Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia kidogo katika Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijatoa mchango wangu kwa ujumla naomba tu nizungumze kidogo kuhusu sheria iliyounda mawakala ikiwepo TANROADS maana nitazamia kwenye TANROADS. Kifungu namba 12(2)(a) cha Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 kinataka wakala wote wafanye kazi kibiashara na mapato yao yatoshe kulipia matumizi yao. Hii sheria imetekelezwa kwa kiwango kidogo sana. Kwa mwaka 2015/2016, mapato ya ndani ya mawakala wengi yalishuka kutoka asilimia 45 hadi kufikia asilimia 16 mwaka 2020. Ni mawakala wachache tu walioweza kujitegemea, lakini mawakala wengi ikiwemo TANROADS wametegemea Serikali kwa kiwango cha asilimia 84.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nataka Waziri atakapokuja kuhitimisha atueleze tatizo ni nini ambalo linafanya Wakala wa Barabara TANROADS wasiweze kujitegemea angalau kwa kiwango kikubwa. Kama tatizo ni sharia, basi sheria iangaliwe upya, lakini kama si sheria tuambiwe tatizo ni nini. Pia TANROADS kwa mwaka uliopita unaoishia Juni walikuwa na deni la bilioni 833 na kati ya hizo bilioni 57 ni riba ambayo inatokana kutowalipa wakandarasi kwa wakati. Tatizo hili siyo la TANROADS, ni Wizara ya Fedha ambayo imeshindwa kuwapelekea hela kwa wakati, matokeo yake TANROADS wanadaiwa na wakandarasi kiasi kwamba ukiangalia riba ya bilioni 57 ni kubwa sana kiasi ambacho ingeweza kutengeneza barabara nyingi. Kwa hiyo, niseme kwamba sisi tuiambie Serikali inakwamisha sana wakala hawa kufanya kazi, maana nia ya kuanzisha hawa Wakala ni ili kazi zetu ziende kwa tija, lakini unapowakwamisha inapelekea kuonesha kwamba mawakala hawa hawafanyi kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba niingie kwenye hoja yangu ambayo naongea kwa niaba ya Wabunge watano kuhusu barabara ya Same - Kisiwani – Mkomazi. Barabara hii ambayo inatumiwa na Mbunge wa Same Magharibi, Mheshimiwa Mathayo ambayo pia inatumiwa na Mbunge wa Mkinga, Mheshimiwa Kitandula; Mheshimiwa Mnzava wa Korogwe Vijijini; Mheshimiwa Shangazi wa Mlalo na mimi mwenyewe. Ni barabara ambayo ina tija sana kwa Taifa kama ingetengenezwa kwa kiwango cha lami. Ni muda mrefu sana barabara hii tumeipigia kelele, tangu nilipoingia mara ya kwanza. Imeshafanyiwa upembuzi yakinifu mara tatu na mpaka mara ya mwisho nimeongea na Engineer Mfugale ambaye anaheshimika Kitaifa na Kimataifa, akaniambia alikuwa katika hatua ya mwisho ya kufanya design.

Mheshimiwa Naibu Spika, cha ajabu barabara hii imetengewa milioni 300 kwa kilomita moja. Sasa hebu angalia barabara ambayo inatumiwa na Wabunge watano, wanaume wanne na mwanamke mmoja; wa CCM wane na wa CHADEMA mmoja; Viongozi wa Kamati za Kudumu wawili, bado Waziri haoni umuhimu kwamba hii barabara inategemewa na wapiga kura wengi wanaotokana na majimbo haya matano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nasema barabara yoyote ukiitengeneza, unaangalia kwamba ina manufaa gani kwanza kiuchumi because lazima kuwe na return to capital, return kwenye investment, hatutengenezi barabara tu kumfurahisha mtu, nimeshaona barabara nyingine inatengenezwa kutoka kata kwenda kata ikawekwa lami na ukiangalia ina-produce nini pale, inabeba watu wangapi. Nasema na ndiyo maana nimesema niangalie hii sheria ya kuunda mawakala ili tujue, je, tunafanya kazi kibiashara au tunafanya kazi kihasara? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe, Tanzania tutokane na kufanya kazi kana kwamba sisi hatujali uchumi wetu, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, anajali sana kwamba nchi hii ipige hatua, tuingie nchi ya viwanda, ya uchumi wa kati, lakini kwa mtindo huu unampa kabarabara kamoja kadogo yaani kilomita moja unaangalia tija yake ni nini.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kusema TANROADS wamejitahidi, lakini kuna barabara zimetengenezwa kwa kiwango cha kutisha kibaya mno, Kamati yangu ilitembelea barabara kutoka Dodoma kwenda Iringa, ilikabidhiwa miaka minne iliyopita, inatisha na nafikiri niliona kama imetengewa tena hela. Sasa kama barabara zetu kwa muda mfupi inaharibika inarudi kuanzia kutengeneza tena na hii iko katika Great North Road, lakini imetengenezwa kwa kiwango cha chini kiasi kwamba tunaonekana kwamba laissez-faire. Hivyo, nimwombe Mheshimiwa Waziri tuangalie utengenezaji wa barabara zetu, ametoka kwenye Maji, ameletwa kwenye eneo lake la kujidai tunaomba aangalie sana wakandarasi alionao.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama barabara zetu kwa muda mfupi zinaharibika inaanza kutengenezwa tena na hii iko katika Great North Road lakini imetengenezwa kiwango cha chini kiasi kwamba tunaonekana Watanzania ni laissez-faire. Naomba Mheshimiwa Waziri tuangalie utengenezaji wa barabara zetu. Mheshimiwa Waziri umetoka kwenye Wizara ya Maji umeletwa kwenye eneo lako la kujidai, tunaomba uangalie sana wakandarasi ulionao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimeona kule kwenye barabara hii ninayozungumzia ya Same - Kisiwani - Mkomazi mara nyingi inatengewa fedha ambayo mnaziita Upgrading DSD, labda mtanieleza maana yake, inatengewa hela lakini kila nikipita sijaona mahali ambapo pamefanyiwa upgrading hapo hapo hiyo DSD inatengewa hela. Kwa mfano, hiyo upgrading DSD shilingi milioni 175 na mwaka huu imetengewa shilingi milioni 200 lakini nikipita sioni mahali palipotengenezwa. Labda baada ye utanielimisha maana ya haya maneno ni nini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kibaya zaidi unpaved roads zinatengewa hela nyingi sana, shilingi milioni 848, mwaka jana shilingi milioni mia nane sijui ishirini na ngapi, mwaka juzi shilingi milioni mia nane na kitu. Sasa najiuliza, hivi kwa nini upeleke hela nyingi kwenye kuparura barabara wakati hela hizo hizo ungeweza kusema uziongezee utengeneze barabara ya kiwango cha lami? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli kuna mambo mengi ya kutafakari, muda wetu wa kuongea ni mdogo lakini nafikiri ifike mahali tufanye analysis kwamba hivi hizi barabara tunajenga kisiasa au tunajenga kiuchumi ili uchumi wetu upande? Tukijenga kiuchumi tutapata pesa kutokana na kusafirisha mazao ya kilimo na kusaidia sekta nyingine kama za afya na maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ambayo nairudiarudia imechezewa kwa muda mrefu sana. Najua haitengenezwi kwa kiwango cha lami, maana ni rahisi ku- trace lami inatengenezwaje lakini mkandarasi anapopita anaiparura tu barabara hii kwa miaka yote na kila mwaka shilingi milioni mia nane arobaini na kitu, kwa kweli nafikiri kuna aina ya ufisadi ndani yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Waziri atakapojumuisha anieleze kwa nini barabara hii moja inawekewa pesa nyingi kwenye unpaved road? I do not know utaita unpaved nini lakini kwenye laki unaweka kilomita 1, kwenye ku-upgrade unaweka nusu kilomita lakini kwa shilingi milioni 200, maana yake ni nini? Mimi napenda nijue haya yote na hii pia ingetusaidia kuangalia kwa nini barabara hii ya Same, Same ina-control 39% ya Mkoa wetu wa Kilimanjaro lakini ndiyo wilaya maskini kuliko wilaya zote za mkoa ule. Kwa hiyo, naomba barabara hii iangaliwe kwani Same ingesaidiwa ina sehemu kubwa ya ku-expand social economically hasa kwa upande wa kilimo lakini Same hiihii ndiyo imewekwa pembezoni …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa, kengele ya pili imeshagonga.

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.