Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika, naomba kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara hii ikiongozwa na Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Wakuu wa Taasisi zote zilizo katika Wizara hii kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.
Mheshimiwa Spika, Juhudi ziendelee za kutafuta vyanzo vingine tofauti vya kuzalisha umeme ambavyo viko hapa nchini. Vyanzo hivyo ni kama vile jotoardhi, umeme wa upepo, jua, maporomoka ya maji (hydropower) yaliyopo maeneo mbalimbali, urania na vinginevyo. Vyanzo hivi vitasaidia nchi yetu kuwa na uhakika wa umeme na wa kutosha vikisaidiana na miradi mikubwa inayoendelea kujengwa.
Mheshimiwa Spika, Mradi wa Umeme wa Rufiji ndio mkombozi na chachu ya maendeleo hapa nchini. Nichukue fursa hii kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uamuzi wa busara na wa kimapinduzi ambao utakumbukwa na vizazi vijavyo. Mradi huu utapunguza gharama za uzalishaji viwandani pamoja na kupunguza bei ya umeme kwa wananchi wetu maskini.
Mheshimiwa Spika, nawapongeza watendaji wetu wa kizalendo kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ya kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele wakiitikia wito wa kazi wa Jemedari wetu Mkuu, Kamanda wa maendeleo Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania; Mwenyezi Mungu awabariki Watendaji wote wa Wizara hii.
Mheshimiwa Spika, katika Jiji la Dodoma, kuna maeneo ya pembezoni hakuna umeme. Ninaiomba Serikali kupitia REA iwapatie umeme wananchi wa maeneo ya Kata ya Mbalawala, Kijiji cha Lugala, Kitongoji cha Matangizi na maeneo jirani ili wananchi wale wanufaike na umeme kwani wanapata taabu kwenda Nala kusaga nafaka zao na mahitaji mengine yanayotokana na huduma ya umeme. Hali hii ni shida kwao.
Mheshimiwa Spika, Mwisho, kazi yenu ni njema sana, chapeni kazi na TANESCO & REA iendelee vyema, kazi zake zinaonekana.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja asilimia mia moja.