Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba Kigosi Kuwa Hifadhi ya Taifa Kigosi pamoja na Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba la Igalla Kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury)

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba Kigosi Kuwa Hifadhi ya Taifa Kigosi pamoja na Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba la Igalla Kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi, na mimi ninaridhia Azimio hili la Mkataba wa Minamata kuhusu zebaki, namba moja kwa sababu ya madhara yaliyo makubwa sana kimazingira na kiafya katika jamii kutokana na matumizi haya ya zebaki na namba mbili ni kwa sababu matumizi haya ya zebaki nchini yako makubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, article namba 3 ya mkataba huu unaongelea masuala ya ni nchi kutambua ni kiasi gani cha zebaki ilichonacho na nimepitia leo asubuhi ripoti ya mazingira kwa mwaka huu inaonesha kwamba Tanzania kwa sasa tumeweza kutengeneza au kusambaza zebaki katika mazingira tani 33.5 ambayo kwenye Mkataba wamesema kwamba nchi inaweza inatakiwa isi-exceed tani 10 katika ku-generate zebaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, article namba 7 ya mkataba huu pia inaongelea kuhusu uchimbaji mdogo wa dhahabu ambao unatumia zebaki na hapa nchini kuna wachimbaji wadogo takribani milioni 1.5 na wengi wao wakiwa katika Ukanda wa Ziwa Victoria, kwa hiyo idadi ni kubwa wanaofanya shughuli za kiuchumi, lakini pia wanajiweka katika risk ya contamination wao wenyewe kujiharibia afya na walio wazunguka na mazingira pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuna umuhimu sana wa kuwafatilia nini ambacho Mkataba huu unaelekeza ili kuwasaidia wananchi kiuchumi na kuwapa alternative sources katika shughuli zao za uchimbaji wa dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo hapo article saba inasema kwamba nchi lazima itengeneze na kupitisha mpango kazi, au mpango mikakati, ni jinsi ya ku-deal na zebaki hususani katika wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, article namba 12 katika mkataba huu, unaelezea kuhusu mkakati kwamba nchi iwe na mkakati mahsusi wa kurekebisha madhara ambayo yametokea kutokana na zebaki katika mazingira, sasa nilikuwa nataka nisisitizie kuwa nimesema asilimia kubwa ya wanaotumia zebaki ambayo inaathiri mazingira ni katika Ukanda wa Ziwa na tunajua kwamba karibu asilimia 90 ya uchimbaji wa dhahabu uko katika Ukanda wa Ziwa na asilimia kubwa ya wachimbaji hao ni wale wadogo wadogo ambao wanatumia zebaki katika kuchenjua hiyo dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiria na lazima sasa tufate mwongozo wa huu mkataba kuangalia jinsi tunai-save vipi Lake Victoria yetu na wale ambao wanafanya shughuli za uchumi kuzunguka eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nisisitizie hapa article namba 13 inamuhusu Waziri husika ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wangu wa Bajeti kuhusu sasa hapo Mfuko wa Mazingira una kazi maalum na mahsusi, kwa hiyo, naomba Wizara ya Fedha wangekuwepo hapa waone kuwa tunaenda kuridhia mkataba huu sisi kama nchi, lakini mfuko wetu wa mazingira unasoma sifuri wakati tuna mambo mahsusi ya kimazingira ambayo yanatakiwa yafanyiwe kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo article 13 katika mkataba huu unaongelea kuhusu rasilimali fedha na utaratibu wa jinsi ya kutumia hizo fedha katika kurekebisha madhara au kutoa elimu kuhusu zebaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa naomba niguse kwenye article 16 ya mkataba huu unaongelea masuala ya afya. Shida ya hii zebaki katika afya zetu zinaweza zisionekane papo kwa hapo na madhara yake ni makubwa sana kwa sababu yanaenda kubadili DNA yako (vinasaba vyako) na pia yanakaa kwenye mazingira kwa miaka elfu na maelfu, haviondoki hivi hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna tayari ambayo wameshapata madhara ya kiafya kutoka kwenye zebaki basi naomba kuwe na mkakati mahsusi wa Kiserikali wa kuwa na vituo vya afya mahsusi na wanaotoa huduma mahsusi kwa wale ambao tayari wamepata madhara ya zebaki...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Ahsante kwa nafasi. (Makofi)