Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, kwanza nakushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika Wizara hii ya Nishati. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika na kuwasilisha hotuba hii kwa umakini mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Bomba la Mafuta Kutoka Uganda – Tanga. Napenda kuipongeza Serikali na Wizara kwa kufuatilia kwa karibu sana juhudi za kufanikisha mradi huu wa bomba la mafuta kutoka Uganda – Tanga, Tanzania. Tuna bahati kubwa kupata fursa hii ya kipekee. Pamoja na vigezo kadhaa vilivyotumika kutupatia mradi huu lakini kigezo cha amani na usalama katika nchi yetu pia kinapaswa kuzingatiwa na Watanzania. Hivyo ni wajibu wetu Watanzania sote kupitia Serikali na Wizara kuilinda amani hii na kuthamini fursa hii tuliyopewa na jirani zetu.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu; katika jambo hili kwa Serikali ni kuendelea kuwashirikisha wananchi wote wa maeneo husika kwa kuwaelimisha faida na hasara zake. Wananchi wa maeneo hayo watakapopata elimu watajiweka katika nafasi ya kujiona kuwa bomba hili ni lao na watachukua hatua za kulilinda na kulienzi.

Mheshimiwa Spika, naunga hoja mkono.