Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nataka kuanza kutoa inputs zangu katika Wizara hii kwa kujiuliza: Je, ni mafaniko yapi tunayo katika Sekta ya Elimu, ukiangalia… okay, samahani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni inputs gani tunaziona katika Sekta ya Elimu? Matokeo gani tunayaona katika Sekta ya Elimu kwa kuangalia shughuli za kiuchumi au shughuli za huduma za maendeleo ya jamii? Je, uchumi wetu una-reflect elimu tuliyonayo? Au huduma za kijamii kama ni afya, Madaktari wanatuhudumia vile tunavyotakiwa kupata? Sekta nyingine kama za Utalii, Service Provisions, zikoje? Je, zina-reflect kiwango cha elimu tulichonacho?
Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko ambayo yametolewa na Wajumbe ni mengi hata kwa Wizara nyingine zilizopita na hii yote ina-reflect level yetu ya elimu ikoje. Kwa hiyo, sitajikita sana katika kusema changamoto ni zipi za miundombinu, lakini changamoto ni zipi ukiziangalia katika outcome na jinsi ambavyo ina-affect elimu yetu kwa ujumla na uchumi wetu kwa ujumla? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika Sera ya Elimu yenyewe, katika kipengele cha muda wanafunzi wanaoanza shule, hii pia inaweza ikawa na outcome au ikaleta impact ambayo siyo sahihi. Watoto wadogo, miaka minne, mitano, mitatu, wanaamshwa saa 10.00 au 11.00 alfajiri, wamepumzika saa ngapi? Akili zikoje? Ukiangalia hata watoto wadogo wa Shule za Msingi Dar es Salaam, miundombinu hairuhusu wale watoto. Wanafika shuleni wamedumaa au hawana hizo akili, hawako creative. Kwa hiyo, chochote unachomfundisha yule mtoto hakiwezi kukaa, hiyo tayari ina impact katika siku za usoni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mitaala au curriculum zetu, ni masomo gani yanafundishwa? Kwa elimu ya sasa hivi, je, curriculum ipo sawa? Watoto wadogo wa primary school au nursery, content wanayofundishwa ni sawa? Watoto wanafundishwa mambo makubwa ambayo ni repetitive, ya kazi gani? Hii inaleta udumaivu au udumavu. Samahani sijui Kiswahili, hakiko vizuri sana, nayo ni reflection ya elimu yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia issue za mitihani ya primary au „O‟ Level, mwanafunzi au mtoto huyu anapewa one time chance, ambayo si sawa. Mtihani unafanya kwa siku moja mtoto wa Darasa la Saba, miaka yote saba inakuwa judged na siku moja. Hii lazima iwe reflected, haiko sawa. Au mtoto wa Form Four au Form Six, miaka yote hiyo minne au miwili aliyosoma inakuwa judged one time na chochote kinaweza kikatokea. Kwa hiyo, tunamnyima huyu mtoto nafasi au fursa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niguse kwenye issue ya Vyuo Vikuu na specialization. Tuna vyuo vya Serikali, naona hapa list inaonyesha vyuo 31. Ni chuo gani au vyuo hivi vikuu vime-specialize kwenye nini? Chuo Kikuu hakiwezi kuwa na faculties saba au nane. Hao wanaofundisha, wanaotoa huduma, hao Walimu wana qualities zinazotakiwa?
Kwa hiyo, lazima na hiyo nayo namshauri Mheshimiwa Waziri mhusika mwangalie specialization katika vyuo lazima iwe reflected inavyotakiwa na wataalamu wanaotakiwa wawepo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, issue nyingine ni miundombinu lakini kwenye njia ya ku-deliver elimu au kutoa mafunzo. Ni mbinu gani zinatumika kufundishia? Style tuliyonayo sasa hivi shuleni, hasa Shule za Serikali na hasa vijijini ni Mwalimu anaandika notes ubaoni na wanafunzi wanafanya kazi ya ku-copy. Kinachofuata ni ku-cram kile Mwalimu alichofundisha.
Sasa mtoto huyu anayefaulu, asilimia kubwa ni yule mwenye uwezo wa ku-cram halafu anakuja kutema baadaye kwenye exam. Hii nayo inakuwa reflected kwenye Vyuo Vikuu. Wanafunzi wanaokuja hawako creative, lakini tunaendelea kuwa na system za kukremisha. Sasa kama umejaliwa kukremisha ndiyo you have a better chance ya kufaulu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni vizuri kujiuliza au kujitathmini, tutaendelea hivi mpaka lini? Tutaendelea kusema madarasa hayatoshi, Walimu hawatoshi, miundombinu hafifu lakini tunataka nini? Serikali kama Serikali tuna strategy gani ya kusema kwamba elimu yetu i-focus kwenye nini ili izae kitu gani? Kwa hiyo, ni lazima tujiulize: Je, ni vipaumbele vipi tulivyonavyo, kama hivyo vipaumbele vipo na tunajiwekea nini katika elimu? Au imekaaje kimkakati ku-reflect uchumi wetu na nini tunataka kukijenga katika nchi yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi katika muktadha huo, naomba tujikite na tu-concentrate kuangalia kwamba elimu yetu ipo katika standard gani na tunataka ku-achieve nini na matokeo hayo ya elimu tunataka yaweje? Tu-focus kwenye impact au outcome ya mfumo mzima wa elimu tunataka uwaje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu kwa sasa. Ahsante.