Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba Kigosi Kuwa Hifadhi ya Taifa Kigosi pamoja na Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba la Igalla Kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury)

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba Kigosi Kuwa Hifadhi ya Taifa Kigosi pamoja na Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba la Igalla Kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury)

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru pia kunipa nafasi ya kuweza kuchangia kwenye maazimio yaliyoko mbele yetu na nita- concentrate sana kwenye maazimio mawili, Maazimio ya Maliasili ambayo ni lile la kupandisha mapori ya Akiba mawili kwenye maeneo ya Tabora kuweza kuwa National Parks.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira kubwa ya maazimio haya natambua kabisa kwamba ni ya kuimarisha ulinzi wa maliasili zetu, lakini pia kufungua fursa za utalii kwenye maeneo ya Kanda ya Magharibi jinsi ambavyo tumekuwa na mkakati huo kuweza kupanua wigo wa utalii zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mapori mengi ya Mkoa wa Tabora yakiwepo haya ambayo yanaenda kuwa National Parks ikiwepo pia na mapori ya misitu mengi sana kutokana na kukosa ulinzi kwa miaka mingi iliyopita yalivamiwa na watu na baadaye baadhi ya maeneo vijiji vilisajiliwa kisheria na watu wakaendelea kuishi kule kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kwa mfano eneo linaenda kuwa Ugalla National Park ambalo kilometa 2065 ambazo zitaungana na zile kilometa 1800 kuweza kuwa National Park hizi kilometa 2065 zinatoka kwenye Msitu wa Ugalla North na kwenye huu msitu wa Ugalla North ndiyo eneo ambalo Kaliua wananchi vijiji vitatu vimo mle ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kijiji cha Zugimlole ambacho kuna vitongoji vyake, Kijiji cha Uyumbu na Kijiji cha Igombe na mwaka 2017 hapa Bunge liliagiza Wizara kuweka mipaka ya maeneo ya hifadhi na wakaanza ule utaratibu wa kuanza kuweka mipaka, lakini hawakushirikisha wananchi, nilivyolalamika Bungeni hapa wananchi wenyewe, Wabunge wengi wanalalamika Bunge likaagiza zoezi lile lisitishwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mipaka ile ilikuwa imewekwa kwenye miji ya watu na hivi tunavyoongea sasa hivi yaani zile beacon ziko kwenye miji ya watu, kwa hiyo tunakwenda kupitisha azimio hili lakini kuna baadhi ya maeneo kwenye Ugalla North ambapo bado wananchi wapo mle ndani, lakini ukiangalia pia hata maeneo ya Kigosi kuna watu walikuwa wanafuga misitu huku nyuki, kitu ambacho ni friendly na mazingira na kwa taarifa za Mheshimiwa Waziri peke yake ni kwamba kuna watu wamefuga kwa muda mrefu na kwa mwaka jana tu kuna watu waliosajiliwa mle ndani, watu wameweza kuvuna tani 701 ambazo zina thamani ya shilingi bilioni saba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lengo langu ni kwamba maeneo haya tunakwenda kuyapitisha kuwa National Park lakini bado kuna agizo la Rais pia ambalo aliagiza maeneo yote ambayo wananchi walikuwa wanabughudhiwa kwanza tutulie na akaunda Tume yake kuweza kuhakikisha kwamba maeneo haya yanapitiwa tuweze kupata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo langu naomba, pamoja na kuwa inaenda kupita, lakini lazima Wizara ituambie namna gani watu hawa ambao bado wako mle ndani watahakikisha kwamba waondolewa kiutaratibu ili wasibughudhiwe, kiukweli hatupendi maumivu haya yaendelee, hatupendi kabisa maumivu haya yaendelee kwa sababu ni kilio chetu cha muda mrefu na mpaka Mheshimiwa Rais amefikia hatua ya kuweza kuunda Tume anajua watu kabisa wako ndani ya Hifadhi, lakini waliingia baada ya kuwa mipaka ile ilikuwa pollars ilikuwa pia...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mimi naomba sana kwamba hilo liangaliwe, lengo letu ni kwamba kweli tuihifadhi kwa kupanua wigo wa utalii lakini pia wananchi wetu wasije wakateswa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaenda kuwapa pia TANAPA mzigo mkubwa sana kwa sababu tukianza....

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.