Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwanakwerekwe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Awali ya yote, nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai na uzima na kutuweka katika Mfungo wa Ramadhan tukiwa wazima na leo kushiriki katika Bunge lako hili Tukufu.
Mheshimiwa Spika, kwenye Ilani ya CCM, ukifungua kifungu cha 226 na 227 na ukurasa wa 276 – 277 inazungumzia mambo ambayo si ya Muungano lakini yanaleta faida katika kutatua changamoto za watu wetu zikishirikiana Serikali zetu mbili; yaani Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kwanza, niipongeze Wizara kwa kutatua baadhi ya changamoto kwa kuunganisha makampuni BRELA na BPRA. Memorandum ambayo wamefanya angalau inasaidia wafanyabiashara wakubwa wenye makampuni; mtu akiwa amesajili biashara yake Zanzibar, basi angalu wakija huku wanakubalika vile vibali vyao nao vinaweza kufanya kazi, niwapongeze kwa hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, vilevile, tukiangalia kwenye ZFDA na TBS wamefanya vivyo hivyo kwa kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo. Mtu akichukua biashara yake Zanzibar akija nayo Bara, basi nayo inakwenda bila usumbufu na cheti chao kinakubaliwa na jambo hilo linakuwa jema kwa wafanyabishara wetu wadogo wadogo. Niwapongeze kwa hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kidogo kuna shida moja, jambo hili tunaomba liende likafanyike katika TBS na ZBS. Tukizungumzia ISO kwenye standard katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tukienda kwenye codex inayotambulika ni moja tu; inatambulika TBS. Kwa hiyo, ZBS wanashindwa ku-recognize zile ISO ambazo wao wenyewe wanatakiwa waende wakazifanye kama ambazo wanazifanya TBS.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kitu kimesajiliwa Zanzibar; TBS inatakiwa iwasaidie ZBS angalau kitu kile kikitoka nje ya Tanzania basi na wao kiende kikatambuliwe kiufasaha. Kwa hiyo, watu wetu ambao wanafanya biashara ndogo ndogo Zanzibar wanakosa fursa ya kupeleka bidhaa zao nje kwa sababu tu ya haya mambo madogo ambayo yapo na yanaweza kutatuliwa kwa kufanya memorandum ambazo wenzetu wa ZFDA na TBS walifanya lakini walifanya hao wa BRELA na BPRA. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama kauli yetu ya Muungano ya safari hii inavyosema, “Muungano wetu ni msingi imara katika mapinduzi ya kiuchumi” basi twende tukawasidie wafanyabiashara hao wadogo wadogo na wao waweze angalau kulipata soko la nje ya Tanzania kwa kuweza kufanya biashara zao zikawa zinakwenda na wakiwa wanapata kipato cha mtu mmoja mmoja. Si haya tu na taasisi nyingine ambazo zinakwenda kufanya mambo kama haya ya ushirikiano, basi tuwaombe sana wazifanye hizi memorandum angalau kuwafanya watu hawa wote wawili waweze kufanya biashara sehemu yoyote ambayo itakuwa ipo bila matatizo yoyote. Ahsante sana. (Makofi)