Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020

Hon Kassim Hassan Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanakwerekwe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020

MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote na mimi nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wa rehema na kutujalia kuwa wazima wa afya njema na kutuwezesha sote kuwa pamoja siku ya leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili nikushukuru wewe kwa kuweza kunipa nafasi ya kusimama katika Bunge lako tukufu kwa mara ya kwanza, pia nikishukuru chama changu Chama cha Mapinduzi kwa kuweza kunipa nafasi ya kuweza kuwakilisha wa Jimbo la Mwanakerekwe, naishukuru familia yangu pamoja na wananchi wa Jimbo la Mwanakerekwe kwa mashirikiano makubwa wanayonipa na nina wahaidi nitawatumikia Watanzania wote pamoja na wao kwa kuleta maendeleo mapana ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hotuba ya Mheshimiwa Rais ukitizama ukurasa wa 13 ameweka kipaumbele kikubwa katika miaka mitano kuendeleza, kulinda na kudumisha tunu za Taifa letu yaani amani, umoja na mshikamano wa nchi yetu, uhuru wa nchi yetu, pamoja na Muungano na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Pia kuhahidi mashirikiano na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, na kusisitiza kuwa hata kuwa na mzaa kwa yeyote atakayetaka kukatisha uhuru wetu Muungano wetu na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, hali ambayo imefanya mpaka sasa hivi kuunda kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika Kisiwa chetu cha Zanzibar na kuleta maendeleo ya uchumi katika Kisiwa cha Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 14 wa hotuba hii Mheshimiwa Rais ameonesha kuonesha mashirikiano makubwa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuendelea kuleta maendeleo ya pande zote mbili za Muungano na kuahidi kuleta meli nne katika Kisiwa cha Unguja. Hii imekwenda kufanya kugawanya usawa, usawa wa meli nne ziwepo katika Tazania Bara na meli nne zije katika Kisiwa cha Unguja inakwenda kutimiza lengo la sera ya uchumi wa blue.

Mheshimiwa Spika, pia utoawaji tumeona juzi tu utoaji wa hati, utiahaji saini wa hati wa yamakubaliano ya maridhiano katika ujenzi wa bandari kuu ambayo itajengwa na mji wa kisasa katika Kijiji cha Manga Pwani kule Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa katika hotuba yake na mimi nimalizie katika ukurasa 36 niipongeze Serikali kwa kutunga sheria mpya kusimamia na kuendeleza uvuvi wa bahari kuu; hii imekwenda kutuongezea ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi kwa vijana wetu ambao watakuwa wanajishughulisha na shughuli hizi na kufanya kwenda kuongeza Pato la Taifa letu la Tanzania, na mimi niunge mkono hoja na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa mashirikiano yake makubwa ambayo ameyaonesha katika kisiwa chetu cha Zanzibar na kufanya mikataba ambayo inakwenda ili iwe haki, uhuru na sisi kufanya Kisiwa cha Zanzibar kiwe kiwe kinamabadiliko makubwa katika miaka mitano inayokuja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana. (Makofi)