Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019

Hon. Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii nichangie kwenye hoja hizi mbili, lakini sana sana nitajikita kwenye hoja ya Kamati ya Miundombinu, Wizara ya Miundombinu kwa kuwa ni Mjumbe vilevile wa hiyo Kamati. Kwa hiyo tunafanya pamoja na Wizara pamoja na mashirika yake yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuzungumzia suala la TAZARA Serikali inaendelea kuwalipa watumishi mishahara, bado mazungumzo yanaendelea kufanyika kati ya nchi mbili na tuliishauri Serikali kwamba kuna haja sasa ya kukaa na kuzungumza na wenzetu wa Zambia ili tuona namna gani tunagawana tutenganishe hivi vitu Tanzania tushughulikie upande wa Tanzania na Zambia upande wa Zambia; kwa sababu kutokufanya hivyo tunaona kuna mdororo mkubwa wa TAZARA na TAZARA ni mwokozi kwa kuokoa barabara zetu na kupata mizigo mingi inayotoka katika nchi mbalimbali kwenda na kuja. Kwa hiyo nashukuru kwamba mambo haya Tanzania yameisha sasa tunawangoja ndugu zetu wa Zambia nao wafanye halafu baade mambo haya haya yatakuja kuingia kwenye Mabunge yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Serikali kulipa watumishi mpaka leo wa TAZARA mishahara, kuna tatizo kubwa la wastaafu wa TAZARA. Kuna wale wastaafu walioenda Mahakamani na wameshinda kesi kama 270 Hazina inaendelea kuwalipa kidogo kidogo ingawaje siyo utarabu, lakini sasa sijui inategemea nani anafuatilia zaidi kwa sababu wameshashinda kesi wameambiwa walipwe lakini inaenda kidogo kidogo sana kiasi kwamba wengine wanakata tamaa na wanakufa hawajapata hiyo hela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naiomba Serikali naishauri Serikali hebu iwalipe hawa wastaafu walioitumikia hiyo reli kwa moyo mmoja acheni kulipa kidogo kidogo, ukiachilia hawa 270 bahati nzuri kuna taarifa kwenye Kamati tuliiomba ya Hazina, na kweli wameileta inawatumishi wengine wastaafu 1,172, hao bado wanataabika wako mtaani bado kuna kizungumkuti mkubwa hawa wanaolipwa walioshinda Mahakamani inaonekana wale waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 badala ya 60 wameshinda kesi na wanalipwa hiyo hela, lakini wale 1172 TAZARA hiyo hiyo kwa sababu hawajaenda Mahakamani wameambiwa hawana stahili ya kulipwa hilo hela na walistaafu miaka 55 wakati Sheria ilikuwa inasema kwa lazima miaka 60. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hiyo ni shida kubwa hivi kwanini hawa watu wanateseka nchi hii, kuna mlolongo mkubwa nilivyopitia ile taarifa ya Hazina kwa kweli inaenda mbele na kurudi nyuma, hebu waurumieni hawa waliofanya kazi Mainjinia, nani wataalam mbalimbali watu wa kawaida, 1,172 siyo watu wachache hao, labda deni lao limekuwa kubwa sana wanawaambia hawa hawana haki wakitaka waende Mahakamani yaani kuna taarifa kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, basi Serikali iitishe mkutano wa pamoja na hawa wananchi hao wastaafu basi wawaambie maana wanateseka wengine kutoka Mlimba wanaitwa Dar es Salam njooni msikie majibu wanaangaika wanakopa wanazani watapata yaani hali ni mbaya kwa wastaafu hawa 1,172. Hebu Serikali oneni uchungu hawa watu wanazidi kuhangaika wazidi kubwa wanazidi kuumia muwape jibu la moja kwa moja siyo la kwenye makaratasi tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongezee masuala ya NIDA, NIDA tuliwaita juzi kwenye Kamati yetu NIDA ingawaje utashangaa mama Kiwanga kwanini anaongelea NIDA, na TCRA ni kama uji na mgonjwa TCRA sisi tunasimamia kama Kamati ya Miundombinu tumewaita NIDA wanachikisema ni tofauti kabisa kwenye ground mimi ni Mbunge wa Mlimba NIDA mpaka tarehe ya Rais aliyotangaza tarehe 20 NIDA wako pale Ifakara tu Mlimba wamegusa Kata 5 tu Kata nyingine zote hawajakanyaga NIDA, nimemuuliza mtaalam wa NIDA pale Kilombero anasema tumepeleka bajeti Makau Makuu lakini hiyo bajeti haijaja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo NIDA wanamatatizo makubwa ya pesa wanawafungia watu simu zao wakati hawapeleki bajeti watu wakasajiliwe. Sasa nataka kauli ya Serikali wanachi ya Vijijini kama hapa Mjini watu wanapanga foleni tunawaona NIDA wapo watu wanaenda kusajili, je huko Vijijini hali ni mbaya NIDA hawapo, hela hamna mitambo haiendi kwa wananchi leo watu wanateseka na simu ni kila kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunataka majibu ya Serikali kwanini wanawafanyia hivi watu wa Vijijini hususani watu wa Jimbo la Mlimba walifika tu pale makutano Kata ya Chita kwa uchache hawajafika Ching‟anda, Kalengakero, Mlimba, Kamwene, Utengule mpaka Tanganyika Masagati mpaka Uchindile NIDA mtafika lini kusajili huko hivyo vitambulisho vya watu mmeshawafungia simu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kikwazo naomba kuishauri Serikali sharti mojawapo ili usajiliwe unatakiwa uwe na cheti za kuzaliwa au cheti cha darasa saba kule kwangu wameamia wengi kutoka katika Tanzania hii hasa kwenye Kanda ya Ziwa wapo kule Vijijini wale watu wamezaliwa huko huko Vijini kabisa hamna hospitali, wale watu hawajasoma kama unavyojua tena wafugaji wameshakuwa wakubwa hawana cheti cha kuzali wala cha darasa saba ina maana hawa watu hawatasajiliwa mpaka milele nchini nchi hii. Hebu Serikali kaeni tuwaangalie hawa watu ambao katika hizo sifa mlizoweka hawatasajiliwa milele, je, mtawahesabu ni watanzania ama ni wakimbizi hebu naomba make mfikirie namna ya kuwasaidia hawa watu katika Vijiji hasa Jimbo la Mlimba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu TASAC tulipitisha Sheria hapa lakini mwaka jana 2019 wameleta amendments za Sheria mbalimbali zile, yaani ukishasikia Sheria mbalimbali zinakuja hapa ujue hapa changalamacho kwenye Kamati haiji tena ikija hapa inapishwa haraka haraka kumbe kwenye TASAC pamoja na kuwa tulipitisha Sheria mama kwamba TASAC itashughulikia masuala ya vitu ambavyo vya usalama wa nchi matokeo yake zile Sheria tulizopitisha za nyongeza 2019 wamesema inclusive ina maana bidhaa zote zinazopita bandarini TASAC watafanya talling hiyo ni hatari kwa sababu wanauwa kabisa suala la ubinafsishaji halitakuwa tena na mtu anayefanya talling kule bandarini kuna mlundikano wa mizigo kule bandarini..

MWENYEKITI: Ngoja taarifa Mheshimiwa Charles

T A A R I F A

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, msemaji anayezungumza anasema hawa watu hawajasoma, nampa taarifa tu kwamba hawajasoma lakini uzalishaji wanaweza.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiwanga unapokea taarifa hiyo?

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo ninaowatetea kwamba hawana cheti cha Darasa la Saba, hawana cheti cha kuzaliwa. Wamezaliwa vijijini, wamekulia machungani. Hawajui kusoma wala kuandika, kwa hiyo, hawatasajiliwa kwa sababu wamekosa sifa, hasa Wasukuma. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeenda kwenye TASAC…

MBUNGE FULANI: Hao ndiyo tax payers hao!

MHE. SUSAN L. KIWANGA: …matokeo yake kwa zile sheria tulizopitisha mwaka jana, 2019 za kuongezea ile sheria kubwa ya TASAC, imetokea hivi; wenye viwanda sasa, wafanyabiashara wakubwa wanahama kwa sababu wana gharama kubwa ya storage. Wale watu ambao wanaingiza mafuta labda, mtu anakaa bandarini mpaka miezi kadhaa hajatoa mizigo yake; watu wa madini wanaagiza vitu vya spare kwenye migodi, wanakaa siku kadhaa, meli zinakaa hapo; watu wanaona hiyo haiwezekani, wanaondoka…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana kwa mchango wako. (Makofi)

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari inakwenda kufa.