Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru na mimi kuipata hii nafasi, lakini ninaiunga mkono kwa asilimia mia moja kwa vile huu mkataba au hili azimio itaisaidia kuifanya nchi iondokane na athari ambayo ilikuwa tayari inaangamia kutokana na climatic change au mabadiliko ya tabianchi ambayo Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi ambayo inaingia katika maangamizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kufanya hizi Hifadhi ya Ugalla na Hifadhi ya Kigosi kuingia katika hifadhi sababu zake kwanza Tanzania ilikuwa tayari misitu inatoweka, Tanzania wanyamapori walikuwa wanatoweka, hata uoto wa asili ulikuwa unatoweka, sasa kitendo cha kujikuta leo tunaazimia hili azimio ni imani yangu kuwa sasa hivi tunakwenda kubadilisha mazingira ambayo yalikuwa nchi inakwenda katika jangwa kuirudisha katika nchi ya kijani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni shahidi, Mikoa ya Singida, Dodoma, Shinyanga, Tabora kote huko ilikuwa tayari kumeshaingia jangwa kubwa sana kwa ajili ya watu walikuwa wanakata miti na ilikuwa sasa hivi mpaka Mikoa ya Lindi, Kusini kote misitu inatoweka, lakini sasa hivi TANAPA ina mbuga 20 wana matatizo makubwa ya kutozwa kodi nyingi ambazo zimeingizwa mle ndani. Je, mmewapangiaje kuwaondolea hizo kero ambazo itaifanya kuzitengeneza hifadhi zingine ambazo hazizalishi ili kuifanya hizi hifadhi zingine ziweze kuzitegemea zile hifadhi ambazo zinazalisha?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, leo hatuitegemei Ugalla katika muda mfupi huu kuweza kuzalisha wala Kigosi, Burigi na hizi hifadhi mpya hii ya Selous, lakini mkiwatengenezea mazingira ambayo itaifanya hii taasisi iweze kujiendesha mtakua mmefanya vizuri sana, lakini si hivyo tu, kuwaweka viongozi ambao wana uwezo. Tumezoea kuwaweka watu ambao hawana uwezo matokeo yake baada ya muda watu hawa watatoweka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo, Director General wa TANAPA amepewa hifadhi 20 kwa kweli tumpigie makofi huyu baba amefanya kazi ya ziada sana, ameweza kuifanya TANAPA kuweza kupata mapato na nchi hii kujivunia TANAPA kama eneo la kujivunia. Je, mmempa hizi hifadhi, mmemwekeaje mazingira yake, anastaafu niliongea katika Bunge lililopita, kama anastaafu mmejipanga vipi hao wanaotaka kuja ili angalau awaachie watu ambao mfumo mzuri ambao aliuendeleza ili uweze kuendelea vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mategemeo yangu kuwa Serikali isiangalie watu kwa ajili ya uzee, angalia leo Malaysia watu wazee ndio wanaiongoza Malaysia, siyo lazima kila mahali iwe kijana, hata mzee ukimuongezea muda akaisimamia hiyo kitu mtafikia mahali nchi hii tunakwenda vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninazungumzia suala la zebaki, hili azimio ni zuri, kwa sababu wachimbaji wadogo wadogo wote wanafanya uchenjuaji wao kandokando ya mito na kandokando ya mito tunategemea binadamu wanakwenda kulima, tunategemea kwenda kuchota maji kandokando ya mito, tunategemea wanyama kandokando ya mito kwenda kunywa maji, sasa contamination hii ya madawa ambayo yanatumika ya zebaki inatufanya Watanzania wengi tunaathirika, tuchukue Mikao ambayo kuna wachimbaji wanahamahama kila siku, athari yake si ndogo, ina maana miti yetu, mito yote inaingia katika maji machafu lakini siyo sababu lazima tupange mpangilio ambao na hawa wachimbaji wadogo wadogo, kwa vile ndiyo maisha yao, tuwe tumewawekea mazingira gani, lazima tuwe na shughuli mbadala ya kuwakabidhi au kuna kitu mbadala cha kuwasaidia hawa watu ili na wao wasiendelee kuwa maskini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana katika masuala ya mazingira, Serikali tuisimamie, tulikuwa na asilimia 20….
(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana. (Makofi)