Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Haji Khatib Kai

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Micheweni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kunipa akili na busara ili kuweza kutoa mchango wangu wa maandishi katika hoja hii muhimu kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imeamua na kupitisha usajili wa line za simu kwa njia ya kidole (finger) kuanzia 1/5/2019 jambo ambalo ni jema, Zanzibar na Wazanzibari kutoka ilipoanza kusajili simu za mkononi, Wazanzibar tulikuwa tukisajili line za simu kwa kupitia kitambulisho cha ZEN ID na hakukuwa na shida wala matatizo yoyote. Ni hivi karibuni tu mwezi Septemba, 2018 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitumia mabilioni kubadilisha na kuboresha kitambulisho cha ZEN ID.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya sana tunaona wakati zoezi hili likiendelea Wazanzibari ambao tulisajili line zetu kwa kitambulisho cha ZEN ID sasa kitambulisho hicho kinakataliwa na kimeondolewa kabisa, kama nilivyosema sisi Wazanzibari tulisajili kutumia ZEN ID bila shida yoyote na vile vile SMZ kutumia mabilioni kuboresha kitambulisho hicho ni kwa nini sisi Wazanzibari ambao tulitumia kitambulisho cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tusiachiwe kuendelea na usajili wa kitambulisho hicho?

Mheshimiwa Spika, vile vile kuondolewa kwenye usajili kitambulisho cha ZEN ID si wazi kwamba kitambulisho hiki Serikali ya Muungano inaenda kukiondoa kabisa. Hivyo hivyo wapo Wazanzibari ambao hawana kitambulisho cha NIDA lakini wana kitambulisho cha ZEN ID.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nimwombe Mheshimiwa Waziri atueleze kwa kutumia kusajili line za simu kwa Wazanzibari kwa kutumia ZEN ID tatizo ni nini? Suala hili ni muhimu wakati Mheshimiwa Waziri anafanya majumuisho ni vyema akalitolea ufafanuzi kwani Zanzibar hasa wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakijiuliza na kutoafautiana sana. Ahsante sana.