Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

Hon. Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

MHE. JOEL M. MWAKA: Mheshimiwa Spika, naomba niongelee kilimo cha umwagiliaji pamoja na wakulima wenyewe. kilimo cha umwagiliaji kwa Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati kwa ujumla kinategemea mabwawa. Mabwawa ya zamani sasa yanaelekea kutoweka kutokana na kujaa tope. Nimepata bahati mara mbili kuwapeleka Mawaziri kuyaona na kuzungumza na wananchi wanaolima. Kwanza nilikwenda na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji wakati huo, Mheshimiwa Engineer Kamwelwe; pili, nilikwenda na Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji sasa, Mheshimiwa Omary Mgumba. Ahadi zilizotolewa za kuyarekebisha Mabwawa ya Buigiri na Ikowa bado hazina mrejesho kwa wananchi, naomba mrejesho. Mabwawa mapya; ujenzi wa Mabwawa ya Membe na Kwahemu bado hakuna maendeleo mazuri, naomba mrejesho au taarifa.

Mheshimiwa Spika, mafunzo kwa wakulima; ili wananchi walime kwa tija kunahitajika elimu; elimu ya kilimo chenyewe, elimu juu ya afya ya udongo, ili waweze kulima mazao yanayostahili na ikibidi kutumia mbolea basi waweke mbolea inayostahili na elimu ya kilimo hai (organic agriculture). Naomba kuwe na vituo vya mafunzo ya kilimo kwa wakulima angalau kila kata au hata kila kijiji ambapo wanalima kilimo cha umwagiliaji kila baada ya miezi mitatu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.