwenda kuzaa tayari anakuwa na elimu ya kutosha anakuwa hana wasiwasi na hata atakapo mzaa yule mtoto anajua huyu mtoto anajua huyu mtoto nimemzaa wa aina fulani na nitakiwa nimuhudumie vipi ili makuzi yake yawee vipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye suala lingine la sober house. Unajua kila siku tunahangaika na vijana wetu wanaokula unga, na hili ni tatizo sugu. Nashukuru Wizara ya Mambo ya Ndani wanavyohangaika nalo, lakini je Wizara ya Afya wamechukua hatua gani? Kwa sababu wanatakiwa lazima kuwa na dawa za kutosha zakuweza kuwatibu hawa vijana wetu. Mambo ya Ndani kazi yake yeye ni kutafuta na kupembua na kukamata lakini wa kutibu ni Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilikuwa naomba Wizara ya Afya mshirikiane na Mambo ya Ndani ili muweze hili jambo kulimaliza, mlimalize kabisa. Kwa sababu watoto wetu wanaumia na wao ndio nguvu kazi bila ya wao wakiwa hawataweza kufanya kazi taifa letu litadolola. Sasa nakuombeni Wizara ya Afya wakati Mambo ya Ndani tayari wanalishughulikia mshirikiane nao kwa kuwaweza kuwatibu wale vijana wetu ambao tayari wameathirika. (Makofi)

Mheshimiwa Mweyekiti, lingine bima ya afya bila ya afya kwa upande wa Zanzibar naomba iboreshwe. Kwa sababu unapokuwa na bima ya afya Zanzibar inabidi uende Vialeni, Globaly, Arhma au Hospitali zilizokuwa chini ya vyombo vya ulinzi kama jeshini au polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwetu kwa upande wa pili ni tatizo kwa sababu tunazo Cortege hospitali kama moja ipo Makunduchi, nyingine ipo Mkwajuni sasa wa Kaskazini watakwenda zoa kule. Wapo watu wanafanya kazi za muungano kuna Wabunge wana familia zoa wanazo bima za afya na wengine kuna polisi kuna wanajeshi wataweza kutumia. Na wa Kusini watakuwa wanakwenda Makunduchi. Lakini sote tunakimbilia mijini huko mjini napo kuna matatizo yake kwa sababu utaambiwa dawa hakuna, hiki hakuna, Na itabidi matatizo. Sasa namuomba Mheshimiwa Waziri najua bima ya afya ipo kwenu mtuboreshee na Zanzibar iweze kuwa na uwezo wa kufanya kazi na uwezo wa kutibu na kila mmoja alidhike na fedha yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu kama Mbunge nakwenda hospitali naambiwa dawa hakuna nikiitizama bima yangu natakiwa kila kitu niifanyiwe. Lakini hakuna kwa sababu hamjaboresha kule. Wanakwambia hakuna, sasa Naomba muwe mnalingalia suala hili kwa jicho la rehema ili liweze kufanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja suala la mwisho, Usambazaji wa dawa za baridi na moto katika Pharmacy zetu. Najua kuna kanuni zinazongumza dawa aina gani ziende zikauzwe mitaani. Lakini naona hizo kanuni hazifuatwi naweza jirani yangu kaenda hospitali katibiwa nami maradhi yale nikaja nikayapata akaniambia nenda dawa fulani mimi nilipewa wakati mie cheti sina nitakwenda pharmacy na pharmacy atanipa ile dawa na siku nyingine dawa ya moto lakini anayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama mtafanya ziara ya kushtukiza mkawa mna kwenda mara kwa mara mnaangalia kwa sababu hii mnasaidia tiba ya raia wenu ambao ndio raia wa Tanzania watakao weza kufanya majukumu yao na kuwaondoshea matatizo katika miili yao na afya zao. Nafikiri hayo naunga mkono hoja mia kwa mia nawapongeza kwa kazi yao nzuri nashukuru. (Makofi)