Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Julius Kalanga Laizer

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Monduli

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Spika, ushauri wangu; tafiti zinaonesha Ranchi za Taifa ni takribani hekta 200,000, lakini ng’ombe wa Serikali ni chini ya 30,000 na hivyo ranchi hazitumiki ipasavyo. Nashauri tujifunze kutoka Botswana, Serikali ikodishe kwa unenepeshaji na wafugaji walipe kodi.

Mheshimiwa Spika, ranchi zote zinazomilikiwa na wakubwa zifanyiwe auditing ili zile zinazo-operate under performance zirejeshwe kwa wafugaji wadogo.

Mheshimiwa Spika, mashamba makubwa ya NAFCO ambayo hayajaendelezwa huko Simanjiro, Monduli Juu, West Kilimanjaro, yarejeshwe kwa wafugaji.

Mheshimiwa Spika, nashauri tozo ya 30,000 kwa ng’ombe export tax ipunguzwe iwe 15,000.

Mheshimiwa Spika, nashauri Wizara ifuatilie ng’ombe walioshikiliwa na maliasili maana wanakuta na wamekaa muda mrefu, hata baada ya kushinda kesi.