Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Jang'ombe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, ahsante nashukuru kupata nafasi hii kwa ajili ya kuchangia katika Wizara yetu hii adhimu ni Wizara moja ambayo ina umuhimu mkubwa sana katika maisha yetu. Muungano wetu ni zaidi ya hapa ambapo kila mmoja wetu ametaja zile sifa.
Mheshimiwa Spika, nataka nimnukuu mwimbaji mmoja wa kizazi kipya anatokea kule Jang’ombe kwa Alinatu ni mtoto wa Khadija Kopa anaitwa Zuchu alisema kwamba “ladha yake msambaa shira ya kizanzibar” maana sasa hivi tayari… (Makofi)
SPIKA: Hebu iweke vizuri unajua Kiswahili huku bara na hasa Dodoma huku, ebu iweke vizuri tena amesemaje?
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, anasema ladha yake msambaa shira ya kizanzibar, sasa maana yake kwamba tayari katika Muungano huu nikijamii zaidi tumeshachanganyika kiasi ambacho hata kubagua huwezi tena ni sawa sawa na mchanga ambao umeuchanganya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru Wizara kwa kutaja haya mafanikio ambayo katika ukurasa wa 15 na 16 tulizungumza hapa mwaka juzi na mwaka jana, kwa kutosainiwa Mkataba wa SAUD BADEA ambao ulikuwa unahusisha shilingi za Kitanzania bilioni 26 kwa ajili ya barabara ya Chake Chake – Wete hivi sasa imeshasainiwa. Lakini pia tunashukuru kwa kusainiwa Mkataba pia wa Ukarabati wa Hospitali ya Mnazi Mmoja hilo nalo pia tunashukuru. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kupitia wewe kwanza nikushukuru wewe katika Bunge lako la 11 tulizungumzia hapa juu ya kutoa VAT katika umeme ambao TANESCO anauza kwa ZECO na kusamehewa deni la shilingi bilioni 22.9 na tulilizungumza hapa lakini tunashukuru Rais alilisikia na Mheshimiwa Rais Mungu amrehemu ampe mapokezi mema huko alipo, akasema analifuta deni lile na ile VAT imeondolewa, kwa hiyo, tunashukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna neno moja ambalo ninataka niseme haya tunayoyasifu yote hapa leo na tunapata nguvu ya kuyasifu, huko nyuma tulikuwa tukiyataja kama ni changamoto na yalipofanyiwa kazi badala yake ndipo yamegeuka sasa yamekuwa ni sifa na yamekuwa ni ufanisi na yamekuwa mazuri na yanasifiwa kila mahali. Kwa hiyo, na haya ambayo tunayoyataja leo kama ni changamoto isionekane labda tunasema vitu vya ajabu, vitakapopatiwa ufumbuzi tutakuja kukaa katika wakati mwingine tutakuja kusifu kama ni mafanikio ambayo yamepatikana na kwasababu mwanzo tuliyataja kama changamoto. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaomba Wizara ituchukuliwe, mimi ninaelezea changamoto moja, changamoto nayoelezea ni kuhusiana na bei ya umeme, lile jambo tulilozungumza kipindi kile lilikuwa lina component mbili; kulikuwa kuna VAT, lakini pia kulikuwa kuna bei ya umeme. Bei ya umeme ambayo TANESCO anaiuza ZECO ni bei ambayo ipo kubwa, bei ambayo inasababisha ZECO katika ku-pack zile bei za umeme aweze kuwafanyia wale wanaofanya biashara au watu wa viwanda apeleke mzigo mkubwa zaidi kwa kuwanusuru mtu mmoja mmoja au individuals ambao ni raia wa kawaida.
Mheshimiwa Spika, sasa bei ile inachosababisha; kama mtu ana kiwanda kule Zanzibar mfano kiwanda cha Soda Zanzibar Bottlers, na kama mtu ana kiwanda kule cha kukoboa kwa mfano kama vile Zanzibar Milling anaona bora atumie kiwanda kilichopo Tanzania Bara, na kile cha Zanzibar anakiacha kwasababu umeme analipa bei kubwa.
Mheshimiwa Spika sasa hicho ndicho kinachosababisha Zanzibar alikuwa na deni, pale wakati tunazungumza mwaka jana alikuwa na deni la shilingi bilioni 132, lakini deni hilo alilolikubali Zanzibar ni bilioni 65.7 ambapo hili amelipa bilioni 57.9, sasa limebakia takribani deni la bilioni saba. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini deni ambalo Zanzibar hajalikubali ni deni linalotokana na kilowatt Amps ambayo per unit TANESCO anaiuzia ZECO shilingi 16,000 lakini bei waliyokubaliana ni shilingi 8,000 ni double mara mbili zaidi. Kwa hiyo, hapo pana deni zaidi ya bilioni 66, sasa nini wazo langu ambalo ninalosema au maoni yangu au ushauri wangu, hili jambo katika ngazi ya watendaji alitujibu Waziri Mheshimiwa Kalemani mwaka jana kwamba tayari Wizara imekutana wameshazungumza wameshakubaliana lakini lipo katika desk la Muungano.
Mheshimiwa Spika, sasa tulikuwa tunaomba hili lifanyiwe kazi, na lifanyiwe kazi kwenye mambo mangapi? Kwenye mambo haya matatu ambayo ninayasema hapa sasa hivi, lifanyiwe kazi moja; hii bei ya kilowatt amperes ya 16,560 ibaki lilipwe lile lililokuwa la 8,647, ili hili lingine tunaomba lisamehewe. jingine bei ambayo imependekezwa sasa hivi na EWURA ya 157 ambayo ipo isitumike tunaomba bei ambayo ZECO wamependekeza ya kwa unit moja ikiwa ni kilowatts per hour 130 ikitumika bei hii itakuwa kutakuwa huko mbele hakuna mgogoro na hakutazalisha deni. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ombi lingine la tatu kusamehewa kwa hizi Bilioni 66.5 kwasababu zimetokana na bei ambayo imekuwa disputed sasa hicho ndicho ambacho tulichokuja nacho, kwa hiyo hii ni changamoto, changamoto hii inafanya kwamba ZECO asiweze kuendelea kuuza umeme tujue maingira ZECO imeme anavyoununua, anavyoupokea, anavyoupoza, alafu anaupeleka kwa wanachi yeye mwenyewe. Ukimuuzia kwa bei hii ambayo inafanana na ile ambayo mtu anapelekewa moja kwa moja nyumbani kwake au kiwandani kwake itakuwa haiwi-fare price na hapo ndipo kwenye mahusiano yetu na kuna kauli mbiu ambayo imesemwa hapa katika sherehe hii ya Miaka 57 ya Muungano. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwamba Muungano wetu ni msingi imara wa mapinduzi ya kiuchumi kama ni msingi imara ya mapinduzi ya kiuchumi uchumi huu utatokana na viwanda vikifungwa viwanda Zanzibar msingi huo utakuwepo?
SPIKA: Ahsante sana.
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, nashukuru naunga mkono hoja. (Makofi)