Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Iringa Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kumwomba Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi Mheshimiwa Mengi ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika Taifa letu. Pia niwashukuru Madaktari wote nchini, Manesi na Wauguzi wote nchini, kwa kweli wamekuwa wakifanya kazi kubwa, kazi ngumu, kazi ya wito, kazi ya kujitolea. Niwashukuru wote kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la iringa Mjini kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, niseme mawili matatu yanayohusu jimbo langu na mengine nitaangalia yanayohusiana na Taifa. Amezungumza Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum hapa kuhusiana na Hospitali yetu ya FRELIMO ya Manispaa ya Iringa, asubuhi nimeuliza swali hapa, nashukuru Waziri amejibu lakini niombe wizara wasaidiane na TAMISEMI, wilaya zingine zote zilipewa fedha zile karibu bilioni moja kusaidia vifaa, hospitali yetu ile ni ya muhimu, ikiwezeshwa itasababisha hospitali ya rufaa ipunguziwe mzigo. Niombe sana tusaidiane kuhakikisha haya mambo yanafanyika kama Waziri alivyosema wa TAMISEMI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa Mheshimiwa Ritta hajasema sana, hospitali ya mkoa kwa sasa hivi hakuna bingwa wa mifupa, Daktari wa Mifupa wala Bingwa wa surgery. Hii yote aliyoisababisha ni Mkuu wa Mkoa katika ziara yake aliyosema Iringa mpya. Katika Iringa yake mpya imekuwa ni ya kubomoa. Sasa hivi pale Hospitali ya Rufaa kuna matatizo makubwa sana, wagonjwa wanategemea Walimu wanaokuja kuwafundisha wanafunzi wa UDOM kuja kufanya upasuaji, kwa hiyo imekuwa ni ngumu sana. Niombe sana Wizara na Serikali kwa ujumla, hebu tuangalie viongozi wasiwe wana-demoralize wafanyakazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hao Madaktari wanasomeshwa na nchi kwa gharama kubwa sana na wanafanya kazi kubwa sana, kama kuna matatizo ya management, ya kiutendaji, zifuatwe procedures za namna ya ku-deal nalo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakumbuka Mkuu wa Mkoa alimdhalilisha Daktari Nyakioto, ni bingwa, amefanya kazi kubwa sana, pia kuna Daktari Rehema naye ameondoka lakini hawa watu wote wamekimbia Iringa ni kwa sababu ya utendaji wa hovyo wa wanasiasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Wizara iji-commit kwa sababu Wakuu wa Wilaya wala Wakuu wa Mikoa siyo ngazi za kutoa adabu kwa watendaji. Naomba mnapotoa majibu hapa mtangazie Tanzania kwamba wao wala viongozi wa chama kama kule Arumeru, kiongozi wa kata tu anampa maagizo daktari eti dakika 15 umefika. Naomba Serikali itangaze kwamba wao siyo ngazi za kuwawajibisha, madaktari hawa wanafanya kazi kubwa sana. Niombe hilo mlifanyie kazi ili madaktari na manesi wetu wafanye kazi vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, madaktari na wauguzi wetu wanahitaji kutiwa moyo, ni watu ambao wanashika vinyesi, mikojo na mautumbo yetu, lazima tuongee hizo ni kazi za kujitolea. Viongozi wa kiserikali na wenye vyeo tunatakiwa tuwape moyo, tusiwa-demoralize, tuwape moyo wafanye kazi vizuri kama ambavyo tuna mategemeo mazuri kutoka kwao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba yetu ya Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Esther ameorodhesha viongozi wengi wa kisiasa na amewataja. Namba hili suala mlitolee maamuzi ya msingi kabisa ili utendaji kazi uende sawasawa kama sheria na taratibu zinavyotaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine ni hili ambalo na Mheshimiwa Sakaya amelizungumza ni la wazee kwenye masuala ya pensheni, mliahidi kabisa kwamba mtawaongeza kutoka Sh.50,000 kwenda Sh.100,000, wale waliokuwa PPF wameongezwa wengine wamekuwa wakidai hawajapata. Ni lini sasa fedha zao ambazo wanatakiwa waongezewe watapewa? Hawa ni wazee ambao wamefanya kazi kubwa katika Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna wataalam wengine wanasema we are just dwarf standing on the shoulder of the giants. Sisi ni matokeo ya hao wazee waliotangulia. Tutakuwa ni taifa la namna gani tusipowaenzi wazee. Tukumbuke na sisi tuta-phase out, tutazeeka. Hiyo nafasi uliyonayo hapo Mheshimiwa Waziri na Naibu wako kuna wengine walikuwepo wameondoka. Hata mimi nafasi yangu ya Ubunge niliyonayo hapa kuna wengine walikuwepo wameondoka. Tunapofika mahali kama taifa wazee hatuwaheshimu, hatuwatunzi kwa kweli hatuwatendei haki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri katika maeneo haya ya kutunza wazee, hebu tusilaaniwe na Mwenyezi Mungu tunapokuwa tumewasahau wazee. Tupange bajeti za kutosha kuwasaidia hawa wazee. Wazee wengi ukiwakuta katika maeneo mbalimbali wanalalamika.
MBUNGE FULANI: Akina Mzee Lubeleje.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Wanalalamika hawapati huduma zinazotakiwa. Ndiyo maana wakati mwingine tunalazimika kurudi Bungeni humu kwa sababu hali ni ngumu huko mitaani.
MBUNGE FULANI: Usituseme bwana.
MBUNGE FULANI: Akina Mzee Lubeleje.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya bajeti ya Wizara hii imeendelea kushuka, sasa hawa wazee tunawasaidiaje? Wizara hii ni nyeti, amezungumza Mheshimiwa Lwakatare hapa, kweli kuna vifo vingi ambavyo kimsingi siyo Bwana ametwaa, ni kwa sababu hazijapatikana huduma za msingi ambazo zingeweza kuokoa maisha ya watu wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto wengi wanakufa kwa sababu hawajapata huduma zinazostahili. Akina mama wajawazito wengi wanakufa kwa sababu hawakupata huduma zinazostahili. Watu waliopata ajali wengi wamekufa si kwa sababu walitakiwa kufa, ni kwa sababu hawakupata huduma zinazostahili. Tumekuwa hatuna vifaa vya kutosha, hatuna madaktari wa kutosha lakini hata hao madaktari wachache walioko bado tuna wa-frustrate. Naomba sana katika eneo hili Mheshimiwa Ummy na kweli wengine wamesema mara nyingi ukipigiwa simu umekuwa una-respond pamoja na Naibu wako…
MBUNGE FULANI: Wanachapa kazi.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Una-respond na unajibu kwa wakati, ningeomba hii ishuke mpaka huku chini na madaktari hao walindwe. Wana chama chao, wana namna yako ya kuwalinda, walindwe hawa madaktari kama wana makosa mimi siwatetei lakini hatuwezi kuwaadhibu madaktari wetu kwenye mikutano ya hadhara, hatuwezi kuwaumbua madaktari wetu kwenye vikao vya kisiasa. Wahukumiwe, waadhibiwe kwenye proper channel, inaumiza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkutano mmoja wa siasa umeathiri hospitali yangu hakuna madaktari bingwa, ina maumivu makubwa sana. Nikuombe Mheshimiwa Ummy Mwalimu, hili linaniumiza sana kwa sababu hapa napata meseji Iringa kama unavyoiona, tumeitengeneza Southern Circuit ili tukuze utalii, tunahitaji tuwe na hospitali za kutosha. Iringa ni mahali pazuri, pana hewa nzuri, tuna mazingira mazuri lakini inapofika mahali tunakosa madaktari tunaongeza matatizo yasiyokuwa ya lazima katika Manispaa yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambvyo Waziri amekuwa aki-respond nimwombe katika suala hili alisaidie taifa zima kwamba tuheshimu madaktari wetu ili wafanye kazi kwa weledi. Anafika Mkuu wa Mkoa anasema, eti sasa hivi daktari ni marufuku kumwekea drip mgonjwa kabla hujampima. Sasa Mkuu wa Mkoa amesomea wapi kazi hiyo?
MBUNGE FULANI: Na mgonjwa kama anaharisha?
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Ndiyo, kama mgonjwa anaharisha daktari si ndiyo anajua kazi yake? Leo Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya anajua utaratibu huo, pamoja na kwamba mnasema Chama cha Mapinduzi, ina maana chama ndiyo kinatuma watu wawaambie hivyo madaktari? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni mambo ambayo kama Bunge lazima tukemee, madaktari wetu walindwe, waheshimiwe, wasikoselewe kwenye mikutano ya hadhara. Hii Mkuu wa Mkoa wa Iringa anisikie, imeleta shida safari hii, ziara yake ya Iringa mpya imekuwa matatizo katika Mkoa wa Iringa, hatukuwa na mazoea haya. Najua Mheshimiwa Kabati ameogopa kusema kwa sababu ya mambo ya ki- protocal lakini Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ametuletea tatizo katika Mkoa wetu wa Iringa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)