Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Mwanakwerekwe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ALI SALIM KHAMIS: Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii na mimi kutoa mchango wangu wa maandishi kama ifuatavyo:-
Kwanza nianze na maradhi ya Corona. Ili kudhbiti ugonjwa huu mambo yafuatayo yazingatiwe:-
Mosi, kama Serikali imeamua shughuli za kijamii waendelee kama masoko, maeneo ya usafiri wa umma na kadhalika, wakati umefika sasa nikuzuia watu kutoka nje ya nchi, pia maeneo yaliyopatikana maambukizi yazuiliwe watu kutoka na pia kuingia.
Jambo la pili ni muhimu kuangalia upatikanaji wa vifaa vya uchunguzi pamoja na vifaa kwa ajili ya wauguzi na madaktari kuweza kujikinga na maambukizi wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa.
Tatu, katika Ofisi ya Waziri Mkuu iko haja ya kutenga bajeti ya dharura ili kukabiliana na janga hili kwani dharura inaweza kutokea wakati wowote.
Mheshimiwa Spika, nnem mwaka 2017 tulipitisha sheria ya mgawanyo wa wafanyakazi katika taasisi za Muungano asilimia 72 kwa 28 likiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano hadi sasa marekebisho ya wafanyakazi bado, naomba lifanyiwe kazi ili uwiano upatikane.
Tano, kutokana na janga la Corona Serikali iangalie ni namna gani kuangalia kuondoa kodi kwa biashara zote zilizoathirika kutokana na janga hili walau kwa miezi mitatu.
Mheshimiwa Spika, ni matumaini yangu kuwa ushauri wangu utafanyiwa kazi.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.