Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

Hon. Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuunga mkono hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Naishauri Serikali ione haja ya kufanyia kazi maoni ya Kambi Rasmi kwa manufaa ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ningependa niishauri Serikali kuweka mkakati madhubuti wa kujenga mabwawa ya umwagiliaji na majosho ili kuepuka kilimo cha kubahatisha. Mfano ni Jimbo la Mlimba, shughuli kubwa ni kilimo cha mpunga, pia ndizi, cocoa, ufuta, mahindi, miti, maparachichi na kadhalika. Kila zao linastawi lakini Jimbo zima lina mradi mmoja tu wa umwagiliaji ambao hauna tija ingawa unatumia hela nyingi.

Ombi na kilio cha wananchi wa Njagi ni kujengewa bwawa ambalo litawawezesha kulima kwa mwaka mzima, tofauti na sasa hulima wakati wa mvua tu, mara moja kwa mwaka.

Mheshimiwa Spika, pia kwa kuwa Jimbo la Mlimba lina mito mingi inayotiririka mwaka mzima na maeneo makubwa yaliyokuwa yanatumiwa kwa kilimo yamechukuliwa na Maliasili kwa mradi wa bwawa la umeme Rufiji. Hivyo basi kuna umuhimu mkubwa wa Serikali kupeleka fedha kwa uchimbaji mabwawa na malambo ili wananchi wapate kilimo bora katika maeneo machache yaliyobakia vijijini ambapo itawezesha kupata ufanisi katika kilimo. Hivyo ningependa kupata majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Jimbo la Mlimba kuwa ni eneo la kilimo lakini kuna uhaba mkubwa wa wataalam wa kilimo; hivyo napenda kupata majibu ya Serikali; Je, ni lini Serikali itaajiri waghani na kuwapeleka Jimbo la Mlimba ili wakulima hao wapate tija katika mazao yao?

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo la Mlimba wana upungufu mkubwa wa mitambo ya kilimo. Mfano Gereza la Idete la kilimo pamoja na kuwa na maeneo makubwa ya kilimo lakini Serikali imewapatia trekta moja tu na kuwafanya washindwe kuyalima mashamba yote. Pia mitambo ya kuvunia ili kuwezesha kupata mazao bora na kuondosha upotevu wa mpunga kwa kutumia wafungwa kuvuna. Je, Serikali iko tayari kupeleka matrekta na harvester gereza la Idete? Je, Serikali iko tayari kupeleka matrekta katika Halmashauri ya Kilombero ili wakulima waweze kukopa na kuongeza mazao yao?

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo la Mlimba wanalima sana lakini mazao yao yanakosa soko kutokana na ubovu wa barabara. Kukosekana kwa soko, vikwazo vya Serikali kuweka zuio la kuuza nje ya nchi isipokuwa ndani ya nchi tu inamkandamiza mkulima kwani anatumia gharama kubwa na kuuza bei ndogo hivyo kumuongezea umaskini. Nashauri Serikali isiwe inamzuia mkulima huyo kuuza mazao yake nje ya nchi kwa faida, ahsante.