Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia katika haya yafuatayo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali ilipanga na imepanga kuendelea kujenga Mabwawa na malambo kwa ajili ya kunyweshea wanyama (Mifugo). Je, ni lini sasa mabwawa na malambo hayo yatajengwa katika Jimbo la Kavuu Halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi?
Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wa kuhamisha ufugaji wa kuku wa kienyeji katika maeneo ya kijijini hasa katika maeneo ya vijijini kama maeneo ya Jimbo la Kavuu?
Mheshimiwa Spika, kupitia Wizara hii kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Wanyamapori iainishe mipaka kati ya hifadhi na matumizi ya mifugo.