Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020

MHE. FAKHARIA SHOMARI KHAMIS: Mheshimiwa Spika, ahsante sina budi kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu na kukushukuru wewe pia na kukishukuru Chama changu cha Mapinduzi pamoja na UWT kwa kuniwezesha leo miye kuwa bado niko Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nitazungumzia ujio wa Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuja Zanzibar wakati wa kampeni. Amekuja Zanzibar kwa kweli tulimpokea kwa shangwe kubwa na tukakuweko pale Mnazi Mmoja tuliujaza uwanja na kwa kweli wananchi wa Zanzibar walifurahi na tunzo yao waliyoitoa kwamba majimbo yote ya Ugunja wamechukua na ngome ya Pemba tumeivunja na hadi hii leo tunakwenda kifua mbele Zanzibar, haya yote yalikuwa ni matunda ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kufika na kutuhamasisha na kutupa busara katika hotuba zake alizokuwa akituelezea pale Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 15 Mheshimiwa Rais alisema tunu ya Taifa, tunu ya Taifa kuna vitu alivitaja na hivyo na ndivyo vilivyotupa moyo sisi kule Zanzibar, ambapo alisema amani, umoja na mshikamano, uhuru wa nchi yetu, Muungano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli atakuwa karibu na atashirikiana sana na Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hilo la kwa Zanzibar tumelipokea na lilikuwa jambo la tunu kwetu na tumekubali katika tunu zake alizozisema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Bunge la Kumi na Mbili, wakati anakuja kutuhubia Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, alizungumza kwamba atashirikiana na akinamama kwa karibu na kwa kweli Mama Samia anafanya kazi nzuri na Mheshimiwa wetu na yeye ndiye aliyetupelekea akatuona kwamba wanawake tunafaa na akasema wanawake ukiwakabidhi dhamana ni watendaji wazuri na hii lazima tumpongeze kwa sababu yeye katuweka karibu, baadhi ya Mawaziri wanawake wapo na wanafanya kazi nzuri, Makatibu Wakuu wako wanafanya kazi nzuri ili kwetu sisi lazima tumlipe wema wanawake wote wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kwa nini tumeingia? Mheshimiwa alijitoa alitembea mikoa yote, na akatuletea kura za kishindo, leo humu ndani wengi wetu UWT tunatamba na tusingeweza kutamba kama sisi yeye Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kutupatia kura nyingi tukaweza kuingia humu Bungeni, hatuna la kumshukuru isipokuwa tufanye kazi nzuri akinamama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna lingine katika ukurasa wake wa 15 Mheshimiwa Rais alisema kwamba anampongeza Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuimarisha utawala bora hususan kwa kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma na kuzidisha mapambano dhidi ya ubadhirifu, rushwa, wizi, ufisadi na hili kwa Zanzibar ambapo yeye ameweza kuonesha njia kwa Bara na Zanzibar alivyokuwa amelizungumza hiliā€¦

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

MHE. FAKHARIA SHOMARI KHAMIS: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)