Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo

Hon. Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii awali ya yote nikushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuwa mmoja kati ya wachangiaji wanaochangia katika Taarifa za Kamati zetu tatu ambazo zimewasilisha Taarifa zao leo; Kamati ya TAMISEMI, Kamati ya Katiba na Sheria na Kamati ya Sheria Ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote niwapongeze sana waliowasilisha Taarifa hizi, wameziwasilisha kwa makini na zimeandaliwa kwa ubora, zimeeleweka na tunawaunga mkono na tunawapongeza kwa kazi kubwa wanazozifanya kwenye Kamati zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi ili iweze kuendelea inahitaji kuwa na amani, nchi ili iwe na amani inahitaji kuwe na Utawala Bora, ili kuwe na Utawala Bora tunahitaji sana kuwa na Sheria nzuri. Sheria nzuri zitagemea na wakati, kuna Sheria zilikuwa nzuri miaka ya nyuma lakini kadri tunavyokwenda mbele inabidi zibadilike ziende na wakati. Kuna Sheria ambazo sasa tunazo zinatusaidia ni nzuri sana lakini huko mbele tunakokwenda zitatakiwa zibadilike ili ziende na wakati na ndiyo maana tuna hizi Kamati kuzipitia Sheria zetu kwa wakati tofauti tofauti ili kuja na Sheria muafaka kwa wakati muafaka tulionao. Kamati zetu za Katiba na Sheria pamoja na Sheria Ndogo wanaifanya hiyo kazi kwa vizuri sana, nawapongeza sana. (Makofi)

Mhesheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala zima la Uraia pacha; uraia pacha kwa wakati tulionao, ninaiomba sana Serikali iuangalie kwa karibu. Naziomba Kamati zetu hizi husika hasa Kamati ya Katiba na Sheria iangalie kuingiza na kuifanya nchi yetu iwe na Uraia Pacha. Tunapozungumzia maendeleo, maendeleo lazima yawe shirikishi, tunaposema maendeleo shirikishi maana yake tunashirikiana sote wananchi tulio ndani ya Nchi na walio nje ya nchi. Kwahiyo, tunapoondoa hii Sheria inakua haipo kwetu, tunaacha kuwashirikisha kwa karibu kabisa Ndugu zetu ambao wanaishi nje ya Nchi. Kwa hiyo, naomba sana Kamati husika ziliangalie jambo la uraia pacha iwe ni Sheria inayokubalika hapa Tanzania pia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kuwashukuru sana Mheshimiwa Waziri Jafo na Manaibu wake wote wawili na Wizara nzima kwa ujumla, nimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuchika, Makamu wake pamoja na Wizara nzima kwa ushirikiano mkubwa ambao wametuonyesha sisi Wajumbe wa Kamati ya TAMISEMI. Tumeshirikiana nao vizuri katika kuwashauri, katika kuwaeleza na tunashukuru kwa kweli wamekuwa wasikivu sana. Serikali hii ni sikivu kupitia kwa Mawaziri wetu hao katika kuyatekeleza yale ambayo Kamati inawashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la MKURABITA; amelizungumza mwenzangu hapa jirani lkwa kipfupi. MKURABITA wakati unaanzishwa kwa maana ya kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge ili ziweze kuwasiaidia katika maisha yao. Amezungumza kwa uzuri kabisa kwamba watu wengi na sisi tumepata nafasi kama Kamati, tumetembelea sehemu nyingi, tumeona watu wakikabidhiwa Hati za Kimila katika mpango mzima wa MKURABITA ili ziweze kuwasaidia wao kujinyanyua kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme bado kuna Mabenki yanasumbua kuzitambua Hati hizi za Kimila katika kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo. Niombe sana Mheshimiwa Mkuchika na Wizara yako hebu mliangalie hili kwa karibu sana. Mabenki ambayo bado yanasumbua yapewe maelekezo ili wananchi waweze kufaidika na mali zao walizonazo. Maeneo fulani tumejenga mpaka vituo vya biashara lakini vinaonekana havifanyikazi kwa sababu watu wa kwenda pale na kufanya hizo biashara hawapo kwa sababu hawana fedha kwahiyo naomba sana mliangalie hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili; ameongea Makamu wangu Mwenyekiti hapa madeni ya Madiwani. Halmashauri nyingi Madiwani wanazidai halmashauri hawajalipwa fedha. Hivi tunavyoelekea mwisho Madiwani hawajui nini cha kufanya lakini tumshukuru sana Mheshimiwa Jafo ulizungumza kwa umakini na kwa ukali sana wakati tupo kwenye kikao cha Kamati, umetoa maelekezo. Naomba maelekezo hayo uyakazie ili kwa kweli tufikapo mwezi wa sita tusingumzie tena madeni ya Madiwani kwenye halmashauri zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nizungumzie kwa uchache kuhusu barabara; kweli barabara zipo, mvua zimenyesha na barabara zinaharibika tena kwa sabbau ya mvua. Niombe sana TARURA wajitahidi sana, waweze kuzirudisha barabara zetu katika hali ya kupitika ili mawasiliano yaendelee kuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa machache hayo, naomba niunge mkono hoja kwa asilimia 100 Kamati zote hizi tatu, ahsante sana. (Makofi)