Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, hatuwezi kuondoa umaskini bila kuigusa sekta inayoajiri Watanzania wengi, hivyo basi, napendekeza kuondoa kodi kwenye Uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kuboresha na kukuza uchumi kupitia sekta hii.
Mheshimiwa Spika, wananchi walio wengi wanaojishughulisha na kilimo wameachwa na Serikali kujitegemea wenyewe. Serikali ingewekeza angalau asilimia 40 katika sekta hii, itasaidia katika kuboresha na kuimarisha/ kukuza mnyororo wa thamani (Agricultural value chain), na kwa jinsi hii itaweza kutengeneza ajira nyingi katika ngazi mbalimbali (vitongoji – wilaya – mikoa) na itakuwa na major impact katika nchi.
Mheshimiwa Spika, Serikali haijaweka wazi mikakati ya wazi ya kufungamanisha sekta ya kilimo, na sekta ya viwanda. Ni wakati sasa suala hili likaangaliwa katika upana wake.
Mheshimiwa Spika, Suala la Pembejeo Katika Ujumla Wake. Kuna uhaba na ucheleweshwaji wa kusambaziwa kwa Wakulima, ubora hafifu, kutokufika kwa wakati (msimu), bei kuwa juu kwa baadhi ya maeneo na kukosekana mfumo thabiti kuzuia pembejeo zisizo na ubora kwenye soko kwa kuzingatia haya. Wizara ifanye tathmini na kutengeneza mikakati mahsusi ya kuboresha haya.
Mheshimiwa Spika, Raslimali Watu Katika Sekta ya Kilimo. Kuna upungufu mkubwa wa wataalamu na maafisa ugani katika sekta hii. Hata kwa wafanyakazi waliopo (especially maafisa ugani) wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa ukosefu wa vitendea kazi. Wizara ilifanyie kazi suala hili.
Mheshimiwa Spika, Udhibiti wa Mazao Baada ya Kuvunwa (Post-Harvest Losses); hii husababishwa na:-
(i) Wakulima kuwa na elimu ndogo na miundombinu hafifu ya kutunza/ku-store mazao yao (na hata wakati mwingine kusababisha kutokea kwa aflatoxins) na (kuhatarisha afya za binadamu na mifugo);
(ii) Idadi ndogo sana za maghala za kuhifadhi (kati ya vijiji 13,000, kuna maghala mangapi?);
(iii) Teknolojia zinazotumiwa wakati wa kuvuna na kusindika ni duni sana, hii husababisha upotevu mkubwa wa mavuno (n20% ya mazao hupotea baada ya mavuno).
Mheshimiwa Spika, Kuimarisha na Kuboresha Mfumo wa Masoko (Ndani ya Nje ya Nchi). Changamoto ni nyingi na kusababisha hasara na ugumu wa maisha (hususan kwa wakulima wadogo). Wizara/ Serikali ijifanyie tathmini ili kuboresha suala hili.